MAANA, AINA, DHIMA, SIFA YA MISIMU

     


    MAANA YA MISIMU:
  • Misimu ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. misimu inayodumu huweza kuingia katika methali, nahau au misemo ya lugha ya jamii hiyo.
    AINA ZA MISIMU:
  • pekee
  • kitarafa.
  • zagao
    SIFA YA  MISIMU:
  • Huzuka na kutoweka  kufuatana na mabadiliko ya jamii.
  • Ni lugha isiyo sanifu.
  • Ina chuki (kutoelewana) kwani maneno mengi yamebeba kebehi.
  • Ni lugha ya mafumbo.
  • Ina maana nyingi.
   DHIMA YA MISIMU:
  • Hutumika kupamba lugha.
  • Hutumika kukuza lugha.
  • Hutumika kutunza historia ya jamii fulani.
  • Hutumika kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji.
  • Hufurahisha na kuchekesha. 

      MATATIZO YA MISIMU:
  •        Misimu huleta msamiati wenye matusi: baadhi ya matumizi ya misimu huleta maneno yenye matusi katika lugha inayohusika , mfano, demu –msichana ambaye niwa muda tu.
  • ·             Misimu hupunguza hadhira: kutokana na misimu kuzushwa na kikundi kidogo cha watu , basi misimu hiyo hufahamika na kikundi hicho tu na hivyo hupunguza hadhira .
  • ·            Misimu ni lugha ya mafumbo na hufahamika na kikundi kidogo kinachotumia misimu hiyo: misimu kama lugha ya mafumbo si rahisi mtu asiye mwenyeji wa kikundi hicho kuelewa kile kinachozungumwa na kikundi hicho.
  • ·           Misimu huzuka na kutoweka: misimu ina tabia ya kuzuka na kutoweka  hivyo inakuwa na mchango sana katika kukuza lugha inayohusika.
  • ·          Misimu  imetiwa chumvi nyingi kwa hiyo haiamiki katika jamii: kutokana na hali hii hutegua mawasiliano.

 

Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

20 comments:

  1. ningeomba kwamba kwenye misimu mfafanue kwa mfano sifa mojawapo ya misimu inasema ;misimu ina chuki,mimi sijaielewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ina chuki (kutoelewana) kwani maneno mengi yamebeba kebehi.

      Delete
  2. ningependa kuuliza kama kuna matatizo yanayotokana na kutumia misimu?na kama yapo hayo matatizo je ni yapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. MATATIZO YA MISIMU:

      Misimu huleta msamiati wenye matusi: baadhi ya matumizi ya misimu huleta maneno yenye matusi katika lugha inayohusika , mfano, demu –msichana ambaye niwa muda tu.

      · Misimu hupunguza hadhira: kutokana na misimu kuzushwa na kikundi kidogo cha watu , basi misimu hiyo hufahamika na kikundi hicho tu na hivyo hupunguza hadhira .

      · Misimu ni lugha ya mafumbo na hufahamika na kikundi kidogo kinachotumia misimu hiyo: misimu kama lugha ya mafumbo si rahisi mtu asiye mwenyeji wa kikundi hicho kuelewa kile kinachozungumwa na kikundi hicho.

      · Misimu huzuka na kutoweka: misimu ina tabia ya kuzuka na kutoweka hivyo inakuwa na mchango sana katika kukuza lugha inayohusika.

      · Misimu imetiwa chumvi nyingi kwa hiyo haiamiki katika jamii: kutokana na hali hii hutegua mawasiliano.

      Delete
  3. maneno ambayo yanaweza kuwa mifano ya misimu kitarafa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Misimu kitarafa:
      hii ni misimu iliyovuka vitongoji na mji na kuenea maeneo mbalimbali:
      mfano futa- ni mtu ambaye hana akili timamu (misimu hii inapatikana vijiweni).
      1-cha hela - mpenda pesa ( misimu ya nyumbani).
      2- shegha- safi ( misimu hii inapatikana vijiweni).
      3- Bati - shilingi mia (misimu hii ni misimu ya pesa).

      Delete
  4. Replies
    1. Mfano ni baba wa taifa kumaanisha rais

      Delete
  5. Naomba kujua mofano zaidi ya misimu

    ReplyDelete
  6. Ni zipi vyanzo vya misimu

    ReplyDelete
  7. Ni zipi vyanzo vya misimu

    ReplyDelete
  8. Nataman kujua hoja 5 za dhima za misimu

    ReplyDelete
    Replies
    1. (a) huhifadhi siri ,(b) hupunguza hadhira ,(c) ni kitambulisho cha kikundi Fulani ,(d) hukuza lugha na (d) kupamba lugha na kadhalika

      Delete
  9. Asante umenisaidia mno

    ReplyDelete
  10. Asante lakini mbona misimu husanifishwa na kuingizwa katika lugha sanifu

    ReplyDelete
  11. Asante mno lakini naomba ufafanuzi wa kina sio juu juu

    ReplyDelete