Neno uambishaji linatokana na kitenzi kuambisha ambalo nalo latokana na
kitenzi kuamba. Kuamba maana yake ni kukifunga kitu fulani kwenye kitu kingine
ili kibakie hapo; au kukinatisha kitu fulani kwenye kitu kingine. Neno
kuambisha lina maana ya kukifanya kitu kinate mahali fulani.
Katika Kiswahili, uambishaji unafanyika
kwa kuongeza mofu fulani mwanzoni au mwishoni mwa mzizi wa neno. Kwa mantiki hii, maneno yanayoundwa hupewa maana ama
mpya, au ya ziada au hata yakageuza hali yake ya asili na kuchukua nafasi
nyingine katika muundo wa kishazi. Kinachoambishwa
huitwa kiambishi ambacho, aghalabu, hubeba maana katika lugha; na kwa mantiki
hiyo, kiambishi ni sawa na mofu.
Kwa mfano, katika neno piga, pig
ni mzizi, na a ni kiambishi/mofu
ishilizi au tamatishi katika kila kitenzi asilia cha Kiswahili.
Tunaweza kunatisha viambishi kadhaa mwanzoni mwa mzizi pig kama ifuatavyo:
tu-ta-m-pig - a,
lakini pia tunaweza kunatisha viambishi kadhaa mwishoni mwa
mzizi uo huo pig kama ifuatavyo:
pig-an-ish-a
au hata pengine tunaweza kuvinatisha viambishi
vya mwanzoni na vya mwishoni mwishoni mwa
mzizi huo huo pig na kupata tungo
kama ifuatavyo:
tu-ta-m- pig
-an-ish-a; au
tu-ta-m-pig - an-ish-a-je ? (na wenzake).
0 comments:
Post a Comment