Aina za Mofu


           
Mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili:
(i)     Kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu;
(ii)    Kigezo cha mofolojia ya mofu.

Tunapotumia kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu, tunapata aina tatu za mofu, yaani:
 (i)    Mofu huru
 (ii)   Mofu funge
 (iii) Mofu tata

Kwa upande mwingine tunapotumia kigezo cha mofolojia au maumbo ya mofu zenyewe tunapata aina mbili za mofu, yaani:
(i)     Mofu changamano
(ii)    Mofu kapa

Kwa mantiki hii tunazo aina tano za mofu ambazo ni:
(i)     Mofu huru
(ii)    Mofu funge
(iii)  Mofu tata
(iv)   Mofu-changamano

(i)     Mofu Huru
Mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yenye maana inayoweza kueleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine. Aghalabu, mifano mingi ya mofu huru hupatikana kutoka kwenye vipashio vya lugha, kama ifuatavyo:

(a)       Nomino:  {baba}, {kuku}, {sungura}, {ndege}, {dada}, {paka}, nk.

(b)       Vivumishi: {safi}, {baya}, {dhaifu}, {zuri}, {imara}, {hodari}, nk.

(c)       Viwakilishi:{mimi}, {sisi}, {wewe}, {ninyi}, {yeye), {wao}, nk.

(d)       Vielezi:  {upesi}, {haraka}, {sana}, {leo},          {jana}, {juzi}, nk.

(e)       Vitenzi: {tafiti}, {samehe}, {arifu}, {sali},         {jibu}, {badili}, nk.

(f)        Vihusishi: {ya}, {juu}, {mbele}, {kwa}, nk.
(g)       Viunganishi:{na},{halafu}, {bado}, {ila}, {aidha},{pia}, nk.
Kwa mujibu wa mifano hii inadhihirika kwamba Kiswahili kinazo mofu huru nyingi ambazo zimo katika aina zote za vipashio vya lugha. Hivyo, mofu huru ni mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yanayoeleweka bila kusaidiwa na viambishi.

(ii)       Mofu funge au Mofu tegemezi
Mofu funge au Mofu tegemezi ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa peke yake kama neno lililo na maana yake kamili; aghalabu mofu funge hutumiwa kama kiambishi tu kinachoambatanishwa na mzizi au viambishi vingine ili kulikamilisha neno husika. Mofu funge ina sifa zake ambazo ni pamoja na:

(a)    Mofu funge haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili.

(b)    Mofu funge ni lazima iambatanishwe na angalau mafu nyingine moja ndipo tupate neno kamili.

         Kutokana na sifa hii ndiyo mdiyo maana wanaisimu wengine huziita mofu hizi kuwa ni mofu tegemezi ambayo ina maana sawa na mofu funge

Mfano:
Idadi ya Umoja       Idadi ya Uwingi
m-toto (m)                 wa-toto (wa)
ki-su (ki)                    vi-su (vi)
m-ti (m)                      mi-ti (mi)

Ukumbwa wa Nomino        Udogo wa Nomino
ji-tu (ji)                                  ki-ji-tu (ki)
ji-su (ji)                                  ki-ji-su (ki)

Maana za mofu funge hutegemea sana muktadha wa mofu funge husika. Mofu funge ikiondolewa kwenye muktadha wake hukosa maana na ni vigumu kujua maana yake bila kuiweka katika muktadha wa neno. Mofu funge inaponing’inizwa peke yake haituwezeshi hata kidogo kujua maana yake. Umbo moja linaweza kuwa na maana nyingi kwa mujibu wa miktadha ambamo imeambatanishwa katika mzizi wa neno. Aghalabu, mofu funge ni sawa na viambishi vya mizizi mbalimbali katika neno. Hii ina maana kwamba viambishi vilivyo vingi katika lugha huwa ni mofu funge. Tunasema viambishi vingi kwa sababu si viambishi vyote ambavyo huundwa kwa mofu funge. Vipo viambishi vingine ambavyo huundwa kwa mofu huru. Baadhi ya mizizi ya maneno pia huwa ni ya mofu funge kwa sababu mizizi hiyo huwa haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili. Mifano mizuri ya mizizi ya maneno ya Kiswahili ambayo huundwa kwa mofu funge ni ile ya vitenzi vya silabi moja moja, kama ifuatavyo kwa mfano:

Mofu funge               Neno                   Mofu funge        Neno
            {l-)                  kula                            {-p-}               mpe
            {-j-}                kuja                            {-ny-}            kunya
            {-f-}                kufa                            {-nyw-}          kunywa
            {a}  +  {me}  +  {m}  +  {nyw}  +  {esh}  +  {a}  amemnywesha

Mizizi ya vitenzi hivi ni mizizi ya mofu-funge kwa sababu haiwezi kutumiwa peke yake kama neno na, pia maana zao huwa hazijitokezi mpaka mizizi iwekewe viambishi.

(iii)   Mofu Tata
Mofu tata ni mofu ambazo huwa na maana zaidi ya moja au kuanzia mbili na kuendelea.

Mfano:
Saidi alimpigia Mbaraka mpira.
Sentensi hii ni tata kwa sababu ina maana zaidi ya moja.  Utata wa sentensi hii haupo kwenye muundo wake wa kisarufi, bali upo katika kitenzi alimpigia.  Kitenzi hiki kina mofu sita, yaani:
{a-} + {-li-}  + {-m-} + {-pig-} +  {-i-}   + {-a}
  1            2             3             4               5             6

Kati ya mofu hizi zote sita, mofu ya tano {-i-} ndiyo yenye utata. Mofu {i} ni mofu ya kutendea kwa sababu tukisema: ‘Saidi alimpigia Mbaraka mpira’, maana zinazoweza kueleweka na wasikilizaji ni nne:
 (a)   Saidi aliupiga mpira kwa niaba ya Mbaraka; yaani Mbaraka ndiye aliyetakiwa aupige mpira ule, lakini kwa sababu ambazo hazikuelezwa, badala ya Mbaraka kuupiga mpira ule, Saidi akaupiga.

(b)    Saidi aliupiga mpira kuelekea kwa Mbaraka; yaani Saidi na Mbaraka walikuwa wakicheza mpira. Ikapatikana fursa, Saidi akaupiga mpira ule kuelekea kwa Mbaraka. Kwa hiyo, hapa tunazungumzia mwelekeo wa mpira.

(c)    Saidi alimpiga Mbaraka kwa kuutumia mpira; yaani, Saidi anautumia mpira kama ala (silaha) ya kumpigia Mbaraka.
 (d)   Saidi alimpiga Mbaraka kwa sababu ya mpira; yaani hapa, mpira ndio sababu kubwa ya Saidi ya kumpiga Mbaraka. Tuseme labda Saidi alikuwa na mpira wake, halafu Mbaraka akauchukuwa kuuchezea na kwa bahati mbaya akaupoteza. Saidi anapogundua kwamba Mbaraka ameupoteza mpira wake, basi ndipo akampiga.

Kwa maelezo hayo, ni wazi kwamba sentensi yetu ina utata kwa kuwa inatupatia maana tofauti tofauti zipatazo n’ne ambazo zimesababishwa na mofu {-i-} ya kutendea.

(iv)      Mofu Changamani

Mofu changamani ni mofu ambazo huundwa kwa kuweka pamoja angalau mofu-sahili mbili au mofu funge na mofu sahili yakafanyiza neno lenye kuleta maana kamili, kwa mfano:

Mofu sahili + Mofu sahili
(i)        {askari} + {kanzu} = askari kanzu.                     
           
(ii)       {gari} +  {moshi} =  gari moshi.

(iii)     {paka} + {shume} = paka shume.
(iv)      {m’mbwa} + {mwitu} = m’mbwa mwitu.
           
(v)       {fundi}  +  {chuma} = fundi chuma.
nk.

Mofu funge   +   Mofu huru    
                       
(i)        {mw} + {-ana}+       {nchi}            =  mwananchi.         

(ii)       {ki} + {-on-} + {a}  +          {mbali}=  kiona mbali.

(iii)     {mw} + {-ana}+       {hewa }=  mwanahewa.
             nk.

(v)       Mofu Kapa
Mofu kapa ni mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno, lakini athari zinazotokana na hiyo mofu kapa husika hueleweka. Ingawa mofu hizi huwa hatuzioni wala kuzitamka au kuziandika, lakini maana zake tunazipata. Tukichunguza ruwaza ya viambishi awali vya umoja na wingi katika lugha ya Kiswahili, tunaweza kuzigawa nomino za Kiswahili katika makundi makuu man’ne, yaani:


 (a)      Nomino zilizo na viambishi bayana vya idadi ya umoja na uwingi:
                               
            Mfano:
            Umoja            Wingi
            m - tu              wa - tu
            m - toto           wa - toto
            m - ti               mi – ti
            nk.

(b)       Nomino zilizo na kiambishi awali cha umoja tu, cha wingi hakipo, kwa hivyo, ni kapa  (φ)
   
            Mfano:          
            Umoja                        Wingi
u - kuta                       φ - kuta
            u - funguo                  φ - funguo
            u – kucha                  φ – kucha.
            nk.

 (c)      Nomino zilizo na kiambishi cha wingi tu, cha umoja hakipo; kwa hivyo, ni kapa  (φ)

Mfano:
            Umoja                        Wingi
            φ – kasha                 ma – kasha.
            φ – debe                    ma – debe.
            Φ – jembe                 ma - jembe
            nk.

(d)       Nomino zisizo na kiambishi awali cha umoja wala cha wingi

            Mfano:
            Umoja                        Wingi

            Φ - mama                   Φ - mama.
            Φ - ng’ombe              Φ - ng’ombe.
            Φ - baba                     Φ - baba.       
            Φ  - kaka                    Φ - kaka.
            Φ - dada                     Φ - dada.
            Φ - mbuzi                  Φ - mbuzi.
            Φ - ngamia                Φ  - ngamia.
            Φ  - kondoo               Φ  - kondoo.
            Φ  - tembo                 Φ - tembo.
            Φ  - sungura              Φ  - sungura.
            Φ  - nguruwe             Φ  - nguruwe.
            Φ  - simba                  Φ  - simba.
nk.
(e)       Sherehe kuhusu Mofu kapa

Katika kuonyesha mofu kapa tutatoa sherehe kuhusu kundi la 1.2.5.3 na la 1.2.5.4. Katika kundi la 1.2.5.3 nomino zina kiambishi awali cha umoja tu, wakati cha wingi hakipo. Kinachotokea hapa ni kwamba ukisema ukucha watu wanaelewa kuwa ni ukucha mmoja tu. Lakini ukisema kucha,  watu wataelewa kuwa ni kucha nyingi.

Na hali hii ndivyo ilivyo kwa maneno ufunguo ǂ funguo; ukuta ǂ kuta, nk. inajulikana kuwa ni ufunguo mmoja tu na akisema funguo, ni kwa maana ya wingi; lakini umbo  lenyewe linaloileta hiyo maana ya wingi halionekani bayana katika neno.

Ili kuyaeleza haya maumbo ambayo hayapo lakini maana zinazowakilishwana maumbo hayo zipo, Wanaisimu wamekubaliana kuyaita maumbo  haya kapa, yaani mofu ambazo hazipo. Mofu hizi ni             dhahania tu katika akili zetu kwa kufahamu tu kwamba maana fulani haiwezi kuja tu yenyewe lazima iletwe na mofu fulani. Kwa hivyo, hata kama mofu hiyo haionekani, lakini ipo; ni mofu-kapa.

Kwa mfano, katika matamshi ya maneno: kasha, debe, jembe, umoja na uwingi wake hudhihirishwa kama ifuatavyo:

Umoja                        Uwingi
kasha                          makasha
debe                            madebe
jembe                         majembe

Katika nomino hizi mofu ya uwingi ni mofu  {ma} lakina mofu ya    umoja ni mofu kapa, yaani haipo na huoneshwa kwa alama {Φ}.

Kwa mantiki hiyo, mofu za maneno haya ni kama ifuatavyo:

Umoja                        Uwingi
{Φ} + kasha              {ma} + {kasha}
{Φ} + debe                {ma} + {debe}
{Φ}+jembe               {ma} + {jembe}





MAREJELEO



Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N. (2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili, Kidato cha 5 na 6.  Aroplus Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.


leksimu inaweza kuwa neno si kila leksimu ni neno wala kila neno sio leksimu Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

13 comments:

  1. kazi nzuri ya kusaidia

    ReplyDelete
    Replies
    1. asante kwa maoni yako karibu tena kwa maswali na usauli

      Delete
  2. hogera ustadhi kazi zuri hiyo imenisaidia kupata umilisi wa lugha katika mofolojia juu ya mofimu kapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. asante kaka karibu tena tunaomba uwataarifu wengi huwepo wa swahili form blog waweze kupata elimu

      Delete
  3. hongeara ustadhi umenisadia sana umilisi unao

    ReplyDelete
  4. Replies
    1. asante kaka karibu tena tunaomba uwataarifu wengi huwepo wa swahili form blog waweze kupata elimu

      Delete
  5. nilikua nataka ufafanuz juu ya dhana ya leksimu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Cystal (1980) anaelezea kuwa leksimu
      ni kipashio dhahania kinacho wakilisha maumbo kadhaa yanayotokana nacho.

      Kwa mfano;
      refu – ndefu, mrefu, kirefu
      baya- baya, mbaya, wabaya

      Delete