Fasihi Simulizi
|
Fasihi Andishi
|
|
a)
|
Umri: Ina umri mkubwa kuliko fasihi andishi. Pengine huitwa fasihi kongwe.
|
Ina umri mfupi kuliko fasihi simulizi. Hii inatokana na ukweli kuwa
maandishi yamegunduliwa hivi karibuni.
|
b)
|
Uhifadhi: Inahifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya
masimulizi.
|
Inahifadhiwa kwa maandishi na kusambazwa kwa njia ya maandishi.
|
c)
|
Tanzu: Ina tanzu mbalimbali, lakini ni tanzu nyingi kuliko zile za
fasihi andishi: sanaa za maonyesho, ushairi, nathari n.k.
|
Ina tanzu tatu tu: ushairi, tamthilia na riwaya
|
d)
|
Uwasilishaji: Huwasilishwa kwa njia ya simulizi ya mdomo. Hutegemea
sauti
|
Huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
|
e)
|
Mabadiliko: Hubadilika kulingana na mfumo wa kihistoria. Aidha, fanani anaposimulia hadithi anaweza
kuongeza au kupunguza jambo kila pale anapowasilisha sanaa yake. Pia, fanani
akifa na kazi nayo italazimika kubadilika kutokana na yule atakayechukua
nafasi yake.
|
Haibadiliki baada ya kuandikwa.
|
(f)
|
Wahusika: Wahusika wana uwezo wa kuchukua
majukumu mawili kwa wakati mmoja. Mfano mhusika mtu anaweza kuwa pia mnyama.
Wahusika wafuatao wanatambulika. (i) Msimuliaji (ii) Wasikilizaji
(iii) Wanyama (iv) Vitu na Mahali.
|
Kwa kawaida wahusika hushika jukumu moja kwa wakati mmoja. Wahusika
wanaweza kuwa watu au wanyama au hata vitu, kama vile mti, jiwe, mwezi, nk..
|
(g)
|
Umiliki: Jamii nzima ndiyo inayohusika.
|
Umiliki: Mtunzi wa kazi hiyo ndiye anayehusika.
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu
|
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
nzuri kabisa
ReplyDeleteasante sana kwa ufanisi huu wa tanzu za fasihi.
ReplyDeleteIko vizuri sana
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteAsante kwa maarifa hayo
ReplyDeleteWell done!!!!!!
ReplyDeleteFasihi andishi ina tanzu tatu tu..........??? hio hoja (C)
ReplyDelete