MAMBO YANAYOSABABISHA LAHAJA KUTOKEA NA



MAMBO  YANAYOSABABISHA  LAHAJA KUTOKEA NA YANAYODHOOFISHA LAHAJA :

  • Utengano  wa kijiografia: kuna mambo yanayosababisha watu  wanaozungumza  lugha moja kutengana  kimahali na kimielikeo. Makitengana mawasiliano yao hupungua . kwakuwa mawasiliano  ni haba, kuna uwezekano mpana wa watu walioachana  kukuza upekee wa namna Fulani katika usemaji wao. Kwa hivyo, msingi wa upekee wa usemaji au kuzuka  kwa  lahaja utengano wa kijiografia.

  •  Utengano  wa kitabaka: katika jamii moja kunaweza tabaka mbalimbali za watu . kila tabaka hujihisi na kujitambulisha kwa namna ya pekee japokuwa matabaka hayo huishi katika eneo moja. Msingi wa mwachano wa kitabaka hunaweza kuwa  uchumi, dini,elimu,au siasa . kwa sababu ya mwachano wa kitabaka, mawasiliano ya mara kwa mara baina ya watu wa tabaka mbalimbali hupungua. Na mawasiliano ya mara kwa mara yakipungua nafasi ya kuchipuza upekee hata katika usemaji hupanuka . hivi ndivyo vianzavyo vipengele vya usemaji vifungamanavyo na tabaka.

  •   Utengano wa kiwakati: wakati ni kipengele muhimu katika kuzuka kwa lahaja. Umbali tu hautashiuwe wa kijiografia au kitabaka. Hata baada ya wasemaji wa lugha moja kutengana kwasababu ya hiki au kile, upekee katika usemaji hauzuki mara moja. Hutokea taratibu kadri wakati unavyopita. Kipengele cha wakati ni muhimu vilevile katika ukuzaji wa lahaja za kijamii au za kitabaka.

MAMBO YANAYODHOOFISHA LAHAJA :

  •   Maendeleo ya njia za usafiri kama : vile barabara,reli,mitumbwi,televisheni,magazeti nk. vyombo hivi huwakutanisha watu pamoja huunda waliotengana kiografia na matokeo ya kukutana huko husababisha kusawazisha hata namna yakusema, maana za za maneno.n.k.

  •   Maendeleo ya njia za upashanaji habari kama: vile redio,televisheni,magazeti,n.k. vyombo hivi vya upashanaji habari huunda umoja wa pekee miongoni mwa watumiaji kwa vile wote huathirika na mawazo na usemaji wa namna moja kwa  wakati mmoja.

  •   Kuwepo chini ya utawala au dini moja: dini na utawala ni vitu vyenye kukazia umoja miongoni mwa raia au wafuasi wake. Umoja wa aina yoote ni kichocheo cha ukaribiano katika usemaji.

  •   Usanifishaji: husababisha baadhi ya lahaja kudumaa.

  •   Biashara na dini: hivi pia ni vitu ambavyo huwakutanisha watu pamoja.
Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

1 comments:

  1. nimeelewa vizuri kuhusu mambo yanayodhoofisha lahaja asnteniii

    ReplyDelete