NGELI ZA NOMINO:
Ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika mpangilio au kupanga nomino katika makundi yenye nomino zinazofanana. Mfano maneno mtoto na mjomba yako katika ngeli moja, kwa sababu katika umoja, yote yanaanza na m huku vitenzi vyake vikianza na a.
AINA ZA NGELI ZA
NOMINO:
Kwakuzingatia kigezo cha upatanisho wa kisarufi, kuna ngeli
tisa za nomino.ngeli hizoni:
1.
NGELI
YA a-wa :
Ngeli hii inajumuisha majina ya viumbe hai,kama vile watu,
wadudu.
Kwa mfano:
Njiwa anapaa.
– Njiwa wanapaa.
2.
NGELI YA
u-ya:
Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi
awali u- katika umoja na ma-
katika wingi.
Mfano:
Uuaji umedhibitiwa – Mauaji yamedhibitiwa.
3.
NGELI
YA u-zi.
Ngeli hii inajumuisha majina yenye viambishi awali u-
na w- katika umoja zi- katika katika wingi:
Mfano:
Wembe umevunjika
- Nyembe zimevunjika.
4
.
NGELI
YA u-i:
Ngeli hii inajumuisha majina ya baadhi ya sehemu za
mwili,kama vile mikono, miguun.k.
Mfano:
Mguu umepinda.- Miguu imepinda.
5
.
NGELI
YA li-ya:
Ngeli hii inajumuisha majina ambayo yana kiambishi awali li-
katika umoja na ya- katika wingi:
Mfano:
Gari limeanguka -
Magari yameanguka.
6.
NGELI
YA ki-vi:
Ngeli hii inajumuisha
majina ya vitu visivyo hai.kama vile kisima, kitanda.
Mfano:
Chuma kimepinda. – Vyuma vimepinda.
7.
NGELI
YA ku-:
Ngeli hii inajumuisha majina yote yanayotokana na
kunominishwa kwa vitenzi. Kama vile kusoma.
kwa mfano:
Kulala kunasaidia.
8.
NGELI
YA i-zi:
Ngeli hii inajumuisha majina ambayo ayabadiliki umbo katika
umoja na katika wingi.
Mfano:
Njia ina majani. – Njia zina majani.
9.
NGELI
YA pa/mu/ku:
Ngeli hii inajumuisha majina yanayoonesha mahali.
Mfano:
Mahali pale palitumikaa.
Mahali mule mulikodiwa.
Mahali kule kunauzwa
0 comments:
Post a Comment