UPATANISHO WA KISARUFI:


Ni hali ya viambishi vya maneno ndani ya tungo kukubaliana na kushikamana ili kuleta maana iliyokusudiwa. Upatanisho wa kisarufi unaweza kuonekana kati ya vipashio mbalimbali vya tungo:


MFANO:(A) NOMINO NA KITENZI:
Kwa mfano:Unyasi umeota   =    Nyasi zimeota.


(B) NOMINO NA KIVUMISHI:
Kwa  mfano:Kiazi  kitamu.  =   Viazi vitamu.


(C) KIWAKILISHI NA KIVUMISHI:
Kwa mfano:Huyu mnene.   =   Hawa wanene.


(D)KIWAKILISHI NA KITENZI:
Kwa mfano:Huyu anakuja.  =   Hao wanakuja.


(E)  NOMINO NA MZIZI WA AMBA :
Kwa  mfano :Mtu ambaye.  =  Watu  ambao.


(F)  NOMINO NA KIREJESHI:
Kwa mfano:Mtu aliyesafiri. = Watu waliokatwa.
 

  jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu.    




Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

1 comments: