Mzizi , Shina katika kitenzi.

Mzizi wa kitenzi 

ni sehemu ya neno inayobakia mara baada ya kuondoa viambishi vyote vya awali na tamati katika neno hilo.

Mfano: - a-na-chez-a {-chez-}, m-ku-lim-a {-lim-}

Aina za mzizi.

Mzizi funge ni ule ambao hauwezi kujikamilisha kimaana yaani hauwezi kusimama kama neno.

Mfano; -lim-, -chez-, -imb- n.k.


Mzizi huru ni ule ambao huweza kusimama kama neno na ukichanganuliwa zaidi hupoteza maana yake ya msingi.

Mfano; Kinu, Kazi, Arifu, Sali n.k.


Shina la kitenzi 

ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi fuatishi (tamati) au ni sehemu ya neno ambayo hubakia baada ya kuondolewa viambishi tangulizi.

Mfano:- chez+a = cheza, lim+a = lima. Sehemu hii ya neno hutumika kuundia neno jipya.

Aina za shina.

Shina sahili – hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo ni mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu huru,

Mfano; Kesho, jana, kitabu, jarida n.k.


Shina changamano – shina hili huundwa na mzizi na kiambishi tamati maana.

Mfano; cheka, lala, lia, kula n.k



Shina ambatani – shina hili huundwa na mofimu mbili ambazo ni huru.

Mfano; mwana + kwenda = mwanakwenda, mbwa + mwitu = mbwamwitu

Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment