UHAKIKI WA VITABU



FORM THREE BOOKS.


Click here 👉 UHAKIKI WA ENGLISH BOOKS

FORM TWO BOOKS


__________________________________________________


TAMTHILIYA YA KILIO CHETU
MTUNZI: MEDICAL AID FOUNDATION
WACHAPISHAJI: TPH
CHAPA YA 1: 1996


UTANGULIZI
KILIO CHETU ni tamthiliya inayojaribu kuvunja ukimya uliotawala 
miongoni mwa wanajamiii katika kutatua matatizo mbali mbali 
yanayotokana na mahusiano ya kijinsia, matatizo ambayo yasipopata 
ufumbuzi thabiti yanaweza kuliangamiza taifa.

MAUDHUI :

DHAMIRA

i) ELIMU YA JINSIA
Hii ni dhamira ambayo imetawala katika tamthiliya hii ambapo 
wazazi na walezi wengi inaonesha wako tayari kuvunja ukimya uliopo 
kati yao na watoto wao na kuzungumza waziwazi juu ya mahusiano 
ya kijinsia.Baba na Mama Anna na mjomba wahusika hawa 
wamejitoa mhanga ili kuwanusuru watoto wanaoathirika na ugonjwa 
hatari wa UKIMWI kwa sababu ya kukosa elimu.
Baba na mama Anna wanapeana majukumu ya kuongea na watoto 
(baba na watoto wa kiume na mama na watoto wakike) kama uk 10 
unavyoeleza. “Baba Anna:hili ndilo nimefaulu 
mwenzenuNimekwambia,Mama Anna akae na mabinti zake”.Kwa 
upande mwingine kuna wazazi na walezi ambao wanaamini kuwa 
kuwaeleza watoto ni kuvunja mila na desturi pia ni kuwafundisha 
umalaya.Mama Suzi na baba Joti wanawasilisha kundi hili wao 
wanaamini kuwa viboko na vitisho ndio njia sahihi ya kuwafunza 
watoto tabia njema.
Matokeo ya misimamo yote miwili imeonekana bayana kwenye 
tamthiliya hii ambapo,watoto waliopata elimu mfano Anna 
wanajieleza na wana majibu sahihi kuhusu mahusiano ya jinsia 
na wale wasio na elimu mfano Joti na Suzi wanapata maradhi mfano 
Joti alipata Ugonjwa wa UKIMWI na Suzi anapata mimba.kutokana 
na hali hii elimu ya jinsia ni jambo muhimu sana kwa maisha ya 
jamii ya sasa,kuendeleza mila kuna liangamiza taifa letu 

(ii) MAPENZI KATIKA UMRI MDOGO 
Mwandishi ameonyesha jinsi vijana wanavyoshiriki mapenzi katika 
umri mdogo,jambo hili ni hatari katika maisha yao.Matokeo ya jambo 
hili ni kupata mimba za utotoni na maambukizi ya virusi vya 
UKIMWI.Msanii amewatumia wahusika Joti na Suzi kama waathirika 
na mapenzi katika umri mdogo.Aidha ameonyesha pia tabia ya vijana 
wadogo kushiriki ngono na watu waliowazidi umri,hali hii pia inazidi 
kuwaingiza kwenye hatari ya kupata magonjwa.Joti ana mahusiano 
ya kimapenzi na chausiku (mtu mzima)ambae pia ana mpenzi wake 
mpemba(uk 23).
Suala la mapenzi katika umri mdogo (kujamiiana)linachangiwa na 
kuzagaa kwa picha za X na picha za utupu zilizozagaa mitaani(kwenye 
magazeti,mitandao nk).Vijana na watoto wengi hupenda kuangalia 
vitu hivyo na kujikuta wakishawishika kufanya ngono .


(iii)MALEZI
Suala la malezi limezungumziwa katika mitazamo tofauti tofauti 
ambapo kuna wanaoamini kuwa malezi ya watoto ni kuwapiga viboko 
na kuwatisha,mwandishi amewatumia mama Suzi na baba Joti 
ambao wanaamini kuwa viboko vinaweza kuwaadabisha watoto wao,
matokeo ya mtazamo huu ni watoto kuwa na nidhamu ya woga na 
kushindwa kuyakabiri majaribu mfano Suzi anashindwa kumkatalia 
Joti kufanya ngono na matokeo yake anapata mimba 
Aidha kuna wazazi ambao wanaamini malezi bora kwa watoto ni 
kuwaelimisha na kuwapa mifano halisi ya maisha badala ya 
kuwatisha,Mjomba,baba na mama Anna wanaamini mfano huu.Anna 
ameelimishwa na kuelimika hakuna anayemdanganya mfano 
anamweleza Mwarami kuwa kwa sasa wanatakiwa kuzingatia 
masomo na si vinginevyo.
Aidha anamweleza Mwarami madhara ya ngono katika umri mdogo 
pia ni pamoja na kupata magonjwa kama kaswende,kisonono na 
UKIMWI hivyo wasiogope mimba tu kama walivyodanganyana wao 
kwa kupeana vidonge vya kuzuia mimba .
Hivyo suala la malezi litazamwe kama jukumu la jamii nzima na kila 
mwanajamii aone kuwa ana wajibu wa kushiriki malezi.


(IV) UKIMWI NA TIBA YAKE
Mpaka sasa hakuna tiba kamili ya UKIMWI ambayo imethibitishwa 
kinachotolewa mpaka sasa ni dawa za kupunguza makali ya virusi 
vya UKIMWI pamoja na magonjwa nyemelezi (ARV).Dawa hizi 
hutolewa kwenye vituo vya afya vilivyoidhinishwa na serikali au 
mamlaka husika.Pamoja na hayo kumekuwapo na matangazo kadha 
wa kadha kwenye magazeti, runinga au mabango yanayoeleza kuwepo 
kwa watu wanaodai kutibu UKIMWI, ukweli utabaki kuwa hakuna 
tiba kama mwandishi alivyoeleza (uk 34), ugonjwa huu hauna tiba 
ushahidi upo wazi kwani kadri tunavyoona watu walioupata ugonjwa 
huu, tunajua ukweli kwa hiyo matangazo yanayotolewa mengi 
hulenga kutuongezea matatizo na pengine kuleta uhasama miongoni 
mwetu.


(V) NAFASI YA MWANAMKE
katika jamii zetu za kiafrika mwanamke hutazamwa katika sura 
tofauti mathalani katika tamthiliya hii mwanamke ameonyeshwa 
katika sura tofautin kama ifuatavyo;
Mosi,malaya,mtazamo huu umethihirishwa na chausiku ambaye 
licha ya kuhusiana kimapenzi na joti alikuwa na mpenzi mwingine. 
(mpemba muuza duka).Suzi naye licha ya kuwa mwanafunzi wa shule 
ya msingi alijihusisha na uzinzi. 
Pili,Mnyonge hana sauti,mwanamke pia ameonyeshwa kama mtu 
duni na asiyefaa,asiye na sauti ya kutetea haki zake zote.Mfano 

mama joti baada ya kubaini mume wake kutokuwa mwaminifu 
anashindwa kumuuliza badala yake ananunua khanga kuwasema 
wabaya wake.
Tatu,Mlezi wa familia,mwandishi ameonyesha kuwa mwanamke ni
mtu muhimu sana katika malezi mfano,mama suzi yuko mstari wa 
mbele kumlea mwanawe suzi na kuhakikisha anafuata njia njema 
impasayo mtoto mwema. Mama Anna naye ameonyesha kumlea vema 
bintiye Anna na kumwezesha ashinde vishawishi toka kwenye jamii 
inayomzunguka.
Nne,Mwenye msimamo thabiti,mwanamke pia ameonekana kuwa 
mwenye msimamo katika maamuzi yake,Mfano Anna anapotongozwa 
na mwarami anajibu kwa ujasiri kuwa wao bado ni wanafunzi 
wazingatie masomo anasikika akisema “ya nini kukimbilia suti na 
nepi hujavaa”.
Tano,mshauri,katika tamthiliya hii mwanamke ameoneshwa kama 
mshauri bora,mfano Anna anamshauri suzi kutotoa mimba bali 
amueleze mama yake kuhusu swala hilo.

(VI) MAPENZI NA NDOA
Mwandishi ameonyesha kutokuwepo kwa uaminifu katika suala la 
mapenzi na ndoa kwa ujumla.Baba Joti ameoneshwa kuwa na 
wanawake wengi.Joti na Chausiku wana wapenzi zaidi ya mmoja hali 
inayohatarisha maisha yao hasa kipindi hiki cha ukimwi hivyo 
uaminifu ni muhimu sana katika mapenzi.

MIGOGORO

Katika tamthiliya hii kuna migogoro mbalimbali imejitokeza ambayo 
ni;
Mosi,mgogoro kati ya Suzi na mama yake,Chanzo cha mgogoro 
huu ni vidonge vya kuzuia mimba kwenye sketi yake ya shule jambo 
ambalo mama yake hakiliafiki na suuhisho ni mama suzi 
kumwadhibu Suzi.
Pili,mgogoro kati ya mama Suzi na mjomba,Chanzo cha mgogoro 
huu ni tofauti za mtazamo kuhusu elimu ya jinsia,mama Suzi 
aliamini kuwa kumwelimisha Suzi kuhusu mahusiano ya kimapenzi 
ni kumfundisha umalaya,mjomba anapingana na hilo kwa 
kumwambia mama Suzi viboko havisaidii
Tatu,mgogoro kati ya Joti na Chausiku,Chanzo cha mgogoro huu 
ni tabia ya Joti kuwa na wasichana wengi na kutumia vitu vya 
Chausiku kuwahonga wasichana wengine,suluhisho ni Chausiku 
kumkalipia joti.
Nne,mgogoro kati Mwarami na rafiki zake,(Chogo,Joti na Jumbe) 
wanamlaumu Mwarami kutochangamka na kuwa na mpenzi 
wanamwambia kama hachangamki watamtoa umemba.Kauli hiyo 
ilimfanya Mwarami amfuate Anna na kumtaka kimapenzi.
Tano,mgogoro kati ya Anna na Mwarami,Chanzo cha mgogoro 
huu ni tofauti za misimamo,Mwarami anataka Anna akubali kufanya 
ngono,Anna anakataa na kumweleza kuwa wasome kwanza mambo 
ya ngono yana muda wake.

UJUMBE

 Si busarakuchanganya mapenzi na masomo kwani kufanya 
hivyo huleta madhara(Suzi alipatamimba ,Joti alipata UKIMWI)
 Elimu ya jinsia ni haki na stahiki si halali kwa watoto 
(vijana)kuwanyima elimu hiyo kwani kufanya hivyo ni
kuwaangamiza
 Wazazi wabadilike kulingana na wakati wasing‟ang‟anie mila 
ambazo haziisaidii jamii.
 Elimu stahiki kuhusu UKIMWI itolewe kwa wanajamii wote ili 
wasihusishe UKIMWI na mambo ya kishirikina.
 Wazazi wavunje ukimya na wao bayana kuhusu mabadiliko ya 
miili yao ili iwe rahisi kushinda majaribu mbalimbali
FALSAFA 
Mwandishini anaamini kuwa kuwapa watoto elimu ya jinsia ni 
kuwafanya wajitambue na kujielewa barabara na kuepuka madhara 
ya kujiingiza kwenye ngono katika umri mdogo.Elimu ndio njia pekee 
ya kuwaepusha dhidi ya VVU/UKIMWI.

FANI

MUUNDO

Mwandishi wa tamthilia ya KILIO CHETU ametumia muundo wa moja 
kwa moja (msago),mchezo unaanza sehemu ya kwanza ambapo 
dubwana linaingia kisiwani.
 Sehemu ya pili na ya tatu tunajulisha kifo cha fausta na Suzi 
kujihusishwa katika mapenzi na kukutwa na vidonge vya 
kuzuia mimba.Na katika sehemu hii mjomba anawaeleza wazazi 
wa Suzi na Joti elimu ya jinsia kwa vijana.
 Sehemu ya nne watoto wanajihusisha ngono na wasichana 
wanaowazidi umri kama Chausiku Aidha mtoto Anna 
anaonyesha jinsi alivyopatiwa elimu kuhusu jinsia hivyo 
kushindwa vishawishi
 Sehemu ya mwisho Suzi anagundulika kuwa ana ujauzito wa 
Joti ambaye amedhihirika kuwa ana ugonjwa wa UKIMWI 

MTINDO

Mwandishi ametumia baadhi ya vipengele vya sanaa za maonyesho ya 
kiafrika.
Mfano;
 Matumizi ya nyimbo (uk 21 na 25)
 Kiongozi; tunaangamia x4
Wote;tunakwishwax2
(wanainuka huku wanaendelea na wimbo)

 Pia mwandishi anatumia mwanzo na mwisho wa hadithi ambao 
ni mwanzo wa hadithi za fasihi simuluzi mfano 
„Paukwa........pakawa
Mtambaji:niendelee nisiendelee
 Wote: endelea 
 Mwandishi pia ametumia mtindo wa monolojia pale mtambaji 
anapotoa maneno ya 
utangulizi kuhusu 
matendoyanayohusika/yanayotokea
 Pia kuna matumizi ya dayalojia yenye maneno machache lakini 
yaliyopangwa kwa ufundi na ustadi mkubwa .


MATUMIZI YA LUGHA 

Mwandishi anaonyesha ustadi mkubwa katika matumizi ya lugha 
inayofanya wasomaji watafakari kwa makini ametumia lugha nyepesi 
inayoeleweka kwa walengwa(watu wa kawaida) ambao ni watoto na 
wazazi(walezi).Lugha iliyosheheni tamathali za semi ,misemo nahau 
matumizi ya lugha za kiingereza na lughaya kiasili(kibantu)na pia 
matumizi ya taswira 

TAMATHALI ZA SEMI 

Tashbiha
 Walipukutika kama majani(UK 1)
 Miti inayoungua kama mabua(UK 6)
 Mbona unakuwa mgumu kama mpingo(uk 5)
 Unakuwa nyuma nyuma kama koti 

Sitiara
 Ndio mwisho wa kumvumilia huyu nguru anaechimba ndoa 
yangu(uk2)
 Huyu kinyago wako anakimbia nini?(uk 20)

Tashihisi
 Huyu kinyago anakimbia (uk 20)

TANAKALI ZA SAUTI 
 Wacha moyo nipute pwi pwi(uk16)
 Basi vup nikamdaka(uk 16)
Takriri
 Pigadomo ,piga domo( uk 16)
 Watu watapukutika kama majani ya kiangazi 
 Hodi hidi mwenye nyumba (uk 13)

Misemo
 Na wewe utakuwa nyuma kama koti (uk 4)
 Mtakatifu wa usoni (uk 9)
 Mapenzi ni tiba (uk 22)
 Kukimbilia suti na hali nepi hujavaa (uk 20)
 Kukausha (uk 9)
 Anadunda (Uk 8)
 Umekula wa chuya (Uk 25)
 Makapera kibao (Uk 7)
 Kujikaza kisabuni (Uk 21)

 Kushika hatamu (Uk 22)

Methali
 Wembamba wa reli treni inapita (Uk 6)
 Shukrani ya punda ni mateke 
 Asiyefundwa na mamaye hufundwa ulimwengu (Uk 30)

Nahau
 Kufa kwa kukanyaga miwaya (Uk 9)

LUGHA YA KIINGEREZA NA LUGHA YA ASILI
Kwa kiasi kidogo mwandishi anachanganya lugha ya kiingereza na 
Kiswahili kutambulisha namna ya vijana wengi wa siku hizi 
wanavyoongea kwa kuchanganya lugha. Mfano 
JOTI;Ndio umecome sio?,maneno mengine ni 
 Stori (uk 16)
 Umemba(Uk 24)
 Gest(Uk18)
 Chips(Uk16)
 Tuition(Uk 21)
 Mabuku(Uk1)
 Mwandishi ametumia lugha ya asili katika wimbo wa 
maombolezo
 Kiongozi:Jiti afitwe sanda salauyax3
 Wote:Ena,ena,ena salauya
 Kiongozi :umwana afitwe sanda x3
 Wote :ena,ena,ena salauyax3

UTEUZI WA TASWIRA
Mwandishi ametumia taswira la dubwana lililoleta balaa kisiwani (Uk 
1)mwandishi anasema kila aliyegusa wakaharisha mara nywele 
kunyonyoka na vifo vikafuataHaya ni maelezo yanayofanya msomaji 
ajenge woga na kupata picha halisi ya dubwana yaani UKIMWI

MANDHARI
Mwandishi ametumia mandhari ya mjini hii imedhihirika pale jirani 
aliposema „mie toka siku ile niwaone pale shamba sijakaa tena 
mjini,nilienda zangu shamba kupambana na nyani wala nafaka‟
Pia sinema za xzinadhihirisha mandhari ya mjini 
Jumbe:leo si ndio picha
Choggo:ndio tulisahau(Uk 7)
Pia Anna anapoimba (Uk 20)anasema‟pesa zenu,lifti zenu niache 
mie‟wimbo huo umedhihirisha mandhari ya mjini kwani lifti kwa 
wakina dada hasa wanafunzi zinapatikana mjini kuliko vijijini.

WAHUSIKA
MAMA SUZI
 Ni mhusika mkuu msaidizi 
 Mama yake suzi

 Ana msimamowa kizamani kuwa mzazi hawezi kuongea na 
mwanae maswala ya kujamiiana au elimu ya kijinsia haamini 
kuwa watoto wadogo wanaweza kujihusisha na mapenzi
Mfano Fausta alikuwa mtoto mdogo wa darasa la tano mambo hayo 
asingeyajua anaamini kuwa njia pekee ya kumfunza mtoto ni 
kumuadhibu.

SUZI
 Ni mhusika mkuu 
 Ni mtoto wa mama Suzi,
 Ni binti mdogo wa darasa la sita aliyejihusisha kimapenzi na 
Joti kinyume na matarajio ya mama yake.
 Alikutwa na vidonge vya kuzuia mimba,
 Hakupatiwa elimu ya kijinsia na wazazi wake,
 Anapata mimba kutokana na wepesi wa kushawishika

BABA JOTI
 Ni jirani yake mama Suzi bado ameshikiria ukale kwamba 
wazazi hawawezi kukaa na watoto wao kuwaeleza habari za 
ngono anaamini kuwa dawa pekee ya kuthibiti ni viboko na 
mijeledi (Uk 21)sio mwaminifu katika ndoa yake kwani ana 
mwanamke mwingine nje ya ndoa.

MAMA JOTI
 Ni mke wa baba Joti 
 Anaamini kuwa watoto wangejua makubwa kwa kutumia 
methali „wembamba wa reli treni inapita (Uk 6).
 Ndoa yake matatani kwa kuingiliwa na nyumba ndogo .anafikiri 
suluhisho la tatizo ni kununua kanga za mafumbo.

MJOMBA
 Kaka yake na mama Suzi 
 Ana uelewa mpana na upeo wa kufahamu mambo ya 
ulimwengu wa sasa ulivyo hivyo anashauri watoto wapatiwe 
elimu ya jinsia hawatajihusisha na mambo ya kujamiiana 
mhusika huyu anafaa kuigwa na jamii.

BABA ANNA
 Ni jirani yake na baba Joti 
 Pia ana upeo wa kuelewa mambo na anamwambia mkewe 
(mama Anna)akae na watoto wao na kuwaelimisha kufamya 
mapenzi katika umri mdogo.
 Anaamini wapo watoto wataelimishwa kamwe hawatajihusisha 
na kujamiiana.

JIRANI
 Ni jirani yake na baba Joti,
 Hana uhakika na vipimo vya hospitali anashauri Joti apelekwe 
kwa fundi(waganga wa jadi) kwa tiba.
 Anawakilisha watu wengi ambao hawaamini kuwa kuna 
UKIMWI na mtu akiupata ni kwamba amerogwa.
 Hafai kuigwa katika jamii.

ANNA
 Ni msichana mdogo ambaye bado ni mwanafunzi amepata 
elimu ya jinsia na wazazi wake.
 Huyu ana msimamo na maamuzi ya haraka kuhusiana na 
maswala ya kujamiiana mfano Uk21......hujui kama kuna 
madhara mengine....hujui kisonono na mengine kedekede
 Kutokana na elimu ya jinsia aliyopewa kuepukana na kushinda 
vishawishi vingi.
 Pia ni mshauri mzuri, alimshauri suzi asitoe mimba kwani ni 
hatari (uk 20)
 Anafaa kuigwa katika jamii

JOTI
 Ni mwanafunzi wa shule ya msingi anasoma darasa moja na 
Suzi,
 Ana uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi akiwemo 
Suzi,Chausiku,Yoranda,Gelda na sikujua ,
 Alipata UKIMWI kwa sababu wazazi wake hawakumpatia elimu 
ya jinsia yaathari za kujamiiana.

JINA LA KITABU 
Jina la kitabu KILIO CHETU linasadifu maudhui yaliyomo ndani
,mwandishi ameonyesha kilio cha watoto wakiwalaumu wazazi na 
walezi wao kwa kutowapatia elimu ya jinsia ili waweze kujikinga na 
janga hili la UKIMWI.Hiki ni kilio cha jamii nzima „wimbo huu 
unathibitisha
Kiongozo:tunaangamiax4
Watu:tunakishax2
Pia wimbo wa maombolezo kutokana na kilio chetu juu ya janga hili 
la UKIMWI hSWA WATOTO
KIONGOZI:Joti afwite sanda salauyax3
WATU:Ena ena ena salayax3.



UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA ORODHA
Mtunzi:Steve REYNOLDS
Mchapishaji:Macmillan
Chapaya 1:2006


UTANGULIZI
ORODHA ni miongoni mwa tamthiliya ambazo zinaonyesha namna 
jamii hususani watoto na vijana wanavyoangamia kutokana na 
UKIMWI.Vijana wengi wanaangamia kwa sababu ya ukosefu wa elimu 
sahihi kuhusu UKIMWI hali hii yaweza kusababisha ongezeko la 
waathirika,Binti mdogo furaha kwa kutokujua athari za UKIMWI 
anajiingiza kwenye vitendo vya ulevi na uzinzi kama alivyoshauriwa
na rafiki yake Marry na kujikuta akipata UKIMWI mapema hivyo ni 
vyema asasi kama za dini zihusike katika kutoa elimu hiyo.


MAUDHUI

DHAMIRAKUU : MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
Mwandishi wa tamthiliya hii amezungumzia kwa kina suala la 
ugonjwa wa UKIMWI haswa kwa mazingira ya vijijini,mwandishi 
amebainisha kuwa chanzo kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI ni 
umasikinina ukosefu wa elimu sahihi kuhusu VVU/UKIMWI.Pia 
mmomonyoko wa maadili,kukosekana kwa uadilifu,
ukimya/kukosekana kwa uwazi na hata upendo wa kweli.
 Mwandishi licha ya kuzungumza mambo haya kuwa chanzo cha 
UKIMWI,ameonyesha mambo ambayo kama yatazingatiwana jamii 
inaweza kujiepusha na janga hili la UKIMWI,mambo hayo ni kama 
ngono salama,uadilifu,elimu,uamiifu,ukweli,upendo,uelewa 
na 
uwazi.Kwa ufupi ni kwamba endapo jamii itazingatia hayo UKIMWI 
utakwisha, pamoja na dhamira hiyo kuu ya mapambano dhidi ya 
UKIMWI ,dhamira nyingine ni :-

1.  KUKOSEKANA KWA ELIMU 
Ujinga humfanya mtu akose maarifa ya kupambana na 
maisha.Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha kuwa ujinga na 
ukosefu wa elimu ya VVU/UKIMWI ni kikwazo cha mapambano dhidi 
ya ugonjwa huu,elimu hii itolewe kwa watu wa vijijini yaani wajue 
UKIMWI ni nini,unaenezwa vipi ,unaweza kuepukwa vipi,huduma 
kwa wagonjwa iweje na je tiba ipo?
 Mwandishi ameonyesha kuwa kwenye kijiji anachoishi binti 
Furahahajui UKIMWI ni nini,rejea na mazungumzo ya wahusika hawa;
Mwanakijiji wa kwanza :Ndio lakini kwenye ofisi ya daktari kaambiwa 
anaugonjwa wa AIDS
Mwanakijiji wa 4:hicho si kitu kizuri
Mwanakijiji wa 1:wanauita slimu kwa sababu ugonjwa wenyewe 
unakondesha
Mwanakijiji wa 3:lakini unawezaje kupata ugonjwa kama huo?
Mwanakijiji wa 1:nahisi kuna mtu kamroga pengine rafiki msichana 
mwenye wivu
Mwanakijiji wa 2:nasikia unapata kwa kugusana tu
Mwanakijiji wa 4:au hata kwa kuwa nao chumba kimoja

2 . UMASIKINI 
Umasikini ni hali ya jamii kukosa mahitaji muhimu katika tamthiliya 
hii umasikini umeonyeshwa kama sababu ya wasichana kujiingiza
kwenye vitendo vya ulevi na akina bwana Ecko ili wapate vitu vizuri 
kama vile viatu,magauni na begi.Umasikini humfanya mtu ashindwe 
kufanya maamuzi ya busara.Ili kufanikisha zoezi la kupambana na 
UKIMWI ni vema kwanza wanakijiji wakawezeshwa 
kiuchumi.Mwanandishi ameonyesha kuwa mwanakijiji akikombolewa 
kiuchumi atashiriki vema kupambana na UKIMWI.

3 . MMOMONYOKO WA MAADILI 
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha namna jamii inachangia 
maambukizi ya VVU/UKIMWI 
Mfano:furaha na Marry wanatoroka usiku na kwenda kwenye ulevi 
(baa) na hata kujihusisha katika vitendo vya uzinzi kama kauli ya 
baba yake anavyodhihirisha “anilichokuwa nafahamu....na hadi sasa 
Furaha .......ni kwamba amekuwa akitoroka nyumbani usiku wa 
manane ......kutoroka bila ruhusa .....baa .... „wanaume” “wewe”..... 
“Malaya”....asiye na shukrani‟‟
Mmomonyoko wa maadili pia umedhihirishwa kwa watu wazima 
ambao wamekabidhiwa majukumu muhimu katika jamii kama Padri 
James ni miongoni mwa watu waliopoteza mwelekeo na kujiingiza 
katika uzinzi na waumini wakeHoja hii imedhihirishwa na padri 
James mwenyewe anasema “Furaha alikuja kama alivyoagizwa na 
.....ee.....Ekaristi takatifuilipatikana,lazima uelewi jinsi ilivyo vigumu 
kwa mtu wa hadhi yangu na wadhifu wangu.......?
 Kwa ufupi ni kwamba bwana Ecko,Juma,Kitunda na Padri James 
niwatu waliotakiwa kuwasaidia wakina Marry na Furaha kufuata 
mwenendo mwema kwa kuwa kiumri walistahili kuwa baba zao lakini 
ndio wana uhusiano wa kimapenzi 

4 . MAPENZI
 Mapenzi kwenye tamthiliya hii yameonyeshwa kwa namna mbili; 
Kwanza,mapenzi ya ulaghai baina ya wanandoa na wanajamii kwa 
ujumla.Mapenzi haya ni yamekwamisha mapambano na mafanikio 
dhidi ya UKIMWI .
Pili,mapenzi ya ulahai baina ya wanandoa ambapo Bwana Ecko si 
mwaminifu katika ndoa yake na wanawake wengine wa kijiji chao 
wana wanaume wengi hali hii inaweka kijiji chao katika hatari ya 
maambukizi ya VVU/UKIMWI
Juhudi ya kutafuta barua ya orodha ziliwafanya Padri James na 
wenzake ni ishara ya hofu ya kutambulika kuwa ni waathirika wa 
UKIMWI kwa sababu walikuwa uhusiano wa kimapenzi na Furaha.

5. SUALA LA UWAZI NA UKWELI.
Katika mapambano dhidi ya UKIMWI suala la uwazi ni muhimu sana 
katika tamthiliya hii.Furaha baada ya kutambua ana maambukizi ya 
UKIMWI aliamua kuandika barua ya ORODHA kuwataadharisha 
wanakijiji kuhusu UKIMWI 
 Furaha alimwambia mpenzi wake Salim kuwa ana UKIMWI “nina 
UKIMWI salim‟‟ zaidi ya hayo,Furaha katika barua yake alitaja mambo 
ambayo aliamini wanakijiji wakizingatia wataepuka maambukizi ya 
UKIMWI
Mama Furaha nae alijua bayana sababu ya kifo cha mwanae Furaha 
kuwa ni UKIMWI.Mama huyu alitambua kuwa ukweli na uwazi ni 
silaha madhubuti katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.

6. UKOSEFU WA HUDUMA ZA AFYA 
Katika tamthiliya hii mwandishi ameonyesha kuwa ukosefu wa 
huduma za afya unachangia kwa kiasi kikubwa katika kupoteza 
maisha ya watu,katika kijiji cha akina Furaha hakukua na huduma 
za afya ndio maana ililazimu daktari wa Furaha achukue vipimo na 
kupeleka mjini ambako ndipo huduma hizo zinapatikana ili kubaini 
tatizo lililokuwa linamsumbua Furaha
 Maisha ya waathirika kama Furaha yalihitaji huduma za afya ziwe 
bora na karibu na makazi yao.Huduma hizo zitawasaidia kuwapa 
elimu ya magonjwa kama Malaria pamoja na kifua kikuu 
 Pia upatikanaji wa huduma za afya husaidia kuwashirikisha 
wananchi dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI 
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha kuwa suala la ukosefu wa 
huduma za afya linachangia suala la unyanyapaa kwa wagonjwa wa 
UKIMWI kuongezeka siku hadi siku na hivyo kuwafanya watu 
walioathirika wasiwe tayari kujitangaza.

7. TIBA YA UKIMWI 
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha kuwa mpaka sasa hakuna 
tiba ya kitaalamu ambayo inapatikana,kutokana na hali hiyo watu 
wengi wamekuwa wakizua tiba mbalimbali mfano imedaiwa kuwa mtu 
mwenye virusi vya UKIMWI akifanya mapenzi na mtu mwenye bikira 
hupona kama ilivyoeleza Bwana Ecko
 Ukweli ni kwamba hakuna tiba ya ugonjwa wa UKIMWI 
kinachotolewa kwa sasa ni dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo 
na si kutibu 
 Kwa mantiki hiyo ni busara kwa jamii kuhakikisha kwamba 
inaepuka njia zote ambazo zinaweza kusababisha maambukizi ya 
virusi vya UKIMWI.

 MIGOGORO.

Ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili au zaidi zenye mitazamo 
tofauti.Katika tamthiliya hii kuna migogoro mbalimbali kama 
ifuatavyo;
Mosi,Mgogoro kati ya mama Furaha na Padri James,chanzo cha 
mgogoro ni Padri James kupinga mama Furaha asisome Orodha hiyo, 
suluhisho ni mama furaha anamwonyesha kuwa Padri hana cha 
kuficha hivyo aliisoma hiyo barua kwa nguvu
Pili,Mgogoro kati ya Furaha na dada mdogo katika harakati za
kutoroka usiku kwenda baa,dada mdogo hapendezwi na tabia hiyo na
suluhisho ni dada mdogo kumtisha kwenda kusema kwa mama yao 
Tatu,Mgogoro kati ya baba na Furaha kuhusu kutoroka bila 
ruhusa ya wazazi na pia kujihusisha na ulevi na umalaya,suluhisho 
la tatizo hilo ni baba kumpiga mwanae na kumwonya kwa maneno 
makali 
Nne,Mgogoro kati ya mama Furaha na Salim kuhusu 
orodha,Salim kutokukubaliana na mama Furaha na kulazimika 
kuipora orodha na kuichana vipande,suluhisho ni mama Furaha 
kumkumbusha fadhila za Furaha kwa Salim na kuamua kusoma 
karatasi iliyobaki na kuokota vipande vile kuviunganisha na kuisoma 
orodha.

 UJUMBE
Mwandishi wa tamthiliya hii anatoa ujumbe kwamba;
 Elimu ni silaha muhimu katika mapambano dhidi ya UKIMWI 
 Umasikini na ulevi ni vyanzo vingine vya ongezeko la 
maambukuzi mapya ya VVU/UKIMWI 
 Asiyesikia la mkuu huvunjika guu,Furaha hakusikia maonyo ya 
wazazi wake akapata UKIMWI 
 Tamaa mbele mauti nyuma,vijana wengi wanaendekeza tamaa 
za fedha au vitu matokeo yake ni kupata matatizo mfano 
Furaha alipata UKIMWI 
 Umdhaniaye ndiye kumbe siye,Furaha alikuwa anamwamini 
Padri James kama mlezi wa kiroho matokeo yake akamwingiza 
kwenye uzinzi 
 Uadilifu,upendo,uaminifu,uwajibikaji na matumizi ya 
kinga(kondomu)ni baadhi ya mambo yanayoweza kutuepusha 
na UKIMWI.

FALSAFA 
Mwandishi anaamini kuwa mapambano dhidi ya UKIMWI ni jukumu 
la watu wote hivyo uadilifu ,uwajibikaji ,upendo,uaminifu ni nyenzo 
bora katika mapambano hayo.

KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
Kimaudhui,Mwandishi amefaulu kufikisha ujumbe wake kwa 
walegwa.Mwandishi ameweza kujadili vyema tatizo la UKIMWI kwa 
kutumia mazingira ya kijijini 
Mwandishi ameeleza wasiwasi wake kuhusu uelewa wa watu waishio 
kijijini kuhusu ugonjwa waUKIMWI lakini pia ameweza kueleza 
mambo ya msingi ya kuzingatia katika mapambano kwa kutumia 
mbinu ya waraka(baruaya orodha yenye mambo hayo muhimu ya 
kuzingatia).Barua ile imetumika kama wosia unasomwa siku ya 
mazishi siku yenye huzuni na hofu miongoni mwa watu ili kuleta 
athari za uoga kuhusu UKIMWI 
Mwandishi ametumia wahusika wachache ambao hawamchanganyi 
msomaji.Wahusika wa rika na jinsia mbalimbali wametumika 
kuwasilisha mawazo ya watu mbalimbali kuhusu UKIMWI kutokana 
na uzito wa tatizo linalojadiliwa mwandishi amefaulu kutumia lugha 
inayoeleweka kwa urahisi iliyojaa ucheshi tamathali za semi na 
mbinu mbalimbali za kisanaa 
Vilevile mwandishi amekuwa makini kujadii utamaduni wa jamii 
husika kwa kutumia tafsida kulinda miiko ya utamaduni wetu katika 
kutumia lugha
Pia mwandishi amefaulu kupangilia matatizo kutokana na ukubwa 
wa tukio linalozungumziwa,mwandishi anaanza na msiba kuwa 
jambo lililopo mbele yetu ni msiba wa jamii na anamaliza na sehemu 
ya mwisho kwa msiba kuonyesha msisitizo wa dhamira kuu
Kwa ujumla mwandishi amefaulu kwa kimaudhui kufikisha ujumbe 
kama ilivyokusudiwa kwa jamii.

KUTOFAULU KWA MWANDISHI 
Mwandishi ameshindwa kuelewa njia mbalimbali zinazoeneza 
UKIMWI toka mwanzo hadi mwisho wa kitabu mwandishi 
ameonyesha njia moja tu ambayo ni kufanya mapenzi yasiyo salama 
Hii ni muhimu ili kupunguza unyanyapaa.
Mwandishi ameshindwa kugawa kitabu katika maonyesho mbalimbali 
kitabu kizima kina onyesho moja lenye sehemu ishirini,mwandishi 
angeweza kuweka shemu katika maonyesho matatu.Hiii ingeweza 
kufuatilia matukio kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasa.

FANI
Mwandishi amewagawa wahusika katika makundi mawili yaani 
wahusika wakuu na wahusika wasaidizi.

A. WAHUSIKA WAKUU 
 Mhusika mkuu katika tamthiliya hii ni Furaha,
 Msichana aliehitimu darasa la saba,
 Furaha alijihusisha katika mambo ya uzinzi akiwa na umri 
mdogo 
 Furaha hakuwa mtiifu kwa wazazi wake kwani licha ya 
kukatazwa tabia ya utoro wa usiku na ulevi hakuacha tabia 
hiyo bali aliendelea mpaka alipopata maambukizi ya VVU
 Hakuwa mwaminifu kwa mpenzi wake Salim,alikuwa muongo 
kwani alimdanganya Salim hana mwanaume mwingine zaidi 
yake,
 Alijihusisha kimapenzi na watu waliomzidi umri ambao sawa na 
baba yake mfano bwana Ecko na Padri James
 Alikuwa na tama ya pesa na vitu ,alidanganyika kirahisi mfano 
Marry alimdanganya kuwa mwema kwa akina bwana Ecko.
 Si mwaminifu,
 Muwazi,
 Mwenye upendo yuko mstari wa mbele kupambana
 naVVU/UKIMWI.

B. WAHUSIKA WASAIDIZI.

Mama Furaha 
 Ni mama mzazi wa Furaha
 Ni mchapakazi 
 Ni mpole 
 Ni mama mwenye upendo 
 Mkweli
 Ni muwazi 
 Ana msimamo 
 Anafaa kuigwa na jamii kwani ni mama aliyeejishughulisha
katika ulezi wa watoto na familia nzima.

Baba Furaha 
 Ni baba mzazi wa Furaha 
 Ni mkali 
 Ana upendo 
 Ana lugha kali kwa wanae.

Marry 
 Ni msichana 
 Ni rafiki yake Furaha 
 Ni Malaya 
 Mlevi 
 Hafai kuigwa na jamii .

Bwana Ecko 
 Ni mwanaume mtu mzima 
 Ni mfanya biashara 
 Ni mlevi 
 Hafai kuigwa na jamii,sio mwadilifu katika ndoa yake,ni 
mwathirika wa UKIMWI.

Bwana Juma 
 Ni mwanaume mtu mzima 
 Ni rafiki yake na bwana Ecko 
 Ni mzinzi
 Ni mtu mwenye tama 
 Ana lugha chafu hafai 
 Hafai kuigwa na jamii.

Kitunda
 Ni kijana wa mtaani 
 Ni rafiki yake na Furaha 
 Ni msanii 
 Sio mwadilifu 
 Sio muwazi 
 Sio mkweli 
 Anaweza kuwa mwathirika wa UKIMWI japokuwa alitumia 
kondomu baadhi ya siku alizokutana na Furaha.


MTINDO 
Mwandishi wa tamthiliya hii ametumia mitindo mbalimbali katika 
kazi yake mfano matumizi ya majibizano (dayaloji)Mtindo huo 
huruhusu wahusika wake kuzungumza kwa kujibizana mfano 
mazungumzo kati ya Furaha na Kitunda 
Furaha:kuvuta nini lako........(anarudi nyuma)
Kitunda:Mezea mtoto lazima ujifunze lugha za mitaani.

MUUNDO
Mwandishi wa tamthiliya hii ametumia mtindo wa onyesho ambao 
sehemu hizo zipo kwenye makundi matatu ambayo yamejipambanua 
kutokana na matukio mfano sehemu 1-2 ni mazishi ya Furaha 
ikihusisha kuugua na kifo chake ,sehemu ya 17-20 ni mwendelezo wa 
mazishi ya Furaha ikiwemo mchakato wa kutafuta barua ya furaha 
(orodha)mchakato unaofanywa a Bwana Ecko,Padri James na Salim 
na mwiso wa mazishi ulioamatana na kusomwa barua ya orodha
 
MANDHARI 
Mwandishi ametumia mandhari ya kijijini.Hii inawakilisha vijiji 
mbalimbali hapa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla ,mahala 
ambapo elimu kuhusu UKIMWI haijaeleweka vema au hakuna kabisa 
pia huduma za afya kama hospitali hakuna kabisa.

MATUMIZI YA LUGHA 
Lugha iliyotumika ni ya kawaida inaeleweka na inazingatia maadili ya 
kitanzania na kueleweka vema kwa walengwa na kwa kiasi fulani 
tamathali za semi na mbinu nyingine za kisanaa.
 
Misemo/Nahau 
Misemo iliyotumika kwenye tamthiliya hii ni kama ifuatavyo ,
 “Shuga dadi”mwandishi akiwa anamaanisha wanaume wenye 
umri mkubwa wanaopenda kutembea na wasichana wadogo 
umri sawa na binti zao 
 “mshamba “mtu ambae hajui mambo ya mjini au mambo ya 
kileo 
 “furaha anavuna mbegu ya kifo aliyoipanda”kuvuna ni 
msemo unaomaanisha kupata kitu kutokana na matenyo au 
maandalizi ,msemo huu ni sawa na “utavuna ulichopanda”

 MISIMU 
Mwandishi ameweza kutumia lugha ya misimu ili kuweza 
kumtambulisha muhusika ,misimu iliyotumika ni ile ya mitaani au ya 
vijana kutoka kijiweni ,lugha hii tunaweza kuona ikitumika katika 
mazungumzo kati ya Kitunda na Furaha mfano mshikaji,mchizi 
,bomba ,poa majani,nitakulinda ,mwanangu ,kuvinjari haya ni baadhi 
ya maneno yanayotumika mitaani hususani maneno haya hutumika 
na vijana wa kijiweni katika mji 
Maana ya maneno hayo 
Mshikaji-rafiki/jamaa
Bomba mchizi –sawa rafiki/ndugu 
Poa-vizuri /sawa 
Ganja,majani-bangi 
Nitakilinda-nitakusaidia 
Mwanangu-mtu wa karibu/rafiki yangu
Kuvinjari-kuzunguka/kutalii.

TAMATHALI ZA SEMI 
Mfano ....yeye ni kama punda wa kijiji tamathalii hii ilitumiwa 
kumfananisha Furaha na punda wa kijiji ambae kila mwaname 
anampenda ,ilitokana na tabia ya Furaha kuwa uhusiano wa 
kimapenzi na wanaume mbalimbali 
Pia Kitunda anafananisha jiji la Dar-es salam sawa na jiji la New york 
anasema....kisura sawa na jiji la New york 
Pia mwandishi anapoonyesha namna vipande vya karatasi 
vilipoanguka baada ya barua ya orodha kuchanwa na Salim 
anasema.....vipande vikaanguka kama theruji


 SITIARI 
Tamthiliya hii imetumiwa na baba Furaha anapofananisha watoto 
wake ma mbu wanyonyao damu wasioweza kujitegemea anasema 
“nyie mbu wadogo”.

 KIJEMBE
Mwandishi ametumia kejeli kati ya Marry na bwana Juma anasema 
Marry:nielezewewe ni mzee wa kutosha kuwa baba angu
 
 TAFSIDA 
Pia mwandishi ametumia tafsida ili kupunguza ukali wa maneno 
aliyoyatumia 
Mfano :Bwana Ecko:Juma hebu mwangalie yule msichana 
anavyotingisha kile alichopewa na mama yake 
Bwana Juma:kama ulivyofanya wewe mishikaki yangu midogo 
Tamathali hiyo(tafsida)imetumiwa badala ya kutaja sehemu zake za 
siri anazozizungumzia.

 TASWIRA
Mwandisha pia ametumia lugha ya picha(taswira)
Mfano,karibu nitakufa njaa hali nyie mbu wadogo mnainyonya damu 
yangu yote,mbu ni taswira inayoonyesha hali ya utegemezi.

JINA LA KITABU 
Kitabu hiki kinaitwa ORODHA (The list)neno lenye maana la 
mfuatano au mfululizo wa vitabu au mambo.Kitabu hiki kinaonyesha 
orodha zifuatazo
Mosi,Orodha ambayo Furaha alibainisha mambo ambayo 
yalisababisha kifo chake.mfano;ngono zembe,ukosefu wa 
elimu,kukosekana kwa uaminifu,umasikini.
Pili,kuna orodha ambayo ina mambo ambayo jamii inapazwa 
kujazingatia ili waepuke UKIMWI ambayo ni ngono 
salama,uadilifu,uaminifu,elimu sahihi kuhusuVVU?UKIMWI 
Mwisho,orodha inadhihirika kwa kuitafuta orodha iliyoandikwa na 
kuachwa na furaha ili isomwe kwenye mazishi yake.



NGOSWE -PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MTUNZI: EDWINI SEMZABA
MCHAPISHAJI:THE GENERAL BOOKSELLERS LTD 
CHAPA YA 1-1988.

UTANGULIZI 
Ngoswe-penzi Kitvu cha Uzembe inaonyesha namna jamii inapaswa 
kushiriki mipango mbalimbali ikiwepo ya kisiasa kiuchumi na 
kiutamaduni.Mafanikio ya mipango hiyo inategemea na kujulikana 
kwa idadi ya watu utayari,uelewa wa watu hao kuhusu mipango 
husika 
Tamthiliya hii inaonyeshakazi ya kuhesabu watu ilivyokwama kijijini 
kwa mzee mitomingi ngengemkeni kutokana na uzembe wa afisa wa 
kuhesabu sensa Ngoswe.


DHAMIRA

1. MAPENZI 
Mwandishi Edwin semzabaameonyesha jinsi mapenzi yalivyo kitovu 
cha uzembe,wahusika Ngoswe na Mazoea wametumiwa na mwandishi 
kufafanua dhamira hii 
Ngoswe baada ya kufika kwa mzee Mitomingi anashindwa kuitawala 
nafsi yake mara anapomuona Mazoea,Ngoswe aliamua kuanzisha 
uhusiano wa kimapenzi na Mazoea hali iliyomfanya ashindwe 
kuimudu kazi yake na mapenzi kwa wakati mmoja.
Ngoswe anamtorosha Mazoea kitendo hiki kinamuudhi balozi 
Mitomingi Ngengemkeni (baba mzazi wa mazoea)na kuamua kuchoma 
moto karatasi muhimu za serikali.Ngoswe anaonekani ni mzembe kwa 
kuwa alishindwa kutofautisha kazi na mapenzi kama msomi (afisa wa
sensa )alitakiwa ajue umuhimu wa kazi iliyompeleka kijijini.

2. ULEVI NA ADHARI ZAKE 
Katika tamthiliya ya ngoswe penzi kitovu cha uzembe mwandishi 
anaonyesha namna ulevi ulivyoleta madhara,mfano kuchelewesha 
kazi.Wahusika Mitomingi na Ngoswe wanashindwa kukamilisha kazi 
kwa vile wahusika (wahesabiwa)wapo kwenye Pombe kama maneno 
haya yanavyothibitisha;
Mitomingi:Haya ni matatizo yote hii shauri ya pombe nadhani yupo 
kilabuni
Ngoswe :hawezi kwenda kuitwa?
Mitomongi:haitosaidia mkewe tu hana habari ya kuhesabiwa sembuse 
hao wengine kwa leo haitowezekana 
Licha ya kuchelewesha kazi ulevi huaribu kazi.Mfano:ngoswe 
anaunguza karatasi za sensa baada ya kulewa pombe ya mnazi.

3. ELIMU 
Elimu ni chombo cha ukombozi kama itatumiwa vizuri
ipaswavyo,mwandishi wa tamthiliya hii amemuonyesha kijana Ngoswe 
(msanii)alivyoshindwa kutumia elimu yake hususani katika kujua 
namna ambavyo maisha ya mjini yanavyotofautiana na maisha ya 
kijijini,Ngoswe anajikuta akiharibu kazi yake kwa kukosa maarifa.
Mwandishi ameonyesha elimu katika familia ya mito mingi haikupewa 
thamani yoyote ile wananchi wengi hawakuwa na elimu kwa kisingizio 
cha shule kuwa mbali,ukosefu wa elimu ulichangia ukosekanaji wa 
huduma muhimu kama vile hospitali ,miundo mbinu na maji ili 
kupata maendeleo,suala la elimu lazima litiliwe maanani watu 
wakieleweshwa wataweza kujua wajibu wao :-
Mfano:kujali kazi na kuacha ulevi “kutumia vema hospitali badala ya 
kutegemea mitishamba.

4. UCHAWI NA USHIRIKINA 
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha jinsi watu wengi ndani ya 
jamii walivyo na imani juu ya uchawi,wanajamii hawa wameweka 
vikwazo kuhusu sensa wakiamini kuwa mtu anayewahesabu wenzake 
ni mchawi 
Mfano:mama anasema mchawi ndiyo huhesabu watoto wa wenzake ili 
awaroge sasa wewe ni mchawi?hata kama si mchawi siwezi kukubali 
unihesabu maana sijui nia yako kama ni mbaya au nzuri.Imani hizo 
ni za kishirikina zinachangia kukwama kwa zoezi la sensa pia 
maendeleo kwa ujumla kuwachini,watu wakiugua hawapelekwi 
hospitali badala yake wanapelekwa kwa mganga wa kienyeji 
wakidhani kuwa amerogwa.

5. NAFASI YA MWANAMKE 
 Katika tamthiliya hii mwanamke ametazamwa katika mitizamo 
tofauti kama ifuatavyo;
 Mwanamke amechorwa kama chombo cha 
starehe,mwandishiamemuonyesha mzee mitomingi kuwa na 
wake wengi (mitala)bila kuoyesha bayana kazi zao.
 Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na sauti 
mfano:Mazoea na mama yake hawakushirikishwa katikamipango ya 
kutaka kuolewa mazoea kwa vile walionekana hawana mchango 
wowote katika maamuzi hayo 
 Mwanamke amechorwa kama mlezi,
katika tamthiliya hii inamchora mwanamke kama mtu mwenye 
majukumu ya malezi ya watoto,baada ya Mazoea kuwa na mahusiano 
na Ngoswe mzee Mitomingi anamlaumu mama yake Mazoea kuwa 
hakuona dalili ya mahusiano ya kimapenzi kwa kuwa ni jukumu la 
mama kumwangalia binti yake.

5. NDOA NA MALEZI 
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha suala la ndoa ni sualala 
hiyari na si kufuata matakwa ya wazazi,Mazoea alichaguliwa 
mchumba na wazazi wake (baba yake)hali iliyomfanya kutoroka na 
ngoswe 
Hali kadhalika katika tamthiliya hii wanaume wengi wana mke zaidi 
ya mmoja hali hii inapelekea familia kuwa kubwa na kushindwa 
kuzitunza.
Mfano:Mzee Mitomingi ana wake wawili ambao ni mama Mazoea na
mama Mainda,wazazi hawa wanatofautiana katika malezi hasa kwa 
Mazoea hali iliyopelekea kuwa na tabia mbaya.
Kwa upande mwingine ndoa zenye mke zaidi ya mmoja haziwi na 
upendo ndani ya familia hivyo kuwa kikwazo kwenye malezi.

6.UVIVU NA ATHARI ZAKE
Wanakijiji wa Ngengemkeni mitomingi wengi ni wavivu muda mwingi 
wanautumia kwenye ulevi na uvuvi,unawafanya wakose huduma 
muhimu kama shule,barabara na hospitali huduma hizi 
zingepatikana kama wananchi wenyewe wanajitolea.
Siku zote wavivu wanatafuta visingizio,vifo vingine vinatokea sababu 
ya uzembe na uvivu kisha sababu hutafutwa.
Mfano:wanawake wawili walidai mume wao amerogwa ili hali wenyewe 
hawakumpeleka hospitali.

 
MIGOGORO 
Ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili zenye mitazamo tofauti 
Katika tamthilia ya Ngoswe penzi kitovu cha uzembe kuna migogoro 
mingi ambayo imeweza kujitokeza kama ilivyoonyeshwa na 
mwandishi 
 Mgogoro kati ya Ngoswe na wazazi wa Mazoea chanzo cha 
mgogoro huu umetokana na Ngoswe kumtorosha 
Mazoea,suluhisho wazazi kumfukuza Ngoswe na Mazoea 
kuchoma karatasi na kumwadhibu Mazoea 
 Mgogoro kati ya Mazoea na wazazi wake,chanzo cha mgogoro 
huu ni baada ya Mazoea kutoroka na Ngoswe ili hali Mazoea 
tayari ana mchumba wake,suluhisho ni mitomingi kumchapa 
mazoea na kuchoma karatasi za sensa.
 Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali,chanzo cha mgogoro huu ni
Ngoswe kuharibu kazi ya sensa na hivyo kusababishia serikali 
ishindwe kupanga mipango ya maendeleo,suluhisho 
halijapatikana hadi mwisho.


UJUMBE 
 Si jambo zuri kuchanganya suala la kazi na starehe au 
mapenzi,wakati wa kazi uwe wa kazi na wakati wa starehe uwe 
wa starehe 
 Wavulana wanaovuruga wasichana siku moja watakamatwa na 
wasichana wenyewe wanapewa tahadhali wasiwe na maamuzi 
bila kufikilia.
 Elimu ni kitu cha muhimu sana katika jamii na jamii isipokuwa 
na watu walioelimika hawawezi kuwa na maendeleo maana ili 
tuwe na maendeleo tunatakiwa tutupilie mbali ulevi na uvivu 
katika jamii yoyote 
 uchawi na ushirikina ni kikwazo kikubwa katika maendeleo.

FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa ni rahisi jamii kuingia kwenye matatizo 
kama itachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo 
ikumbukwe kuwa kila jambo na wakati wake.

FANI 
Vipengele vya fani katika kazi ya fasihi ni muundo ,mtindo,madhari 
,wahusika na matumizi ya lugha.

MUUNDO
Muundo uliotumika katika tamthiliya ni wamuundo wa moja kwa 
moja ambapo kazi nzima ipo katika sehemu tano ambazo mwandishi 
amezipa majina ya kitwasira kulingana na ukubwa wa tatizo 
linalozungumziwa ,yaani ameonyesha kuingia kwa Ngoswe kijijini 
mazingira yanayoashiria hali ngumu ya maisha(kijito)Mo
 Sehemu ya pili inaonyesha kazi ya kuhesabu watu imeanza na 
watu hawana utayari na uelewa juu ya sensa (vijito)
 Sehemu ya tatu inaonyesha Ngoswe ameanza kujihusisha na 
mapenzi na ulevi,ambavyo ni viashiria vya kuharibu kazi yake
(mto)
 Sehemu ya nne inaonyesha kazi aliyopewa Ngoswe tayari 
imekosa mwelekeo,Ngoswe amebobea kwenye mapenzi na ulevi, 
karatasi zinachomwa moto baada ya kumtorosha Mazoea (jito)
 Sehemu ya tano inaonyesha serikali ikimuhukumu Ngoswe juu 
ya takwimu zilizoungua moto na Ngoswe asingizia kuwa kijijini 
kuna shida ya kuhesabu kwani nyumba zimejitenga na watu 
wenyewe kutoelewa (baharini).


MTINDO 
Mtindo uliotumika ni wa kidayalojia ambapo wahusika wake 
wanazungumza kwa kujibizana
Pia kuna matumizi ya nafsi zote tatu na nafsi hizo zimetumika katika 
sehemu mbalimbali.Mfano sehemu ya tano kwa matumizi ya nafsi ya 
kwanza pale Ngoswe anapoulizwa na serikali kuhusu takwimu 
akajibu “usemi sinao”

MANDHARI 
Kitabu hiki kimejengwa katika mandhari ya kijijini,hii inadhihirishwa 
na ukosefu wa huduma muhimu kama vile shule hospitali na miundo 
mbinu 
Tabia za wahusika pia zinaonyesha mandhari ya kijijini mfano,ulevi 
wa pombe za mnazi,watu kutojali elimu,kun‟gan‟gania mila zilizopitwa 
na wakati.

MATUMIZI YA LUGHA 
Mwandishi ametumia lugha nyepesi na yenye kueleweka pia 
mwandishi ametumia tamathali za semi,misemo na mbinu nyingi za 
kisanaa.

Tamathali za semi 
Hizi ni semi au kauli zitumiwazo na mwandishi katika kazi ya fasihi ili 
kuongeza ladha katika kazi husika.

Tashibiha
Ni tamathali ilinganishayo vitu viwili au zaidi kwa kutumia 
viunganishi kama mithili ya ,kama,mfano wa 
Mfano,Ngoswe anaposhangaa ardhi ya kijijini kwa balozi Mitomingi 
anasema
 Udongo mwekundu kama ugoro wa sabiani
 Tazama suruali yake kama kengele ya bomani 
 Nikitoka hapa najitupa kitandani kama gogo.

Tafsida
Ni tamathali itumiwayo kupunguza ukali wa maneno 
mfano Mainda anasema labda anajisaidia(Uk 21).
 
Takriri
ni tamathali inayorudiarudia neno ili kuweka mkazo juu ya kile 
kinachosemwa 
Mfano; karibu,karibu(pale Ngoswe alipokuwa akikaribishwa).

Mdokezo
Ni tamathali ambayo hueleza jambo kwa kukatakata maelezo
Mfano Mazoea anasema sijui......sijui......siwezi namwogopa baba (Uk 
22)

Tanakali za sauti.
Ni tamathali inayoiga mlio wa vitu 
mfano Ngoswe alishindwa kujizuia akacheka ha ha ha ha 
Methali 
Ngoswe anamwambia Mazoea 
 “Penye nia pana njia” (uk 22)
Misemo 
 Hebu keti tutupe mawe pangoni 
 Kupeleka chakula ndio unafanya makambi 


Taswira/Jazanda
Taswira mbalimbali zimetumiwa na mwandishi katika tamthiliya hii. 
Msanii ametumia taswira ya mtu kwa kuhusisha na matukio ya 
wahusika.Mwandishi analinganisha mwanzo wa mchezo ni kijito ni 
mto mdogo sana hivyo maelezo ya sehemu hii yanategemewa kuwa 
madogo sana 
 Sehemu inayofuata ya vijito,sehemu ya vijito inaonyesha kuwa 
masuala yanashughulikiwa na kujadiliwa hapa yanaongeza 
uzito ingawa sio mazito sana 
 sehemu ya mto inaonyesha ukubwa wa shughuli ya Ngoswe 
yuko kazini (yuko mtoni)tayari yupo ndani ya jukwaa bila shaka 
maji ya mto ni mengi (matatizo mengi)na hivyo yeyote 
atakayeingia mtoni yampasa awe mwangalifu 
 sehemu ya jito inaashiria kuna hatari, kuna matatizo mengi,
katika jito kulivika si kazi rahisi hatimaye tunaonyeshwa 
Ngoswe amezama baharini ambapo kuzama kwa Ngoswe ni 
baada ya makaratasi kuchomwa moto.


WAHUSIKA 
Wahusika ni watu walioshiriki katika mchezo au tamthiliya husika.
Mwandishi amegawa wahusika katika makundi mawili yaani mhusika 
mkuu na wahusika wasaidizi.

MHUSIKA MKUU 
NGOSWE 
Ni msomi anayependa kazi ya kuhesabu watu lakini kutokana na 
tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya takwimu zote 
kuchomwa moto na Mitomingi kutokana na kitendo cha kujaribu 
kumtorosha mazoea .

WAHUSIKA WADOGO 
Mazoea 
 Msichana mwenye umri wa miaka 18-20
 Ni mtoto wa balozi (Mitimingi)
 Anawakilisha wanawake wasio na msimamo katika mapenzi.

Ngengemkeni mitomingi 
 Huyu ni balozi
 Baba yake Mazoea 
 Anachoma karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kutaka 
kumtorosha Mazoea 
 Ni mzee aliyeshikilia ukale na anapenda ndoa za mitara.

JINA LA KITABU 
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe jina hilo la kitabu linasadifu 
yaliyomo ndani ya kitabu ,kwani msanii kwa kiasi kikubwa amejaribu 
kujadili na kuonyesha matatizo yanayoikumba jamii katika shughuli 
za kijamii,matatizo hayo ni kama uchawi ulevi uzembe na dhana
nyingine potofu.


KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI 
Mwandishi katika tamthiliya hii amefeli kwa kuwa ameonyesha 
matatizo yaliyomo katika jamii bila kuonyesha mbinu mbadala ya 
kuyatatua.








UHAKIKI WA RIWAYA YA TAKADINI 
Mwandishi :BEN HANSON 
Mchapishaji :Mathews bookstore


UTANGULIZI 
TAKADINI ni riwaya inayoeleza maisha ya jamii za kiafrika na 
tamaduni zake.Riwaya hii inaeleza namna jamii nyingi za kiafrika 
zinavyowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye ulemavu 
kutokana na mila potofu.Katika riwaya hii mwandishi amemtumia 
kijana Takadini aliyezaliwa sope alivyowakilisha waathirika wa mila 
hizo potofu.

MAUDHUI
DHAMIRA KUU ;UKOMBOZI 
Mwandishi ameeleza kuwa ili tuweze kupata ukombozi wa kweli na 
kujenga jamii mpya tunapaswa kuachana na mila potofu na 
kukomboka kifikra na kiutamaduni.Miongoni mwa mila hizo ni 
mauaji kwa watu wenye ulemavu.Takadini alizaliwa sope aliamriwa 
auawe siku ya pili tu toka atoke tumboni mwa mamaye Sekai.
Aidha makwati anasikitika baada ya kuletewa taarifa kuwa mtoto 
aliyezaliwa ni sope anasema.....hilositalielewa......itakuwaje....aliuliza 
maswali mengi (uk 12).Bila ngozi?,Sope?ni nini ulichokileta hapa 
kwetu?maswali haya yanaonyesha
namna walemavu 
wasivyothaminiwa.Suala hili lilimsononesha sana Sekai inaonyesha 
dhahiri mtoto sope katika jamii ya Makwati hakustahili kuishi.

DHAMIRA NDOGO NDOGO
1. MAPENZI 
Mwandishi anaonyesha mapenzi katika sura mbili tofauti yale ya 
dhati na ya uongo.Mapenzi ya dhati hayachagui hali wala mali pia 
kabila dini wala rangi.Kila mtu ana haki ya kupendwa na kupenda ,
 Mapenzi ya dhati kati ya Sekai na mwanae ,Sekai alikuwa 
radhi auawe ilimradi furaha yake itimie ya kubaki na mwanawe 
sope,hakuogopa kufa alimlinda takadini na kuamua atoroke 
baada ya makwati kuruhusu wazee wamwangamize 
 Mapenzi ya dhati kati ya Sekai na Tendaihawa ni marafiki 
wa kweli walifarijiana baada ya kuelezana matatizo yao,Tendai 
mke mdogo wa mtemi masasa aliyelazimishwa kuolewa na mzee 
wa rika la baba yake.
 Mapenzi ya dhati kati yaMzee Chivero na Sekai,mzee 
Chivero alimpokea Sekai na mwanawe Takadini na 
kuwachukulia kama wanawe (familia yake)licha ya wanakijiji 
wengine kuwatenga 
Mapenzi ya dhati baina ya Takadini na Shingai ,Shingai 
alimpenda Takadini licha ya kuwa na ulemavu wa ngozi (sope)pia 
mlemavu wa mguu (alitembea kwa msaada wa gongo)kama anavyokiri 
mwenyewe “huyu ndiye mwanaume ninayetaka anioe”
Mapenzi ya uongo ni baina ya Makwati na Takadini ,Nhamo na 
Shangai ,Sekai na wake wenza isipokuwa Pindai.

2. NDOA ZA MITARA 
Mwandishi ameeleza athari za ndoa za mitara kuwa ni pamoja na 
chuki baina ya wanawake na hivyo kusababisha migogoro ndani ya 
familia.Mfano Sekai anasengenywa na wake wenza wake Dedirai,na 
Rumbidzai na kudai ni mchawi 
Aidha wake wa Mtemi Masasa wanamdharau Tendai na kuchukulia 
kama mtoto wao na si mke mwenzao kwa sababu ya umri wake 
mdogo.

3. MILA POTOFU
Dhamira hii imetazamwa katika sura tofauti kama vile:-
 Wazazi kuwachagulia watoto wao wenza (wake/waume)Tendai 
na Shingai wanalazimishwa kuolewa na watu wasiowataka,hii 
ni mila potofu zilizopitwa na wakati.
 Mauaji kwa walemavu ,mwandishi anaonyesha kuwa watu 
wenye ulemavu hawakustahili kuishi katika himaya ya akina 
Makwati na mtemi Masasa na ndiyo maana kuzaliwa na kuishi 
kwa Takadini kulileta mzozo.

4. NAFASI YA MWANAMKE 
Jamii nyingi za kiafrika zinamkandamiza mwanamke na kumfanya 
mtu duni katika Nyanja mbalimbali za maisha,kama ifuatavyo;
 Mwanamke hana maamuzi yake binafsi,watoto wa kike 
hawapati haki sawa na watoto wa kiume.mfano Tendai 
anaonekana kutofurahishwa na tendo la kuolewa na mume 
mwenye umri mkubwa (mzee Masasa)alisema “ni heshima 
kuwa mke wa mtemi mwenye nguvu kama Masasa lakini 
namchukulia kama baba yangu kuliko 
mumewangu”.......’’(uk 47)hapa inaonyesha mwanamke hana 
nafasi ya kuongea kama mtu mwingine.
 Mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe,hili 
linaonyeshwa kwa mzee Makwati na Mtemi Masasa kuwa na 
wanawake wengi kwa ajili ya kujifurahisha na hili linajitokeza 
bayana pale(uk 40) aliletwa mtoto kumpa joto mzee angehisi 
msisimko wowote ule wa mapenzi.
 Mwanamke anachorwa kama mwanamapinduzi ,haya 
yanajionyesha wazi kwa Sekai na Shingai ni wanawake 
walioleta mabadiliko katika jamii.mfano Sekai alikuwa wa 
kwanza kuvunja mila na desturi kwa kukataa Takadini asiuawe 
na kuamua kutorokea kijiji cha jirani pia alileta mabdiliko 
akiwa uhamishoni 
Shingai naye mwanamapinduzi kwani alipingana na suala 
kuchaguliwa mchumba aliamini kuwa ndoa ya kweli inahusisha 
watu wawili waliopendana na waliochaguana alisema “ Si 
kwamba ninamchukia Nhamo ,la hasha isipokuwa sidhani

kama nitakuwa furaha ya kuishi naye”(UK 110)mwisho 
mwandishi anaonyesha Shingai ameolewa na Takadini na 
wamezaa mtoto asiye sope.

5. UMOJA NA MSHIKAMANO 
Umoja na mshikamano ni moja kati ya nguzo muhimu katika kuleta 
mabadiliko na ukombozi wa kiutamaduni,mshikamano mzuri 
ulionyeshwa na mzee Chivero,Tendai,mtemi Masasa ulisaidia 
kumlinda Takadini dhidi ya unyanyapaa na hatari ya kupoteza 
maisha katika mapambano yoyote yenye umoja na nguvu utengano ni 
udhaifu.
 
6. UJASIRI
Mwandishi ameonyesha kuwa Sekai ni mwanamke jasiri aliepambana 
kufa na kupona kumlinda mwanae Takadini dhidi ya mila na desturi 
za kikatili hatima yake kuleta ukombozi katika jamii.
 Shingai naye ni mwanamke aliyepambana na matatizo ya 
kuchaguliwa mchumba,mila zinazokandamiza wanawake.

7. SUALA LA MALEZI
Malezi ya watoto yanapaswa kusimamiwa kwa pamoja yaani baba 
na mama.Katika kitabu hiki malezi yanaonekana ya upande mmoja 
mfano Sekai ndio mlezi mkuu wa familia hususani malezi ya 
Takadini 
 Shingai naye anapata malezi kwa mama,shangazi na bibi hata 
anapokata shauri la kutorokea kwa Takadini ,anaulizwa kuwa 
ndivyo ulivyolelewa?mzee Nhariswa anampiga mkewe na 
kusema “umefanya nini wewe mwanamke tangu mwanao 
alivyopeleka maji kwa Sekai umefuatilia kujua
anachokifanya ...uliona dalili kwanini hukutafuta dawa?

UJUMBE 
 Walemavu wana haki sawa ya kuishi kama watu wengine hivyo 
wathaminiwe.
 Malezi yanahusisha pande zote mbili yaani baba na mama hivyo 
kila mmoja awajibike.
 Wanawake wawe na maamuzi katika jamii hiyo ili 
wasinyanyaswe 
 Ndoa nibaina ya watu wawili wapendanao hivyo haipaswi 
kuingiliwa na mtu yoyote
 Umoja na mshikamano ni jambo muhimu katika ukombozi wa
jamii yeyote ile.

MTAZAMO WA MWANDISHI 
Mwandishi ana mtazamo wa kiyakinifu,anaona kuwa matatizo 
yanayotokana na mila na desturi yanaweza kukataliwa na watu 
wengine kwa kuchukua hatua za kujikomboa kama alivyofanya Sekai 
na wenzake.

MSIMAMO WA MWANDISHI
Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani ameeleza udhaifu wa
baadhi ya mila na desturi zinazokandamiza watu hivyo anataka jamii 
ijikomboe dhidi ya mila desturi hizo.


FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa binadamu wote ni sawa hata kama kuna 
tofauti za kimaumbile lakini kila mtu ana haki ya kuishi .

MIGOGORO 
Migogoro imejitokeza sehemu mbalimbali katika riwaya hii ya 
TAKADINI kama ifuatavyo;
 Mgogoro kati ya Makwati na Sekai,chanzo cha mgogoro huu ni 
(mila na imani potofu) baada ya Sekai kuzaa mtoto sope,mtoto 
huyo alipaswa auawe ,mwandishi anasema suala hili 
halikuungwa mkono na Sekai,suluhisho sekai aliamua 
kutoroka kijijini ili kunusuru maisha ya mtoto Takadini.
 Mgogoro wa Shingai na wazazi wake,Chanzo cha mgogoro huu 
ni mila potofu wa kuchaguliwa mchumba ambaye ni Nhamo 
ambapo wazazi walikasirika hata kumtolea maneno 
mabaya,suluhisho ni Shingai anaamua kutorokea kwa 
Takadini.
 Mgogoro kati ya Sekai na wake wenzake,chanzo cha mgogoro 
huu ni Makwati kuzidisha upendo kwa Sekai hivyo waliamini 
kuwa Sekai ni mchawi 
 Mgogoro wa nafsi huu unajitokezakwa Tendai ambaye aliozwa 
kwa mzee Masasa ambaye alikuwa na umri mkubwa 
 Mgogoro wa kijamii,chanzo cha mgogoro ni kuzaliwa mtoto 
mlemavu(sope)kulizuka mgogoro baina ya wanajamii ,wao 
walitaka Sekai na mtoto wake wafukuzwe.


FANI 

MUUNDO 
Mwandishi ametumia muundo wa msago (moja kwa moja).Mwandishi 
ameanza mwanzo kuonyesha mimba ya Sekai ambayo inazua chuki 
kwa wake wenza pia anapozaa mtoto wa kiume (sope)
 Sekai anaamua kutoroka ili kuokoa maisha ya mtoto,anaishi 
ugenini siku nyingi hata sope anakuwa mkubwa na kupata mke 
na mwisho kabisa mwandishi anaonyesha Sekai akipanga 
kurudi kwao.

MTINDO 
Mwandishi anatumia mtindo wa masimulizi vilevile kuna matumizi ya 
dayalojia (UK 4)Dadirai na Rumbidzai wanajibizana 
Je na yule mbuzi wako uliepewa na baba mzee Makwati amekupa 
watoto wangapi?
Tangu nimepata ni miaka miwili sasa na tayari ana watoto wawili 
nabado anatarajia mwingine.
Pia mwandishi ametumia nyimbo (UK 2)
Mashamba yote yamelimwa mbegu zote zimepandwa zimechipua na 
kumea,sisi watatu tumepata mavuno yetu.,Mheshimiwa wetu 
amemiliki mavuno kwa mikono yake halisi kutoka mashamba yetu yote 
lakini ni kipi alichoambulia kutoka ardhi ile isiyomea kitu?...........

MATUMIZI YA LUGHA 
Mwandishi ametumia lugha rahisi inayotumika kwa watu wengi,pia 
ametumia tamathali za semi,nahau,misemo na mbinu nyingi za 
kisanaa.



MISEMO NA NAHAU 
Misemo na nahau imetumika katika riwaya hii ili kuipamba kazi yake 
 “Habari njema kuchechemea kwa mguu mmoja lakini mbaya 
kukimbia kama sungura.Msemo huu unamaanisha kwamba 
habari njema hazienei haraka ila mbaya huenea haraka sana 
Pia kuna misemo mingi kama 
 Pokea upewacho 
 Maosha ni matamu
 Kanga hawezi kutua kwenye bua la mtama 
 Mume ni kiungo kwa mwanamke 

TAMATHALI ZA SEMI 
Tashibiha
Matumizi ya tashibiha yamejitokeza sehemu mbalimbali 
 Giza jepesi lilibakia ukutani kama mgeni asiyekaribishwa na 
asiyetaka kuondoka 
 Muda huenda polepole sana mithili ya mwendo wa kakakuona 
(UK 6)

Tashihisi
Mwandishi wa riwaya ya Takadini ametumia tashihisi sehemu 
mbalimbal; kama vile‟
 Ubongo wake uliathiriwa kwa mawazo yaliofukuza usingizi wake
 Fikra zilizopingana zilijichomeka katika nafsi yake 
 Mwanga wa jua ungaavu za novemba uliingia ndani na 
kulifukuza giza totoro.

Dhihaka
Mwandishi ametumia tamathali iliyoonyesha dharau na yenye lengo 
la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi lakini kwa mbinu ya 
mafumbo (uk 2)
 “Naamini ulichobeba sasa ni mtoto na si dubwasha”
Haya maneno yalimlenga Sekai kwakuwa siku zote waliamini hazai 

Tafsida
Mwandishi ametumia tamathali hii kufichaukali wa maneno (uk 83)
 Akashambulia hata sehemu za siri (UK 17)walifanya tendo la 
ndoa 
 Akajivuta karibu zaidi naye chini ya guza hawakuzungumza 
wakafanya kile ambacho kilitokea kwa asili ya maumbile 
,wakakata kiu ya hisia zilizowavuta pamoja miezi mingi (uk 117)

Takriri
 Wewe ni sope,sope,sope 
 Najua ,najua (UK 79)

Mdokezo
 Siku moja sijui lini ....lakini hivi (UK 75)
 Sukuma mara moja tena ....(UK 125) 
 Mtu mzima kama watu wengine na ameoa 


WAHUSIKA 
Takadini
 Huyu ndiye mhusika mkuu wa riwaya hii 
 Ni mtoto wa Sekai 
 Ni mlemavu wa mguu na ngozi (zeruzeru )
 Kijana wa kiume 
 Ni mchapakazi na anayependa kujituma 
 Ni mtiifu 
 Ni jasiri 
 Ni mwathirika wa mila na desturi mbaya au zilizopitwa na 
wakati 
 Anafaa kuigwa na jamii 

Sekai
 Ni mhisika mkuu 
 Ni mama yake Takadini 
 Ni mke wa kwanza wa Makwati 
 Mwanamapinduzi 
 Mwathirika wa mila na desturi zilizopitwa na wakati 
 Jasiri 
 Ni mwenye huruma 
 Ni mwenye upendo 

Makwati
Mume wa Sekai 
Baba wa Takadini 
Ni mkali 
Anapendana na mke wake 
Anashiriki mila za kale 

Chivero
Ni mzee wa makamo 
Ni mganga wa kienyeji 
Mwenye upendo 
Mwenye huruma
Ni mshauri mkuu wa Mtemi Masasa 
Mpenda mabadiliko 
Alimpokea Sekai na Takadini 

Mtemi masasa 
Mzee wa makamo 
Mtemi wa kijiji 
Mwenye heshima 
Ni mpole 
Mwenye huruma 
Mwenye wake wanne

Shingai 
Ni binti wa mzee Nhasriswa
Mke wa takadini 
Ni jasiri 
Mwanamapinduzi 
Ni msichana mwenye msimamo 
Mwenye mapenzi ya kweli na takadini 
Mpenda mabadiliko 
Ana huruma 
Anafaa kuigwa 



Tendai
Mke mdogo wa mzee Masasa 
Ni mke mkarimu 
Mwanamapinduzi 
Ni mpole
Rafiki kipenzi wa Sekai 
.
Dadirai
Mke wa tatu wa Makwati 
Ni mwenye roho mbaya 
Mpenda majanga
Ana wivu 
Ana mawazo potofu


MANDHARI
Mwandishi ametumia mandhari ya kijijini.Mandhari hii inawakilisha 
vijiji mbalimbali hapa Tanzania na Bara la Afrika.Kwa ujumla mahala 
ambapo hakuna elimu kuhusu ulemavu wa ngozi haijaeleweka vema 
au hakuna kabisa.Pia vijiji ambavyo huduma kama shule hakuna

JINA LA KITABU 
TAKADINI linasanifu yaliyomo kuwa kuna neno TAKADINI lina maana 
ya sisi tumefanya nini?Swali ambalo wahusika wengi wanajiuliza 
mfana Sekai na wanawake wasiozaa na hata vijana au watu wenye 
ulemavu.






WATOTO WA MAMAN’TILIE
Mwandishi –EMMANUELI MBOGO
Wachapishaji : Heko Publishers
Mwaka : 2002


UTANGULIZI 
“WATOTO WA MAMAN’TILIE”ni riwaya inayochambua kwa kina adha 
wanazozipata akina maman‟tilie.Hawa wakina mama wametapakaa 
mjini wakifanya biashara za kuuza vyakula ili kutafuta chochote cha 
kuweza kutunza familia zao.
Mwandishi anatueleza kuwa wakina mama hawa wanaishi maisha 
magumu,watoto wao ambao wangewasaidia hapo mbeleni hawapati 
elimu kutokana na kukosa mahitaji muhumu ya shule.Matokeo yake 
wanajiingiza kwenye vitendo viovu ikiwa ni pamoja na matumizi ya 
dawa za kulevya,wizi na biashara za madawa ya kulevya.

MAUDHUI 

DHAMIRA KUU; UMASIKINI
Hili ni suala ambalo limeongelewa kwa kiasi kikubwa katika riwaya 
hii,takribani wahusika wote wameonekana wakiandamwa na 
umasikini.Kazi zao ni za kijungujiko(ndogondogo)kiasi ambacho 
hakiwezi kuwapatia kipato cha kumudu maisha yao.
 Mfano katika familia ya MAMA NTILIE ,mwandishi anasema 
maisha hayaendi bila mama ntilie kwenda kufanya biashara katika 
genge la Urafiki ,kilichopatikana kinaishia tumboni.

Ni umasikini huu ndio unawakatili kulwa na doto ,watoto mapacha 
walioachwa yatima baada ya mama yao kufariki .Hata hivyo Doto na 
Dani wanajiingiza katika ujambazi hatimaye wanapigwa risasi na 
kufa.


DHAMIRA NDOGONDOGO
1. Suala la Malezi
Mwandishi amejadili
suala hili kwa kuwatumia 
Musa,Doto,Kulwa,Peter na Zittaanaonyesha umuhimu wa wazazi wote 
wawili katika malezi.Mfano Musa na Dani wamelelewa na mama tu 
bila baba hali kadhalika kwa Kulwa na Doto ambao hawakuwa na 
wazazi wote wawili.Hali hii pia inaonekana kwa akina Peter na Zitta 
ambao hawakupata malezi ya kutosha kutoka kwa baba kwani 
ambapo alikuwa anaondoka asubuhi kwenda kwenye pombe na 
kurudi usiku sana jambo ambalo limechangia kutoweza kutoa 
mahitaji muhimu kwa familia yake.

2. Ulevi
Mwandishi amemtumia mzee Lomolomo ambaye alikuwa mlevi wa 
gongo tangu alipoachishwa kazi kule bandarini.Mzee huyo alikuwa 
akinywa pombe bila kufanya kazi yoyote ya kumletea kipato bali 
akiamka asubuhi anakwenda kwenye vilabu vya pombe na kurudi 
usiku akiwa amelewa .Ulevi wa namna hii huchangia umasikini 
katika jamii.

3. Mapenzi 
Katika tamthiliya hii mapenzi yamejitokeza katika pande mbili yaani 
yale ya kweli na yale ya uongo 
 Mhusika Peter ambaye alionyesha mapenzi ya kweli kwa 
Kulwa na pamoja na misukosuko aliyoipata kutoka kwa dada 
yake Zitta.Peter anaonekana hakuwa na msaada .Peter 
anasema “Tungoje mama arudi lakini siwezi .....hatuwezi 
kumfukuza tutamwacha ateseke huko mitaani”
 Maman‟tilie anaonekana kuwa na mapenzi ya kweli kwa 
mumewe kwani pamoja na kwamba alikuwa mlevi wa 
kupindukia lakini bado aliweza kumfungulia mlango usiku 
aliporudi na kumpa chakula
 Kwa upande mwingine mzee Lomolomo hakuwa na mapenzi ya 
kweli kwa mkewe na familia yote kwa ujumla kwani hakutoa 
mahitaji yoyote kama baba wa familia bali alijali pombe tu.


4  Suala la Elimu 
Elimu ni suala la muhimu sana kwa taifa lolote lile lenye mipango 
endelevu.Mwandishi anatueleza kwamba Peter alipenda sana kusoma 
shule hata baada ya kufukuzwa shule kwa kukosa ada na sare lakini 
jitihada hizo ziligonga mwamba na hivyo ndoto zake hazikutimia 
sababu ya umasikini.

4. Nafasi ya Mwanamke katika jamii
Katika riwaya hii mwandishi amemchora mwanamke katika nafasi 
tofauti tofauti kama ifuatavyo;
 Mwanamke amechorwa kama mhimili wa kiuchumi na kijamii 
katika jamii,mfano mamantiliye ameonyeshwa akijishughulisha 
katika biashara ndogondogo kama vile uuzaji wa vyakula na
vinywaji baridi ili kuweza kukidhi mahitaji ya familia yake, 
mwandishi anasema kila kukicha maman‟tilie na Zitta 
wanachukua maharage,unga sufuria na kuni hadi kiwanda cha 
Urafiki kwa ajili ya kazi na kurudi hadi jioni 
 Mwanamke amechorwa kama mwenye mapenzi ya dhati,mfano 
maman‟tilie alimhurumia mumewe wakati akirudi amelewa 
pamoja na kwamba mlevi kupindukia lakini alimfungulia 
mlango na kumpa chakula.
 Mwanamke amechorwa kama mwenye upendo,huruma na roho 
ya kutoa msaada.Wanawake watatu wametumiwa na 
mwandishi kujadili suala hili,mmoja wapo ni Jane rafiki yake 
na Mama Kulwa huyu aliwahurumia watoto wa marehemu 
rafiki yake akawatunza hadi naye alipofariki.
Mwingine ni kula aliyemhurumia Peter wakati Doto alipompiga kule
kwenye jaa la taka bila sababu.
 Pia Zenabu aliyempa Peter chai na kipande cha mhogo baada ya 
kuhisi Peter alikuwa na njaa.

5. Wizi,Ujambazina Biasharaya Madawa ya Kulevya
Vitendo hivi vimeonyeshwa na mwandishi kwa kutumia wahusika 
Dani,Kulwa na Doto ambao walijiingiza katika wizi na ujambazi baada 
ya kukumbwa na umasikini, waliendakuvunja duka la Mhindi 
matokeo yake Dani na Doto wanapoteza maisha kwa kupigwa risasi 
na mlinzi wa duka hilo.
Kwa upande mwingine Musa baada ya kufukuzwa shule kwa kukosa 
ada na sare anaamua kutorudi tena shuleni na hivyo anajiingiza 
katika biashara ya madawa ya kulevya tena anamshawishi na Peter 
kushirikiana naye hatimaye wanakamatwa na polisi na kuishia jela.

MIGOGORO
 Mgogoro kati ya Peter na Doto chanzo ni Doto kumpiga Peter na 
kumfukuza alipokwenda kutafuta riziki kule jalalani,suluhisho
ni Kulwa kumuonyesha kaka yake kwamba hakufurahishwa na 
kitendo cha yeye kumpiga na kumfukuza Peter.
 Mgogoro kati ya Zita na Kulwa ,chanzo ni Kulwa kwenda kukaa 
kwa akina Zita na Peter suluhisho ni Peter kuingilia kati na 
kumueleza Zita habari za yeye kuhusiana na Kulwa.
 Mgogora wa nafsi,Kulwa ameonyesha akiwa anawaza juu ya 
maisha yake ya shida na jinsi alivyokosa mapenzi ya wazazi,hii 
ni baada ya Kulwa kuwaona watoto wawili wadogo 
wakiongozana na mama yao na kila mmoja akieleza anachotaka 
mama amnunulie mwandishi anasema Kulwa alifumbua macho 
moyo wake ukitoa chozi nafsi yake ikimsimanga na kumuuliza 
mama yuko wapi?vicheko na tabasamu zao ziko wapi?alikaa 
pale kwa muda.

MTAZAMO /FALSAFA
Mwandishi ana mtazamo wa kiyakinifu,ana upeo mpana wa kuangalia 
mambo mfano halidhiki na hali walizonazo wakina mama hapa nchini 
ambapo wanahangaika usiku na mchana kufanya biashara 
ndogondogo ili kutunza familia zao.

UJUMBE
 Uhalifu haulipi mema hivyo mtu anayetenda uhalifu hata kama 
kuna matatizo yanayomchochea kufanya hivyo mwisho wake 
hauwezi kuwa mzuri ndivyo ulivyotokea kwa wahusika 
Dani,Doto,Peter na Musa wakati Dani na Doto wanapoteza 
maisha kwa ujambazi Musa na Peter wanaishia jela 
 Wakina maman‟tilie wanakazi kubwa ya kulea familia hivyo 
jamii lazima iwasaidie kubeba mzigo huo 
 Ni muhimu wazazi wahusike katika malezi ya watoto wao 
 Ulevi si kitu kizuri hivyo jamii inayohitaji maendeleo ni lazima 
kupiga vita ulevi.

FANI 

WAHUSIKA

WAHUSIKA WAKUU
Maman’tilie(mama zita)
Ni mke wa mzee Lomolomo
Mama mzazi wa Zita na Peter 
Anajihusisha na biashara ya kuuza chakula katika genge 
la urafiki.

Mzee Lomolomo
Mume wa mama Zita
Baba yao Zita na Peter
Alikuwa mfanyakazi wa bandari kabla ya kufukuzwa kazi 
kutokana na ulevi 
Ni mlevi wa mataputapu na gongo.

Peter
Ni mtoto wa kiume wa maman‟tilie
Alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Mapepele kabla ya 
kufukuzwa shule na mwalimu Chikoya kwa kukosa ada na sare
Anapenda kusoma na alihangaika kupata ada na sare ili arudi 
shuleni lakini hakufanikiwa 
Aligeuza jaa kuwa sehemu yake ya kupa riziki 
Ni mwenye kulipa fadhila
Mwishowe alikamatwa pamoja na Musa na Kulwa kwa 
kuhusika katika biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Zita
Ni mtoto mwingine wa mzee Lomolomo 
Kama kaka yake naye alifukuzwa shule kwa kukosa sare na 
ada
Anashirikiana na mama yake kuuza chakula katika genge la 
urafiki 
Aling‟atwa na mbwa lakini hakupata matibabu yoyote jambo
 
lililopelekea kifo chake.


WAHUSIKA WENGINE
Mwalimu Chikoya
 Ni mwalimu mkuu wa shule ya Nkurumla
 Aliwafukuza wanafunzi wake wote kwa kukosa ada na sare za 
shule
Kulwa na Doto 
 Watoto mapacha ambao hawakumjua baba yao
 Waliishi kisutu kwenye banda chakavu(mbavu za mbwa)
 Wana bahati mbaya kwani mama yao alifariki wakiwa wadogo
 Maisha yao ya dhiki kwani waliishi kwa kutegemea dampo
 Doto anajiingiza katika vitendo vya ujambazi na kupoteza 
maisha kwa kupigwa risasi 
 Kulwa anakwenda kuishi kwa maman‟tilie na hata hivyo 
anaishia jela baada ya kukutwa nyumbani kwa Musa ambaye 
alikuwa anfanya biashara ya madawa ya kulevya.

Zenabu
Ni msichana ambaye ni rafiki na jirani wa maman‟tilie
Ni mfanyakazi wa klabu ya pombe panapoitwa “Kilale bar”
Ana roho nzuri kwani alikuwa anawahurumia watoto wa 
maman‟tilie
Ni yeye aliyekodi taksi kumpeleka Zita hospitali ya Muhimbili 
baada ya kuzidiwa.

Musa
 Ni mmoja wa wanajamii waliofukuzwa shule ya msingi 
Nkurumla kwa kukosa ada na sare 
 Naye hamjui baba yake amelelewa na mama tu 
 Hapendi shule kwani anaona inapoteza muda
 Anamshawishi Peter aingie kwenye biashara ya madawa ya 
kulevya mwishowe wanaishia jela.

Muundo
riwaya ya maman‟tilie ina muundo “rukia”kwani mwandishi 
anatuonyesha kisa Fulani kisha anarukia kisa kingine kile cha 
kwanza kabla hajakimalizia,mfano katika sura ya tatu mwandishi 
anatuelezaugeni wa mjomba aliyeleta taarifa/habari za ugonjwa wa 
mama yake maman‟tilie,anatuonyesha maman‟tilie anavyoondoka 
kwenda Matombo kumuona mama yake kisha anarudisha na kueleza 
habari za kuzaliwa na kukua kwa Kulwa na Doto
Riwaya hii ina sura tano zenye vijisehemu vidogovidogo.

Mtindo
Mwandishi ametumia nafsi ya tatu umoja na wingi pia matumizi ya 
nafsi ya kwanza naya pili katika vipengele vichache na ametumia 
dayalojia(UK 86na 87)
Anatumia mtindo wa fasihi simulizi ambao umetokana na matumizi 
ya nyimbo,mfano wimbo ulioimbwa na mzee Lomolomo wakati 
anarudi kutoka kwenye pombe na wimbo ulioimbwa na watu wa 
mdundiko(UK 9)
Mwandishi ametumia mtindo wa kuchanganya lugha ya kiswahili na 
kiingereza “empire” “chloroguinea” “those wine”, “queen Elizabeth”.

Matumizi ya Lugha
 Tamathali za Semi 
Tashibiha
 .....akamshika mumewe kwa mko mmoja kama bua (ni maneno 
ya mwandishi jinsi maman‟tilie alivyomshika mumewe)
 Mate yenye harufu kali ya gongo yalimtoka mdomoni kama 
cheche za moto.Mwandishi anaeleza mate yaliyomtoka 
Lomolomo mdomoni wakati aliporudi nyumbani akiwa amelewa 
 Akaanguka chini kama mgonjwa maman‟tilie alimwachia 
mumewe naye akaanguka chini 
 Hizo nywele zimekuwa kama kinda la ndege 
 Aliona ile miguu iliyopekupeku yenye ngozi ya mamba
 Mikono yake ilifanya kazi kama mashine
 Baridi ilipenya ngozini kama msumari
 Mdomo wake ulikaa kama bakuli la pombe 
 Mate yake yalisafiri na kutua kama roketi na kutua kwenye 
sikio la Peter pale chini 
 Aliinamisha shingo nayo ikapinda kama tawi la mforosadi
 Maumivu makali yalisambaa kama cheche
 Moyo ukamerimerima kama donge la barafu
 Zita alianguka chini kama gunia.

Tashihisi
“.......Miguuni alivaa raba zilizochakaa kwa huzuni.
mwandishi anaeleza raba aluzokuwa amevaa Dani 
zilivyochakaa 
Koo lilimsaliti ,mwandishi ameeleza pale Kulwa alipotaka 
kulia kwa sauti
Alirudisha kamasi ndani zikakataa
Harufu ile ilimvaa,mwandishi ameeleza harufu aliyoisikia 
Kulwa alipoingia ndani
Alisukuma mlango nao ukamwitikia labeka.

Takriri
 “Nakuacha,nakuacha maman‟tilie alimwambia Lomolomo 
wakati anamuinua aingie ndani (UK 12)
 “Baba,baba,amka baba Kulwa alimuita mzee Lomolomo baada 
ya kuona haamki (UK 91)
 Twende,twende maman‟tilie alimwambia mzee Lomolomo wakati 
aliporudi kwenye pombe akiwa amelewa
 Kukuru,kakara,kukuru,kakara wakati Zita na Peter 
wanapigana (UK 61)
 Nivione ,nivione nivione vinafanya kazi gani ?Zita alimwambia 
Peter alipomuomba pesa za kumnunulia Kulwa dawa ya 
vidonda.

TANAKALI SAUTI
 “Fyzoooio”dereva wa land river alifyonza baada ya kukwarua 
mkia wa mbwa aliyemuumiza Zita
 Alikohoa ukolio,oklio Lomolomo alikohoa wakati mkewe 
anamsaidia aingie ndani 
 Peter aliitikia salamu hizo za ukarimu kwa kupiga chafya mbili 
tatu.tcha,tcha,tcha
 Paa,paa,paa bastola ililia wakati Doto na Dani walipopigwa 
risasi walipokwenda kuiba kwenye duka la themfula



Nahau
 “Kupiga usingizi”mlinzi Simango alikuwa amelala 

Mdokezo
 “Una.....una......”
 We maazita.......una......una(Lomolomo alipotaka kuongea 
na mama Zita)

UJENZI WA TASWIRA
Mwandishi ametumia taswira za aina mbili 
 Taswira zinazoonekana
 Taswira za hisi
 Taswira zinazoonekana zimetumika pale mwandishi pale 
anapotumia mbwa mweusi mwenye mkia mweupe 
aliyemuumiza Zita na kusababisha mauti yake.
 Pia hii inasawiri barabara mazingira ya uswahilini ambako 
mbwa,mifupa na uchafu mwingi hutupwa ovyoovyo
 Taswira hisi ni pale mwandishi anaposema “hatua chache 
mbele yake sufuria ,vikombe na vyombo vingine aliona nzi 
wakirukaruka juu ya vyombo vile vichafu”
Msomaji anaposoma sehemu hii anahisi kichefuchefu kwani msomaji 
atapata picha ya mazingira halisi waishio wakina 
maman‟tilie

MANDHARI
Mwandishi ametumia mandhari ya mjinikatika jiji la Dar-es-salaam.
.Hii inathibitishwa na majina ya maneno kama Kisutu,Kiwanda cha 
Urafiki,Manzese,dampo la Tabata

JINA LA KITABU
WATOTO WA MAMAN‟TILIE kama ilivyo jina la riwaya linasadifu 
yaliyomo kwani mwandishi amejaribu kueleza jinsi wazazi hawa 
wanavyoishi maisha ya shida wao na watoto wao


    Blogger Comment

1 comments: