Maganga, (1997:iv) anatufahamisha kwamba maandishi ya
Kiswahili yalianza kutumika mapema zaidi Kenya kuliko sehemu nyingine ya Afrika
Mashariki. Tenzi nyingi za Kiswahili ziliandikwa katika Pwani ya ya Kenya kama
vile Lamu, Malindi na Mombasa. Kwa ujumla matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini
Kenya yameanza karne zilizopita.
Lahaja zitumikazo
nchini humo ni pamoja na Kimvita, Kijomvu, Kingare Kichifundi, Kivumba, Kiamu,
Kibajuni, Kipate na Kisiu. Lahaja hizi za Kiswahili ni tawi la shina kubwa la
lahaja za Kibantu zinazozungumzwa nchini Kenya.
1 Baadhi ya Sababu Zilizokwamisha Maendeleo ya
Kiswahili Nchini Kenya
Nchini
Kenya, pamoja na kwamba Kiswahili kilianza karne na karne, lakini maendeleo
yake yalikuwa duni sana wakati wa ukoloni ukilinganisha na ilivyokuwa kwa
Tanganyika. Baadhi ya sababu zilizokwamisha maendeleo ya Kiswahili nchini Kenya
ni kama ifuatavyo:
(a) Nchini
Kenya lugha ya Kiswahili haikutiliwa maanani sana katika kufundishia. Lugha za
Kienyeji zilitumika kufundishia katika Shule za Msingi. Baadaye walitumia
Kiingereza, Kiswahili kilifundishwa kama somo tu. Kutokana na hayo Kiswahili
nchini Kenya hakikupamba moto kama ilivyokuwa Tanganyika.
(b) Kiswahili kilienea sehemu za Pwani tu ya
nchi ya Kenya, watu wa Kenya Bara
hawakuwa tayari kuipokea lugha hii ya Kiswahili kwa sababu hawakuipenda;
aghalabu, waliihusisha na dini ya ki-Islamu, jambo ambalo hawakuwa tayari
kulipokea. Leo sote tunafahamu kwamba uhusishwaji wa lugha ya Kiswahili na dini
ya ki-Islamu ulikuwa wa kimakosa kwa sababu kadhaa tuzijuazo.
(c) Lugha zao za makabila makubwa kama vile Kikuyu na Kikamba waliona
watazishushia hadhi wakiongea Kiswahili
badala yake.
(d) Wamishenari wa Kenya walipenda kufundishia kwa Lugha za Kienyeji.
Kiswahili kilitumika iwapo ilikuwa lazima tu kwa kuelewana na Wageni ambao
walikuwa hawajui kilugha au Kiingereza.
(e) Kwa upande wa biashara, misafara yote ya kibiashara ambayo
aghalabu ilianzia Pwani kuelekea Bara ilikwamishwa na makabila makali, kama
vile Wamasai na Wakwavi. Makabila hayo yalizuia Wageni wasipite katika maeneo
makubwa ya Kenya, na kwa hivyo, kuyazuia
maeneo hayo yasifikiwe na misafara ya wageni hao kwa muda mrefu. Tatizo jingine
lililosababisha misafara kutoka pwani ishindwe kupenya bara la Kenya ni la
wanyama wakali katika mbuga za Tsavo.
(f) Kiswahili kilionekana kuwa lugha duni na
kutopendwa na wengi.
Asante sana kwa taarifa hii.Swali langu ni je, tunaweza je kujaza nafasi au pengo lililoachwa na mambo hayo uliotupa ili kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili pamoja na kuilinda lugha ya Kiswahili?
ReplyDeleteNaomba maelezo kuhusu sentensi tegemezi.
ReplyDelete