1 Sentensi Shurutia.
ni sentensi inayohuundwa kwa viambishii kama -ngeli-, -nge-, na -ngali-.
kwa mfano:
(1) ningelikutana naye angelinisaidia sana.
vilevile aina hii ya sentensi hutumia kiambishi -ki-;
kwa mfano:
(1) ni kimwona tu nitakwambia.
kwa mfano:
(1) ningelikutana naye angelinisaidia sana.
vilevile aina hii ya sentensi hutumia kiambishi -ki-;
kwa mfano:
(1) ni kimwona tu nitakwambia.
2 Sentesi-Sahili
Sentesi
sahili ni
kifungu cha maneno chenye kiima na kiarifu na chenye kuleta maana kamili
iliyokusudiwa. Isitoshe, hii ni sentesi ambayo haifungamani na sentesi nyingine
yo yote.
Mifano:
(i) Huu si ugonjwa wa kutisha.
(ii) Mama anapanda mahindi.
(iii) Mbunge wetu anahutubia.
Katika
sentesi-sahili (i) – (iii), zote ni
sentesi sahili ambazo kila moja ina kiima kimoja na kiarifu kimoja.Aidha, zote
huleta maana kamili.
3 Sentesi
Ambatani
Sentesi
ambatani ni
sentesi iliyoundwa ama kwa kuambatanisha au kuunganisha:
Mifano:
(a) Sentesi-sahili na Sentesi sahili;
(i)
Khamisi alifika na Asha akaimba sana.
(ii)
Mgonjwa hali wala haendi choo.
(iii)
Mama analima shambani lakini Baba yeye halimi.
(iv)
Yosefu anakunywa sana pombe ila
sigara havuti.
au
(b) Sentesi sahili na Sentesi changamani;
(i)
Khamisi alifika ukumbini na Binti aliyemwimbia akachoka.
(ii)
Mkewe hampelekei mumewe chakula
sipitalini wala waliopenda hawamletei cho chote.
(iii)
Mama mdhaifu anafanya kazi kila
siku lakini Baba
aliye na afya nzuri hafanyi kazi.
(iv)
Watu wanene hawali sana ila wembamba hula sana.
au
(c) Sentesi-changamani
na Sentesi-changamani;
(i) Khamisi alipofika ukumbini akaketi na binti aliyemwimbia akachoka baada
ya saa moja.
(ii) Wasanii walipoingia ukumbini hawakuimba wala hawakucheza
walipotakiwa kufanya hivyo.
(iii)
Mama asipofanya kazi husemwa lakini baba asipofanya kazi hasemwi.
(iv) Watu walio wembamba hula sana ila wasio
wembamba hawali sana.
.4 Sentesi
Changamani
Sentesi-changamani ni sentesi iliyoundwa kwa sentesi
sahili na tungo
tegemezi. Kwa kuwa maana ya tungo tegemezi hukamilishwa na maana ya sentesi
sahili, sentesi changamani hujitokeza kama sentesi mchanganyiko, yaani maana za
sentesi-mbili sahili zilizochanganyishwa.
Mifano:
(i) Binti ambaye hakufika jana, asimame.
(ii) Viti ambavyo vimevunjika, tutavitengeneza.
(iii) Wanaojidai shupavu, mkamfunge paka
kengele). nk.
JOIN OUR WHATSAPP MATERIAL GROUP
BOFYA👉 PRIMARY MATERIAL GROUP
BOFYA👉 SECONDARY MATERIAL GROUP
BOFYA👉 ADVANCE MATERIAL GROUP
BOFYA👉 NURSERY MATERIAL GROUP
Jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu.
MAREJELEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N.
(2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili,
Kidato cha 5 na 6. Aroplus
Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu,
Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
Amante sana !
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDeleteHivi tukisema " Sentensi shurutia" , hapo tunakuwa tumezingatia kigezo cha muundo au cha dhamira??
ReplyDeleteNinahitaji jibu