UMUHIMU WA FASIHI SIMULIZI KATIKA JAMII



(i)        Kuburudisha
Fasihi simulizi huweza kutumiwa kama burudani kwenye mkusanyiko wa jamii. Tanzu kama hadithi, ushairi, semi (methali, vitendawili, nk.) aghalabu hutumiwa ili kuwaburudisha waliokusanyika katika jamii. Kwa mfano, watoto wanapokusanyika kucheza, aghalabu hutegeana vitendawili kama njia ya kujiburudisha. Hadithi, ngano, hekaya au hata hurafa huweza pia kutambwa kama njia ya burudani.

(ii)             Kuelimisha   
Kwa kutumia fasihi simulizi, wanajamii wanaweza kuzielimisha thamani za kijamii, historia yao, utamaduni na mtazamo wao kilimwengu kutoka kizazi kimoja hadi chengine.

(iii)                       Kuipa Jamii Muelekeo
Kwa njia ya kuelimishana kimawazo yanayohusiana na tamaduni na desturi za jamii husika, wanajamii wanahakikisha kwamba jamii, kwa kutumia fasihi simulizi, inapata muelekeo utakaowabainisha wao mbali na wengine.
(iv)                        Kuhifadhi Historia na Utamaduni
Katika kuhifadhi amali muhimu za  kijamii, fasihi simulizi inakuwa nyezo muhimu. Aidha, wanajamii hufahamishwa kifasihi simulizi historia yao – wao ni nani na wanachimbukia wapi. Maarifa haya ni muhimu kwa kila mwanajamii, kwani yanamsaidia sio tu kujielewa, bali pia kujitambua.

(v)       Kuunganisha Vizazi vya Jamii                 
Fasihi simulizi ni msingi mkubwa wa kuwaunganisha wanajamii waliopo na waliotangulia mbele ya haki. Kwa kutambiwa hadithi, vitendawili, methali na nyimbo zao, umbali wa kiwakati kati ya vizazi vilivyotangulia mbele ya haki, vilivyopo na vijavyo unafupishwa kwa kiasi kikubwa sana.

(vi)            Kufundisha  
Jamii ina jukumu la kuwafundisha vijana wake maadili ya jamii ile ambayo yana adili  yaani funzo au ujumbe unaowaelekeza, kuwaadibu, kuwaonya na kuwaongoza kwenye matarajio ya jamii ile. Kwa hiyo, jamii nyingi hutumia fasihi simulizi kama njia ya kuwaelekeza na kuwafundisha vijana wake mwenendo mzuri, maadili na falsafa ifaayo ili kutunza jina na heshima ya jamii ile. Kwa mfano, katika vita dhidi ya Nduli Iddi Amini 1978/1979 nyimbo za kwaya, nyimbo za muziki wa dansi, tenzi, mashairi n.k. zilitumika kuongeza hamasa kwa askari wetu waliokuwa mstari wa mbele vitani kuwaongezea ari ya kumwadhibu adui yetu. Kitendo cha kushindwa kwa Iddi Amini katika vita vile tunaweza kusema kwamba kazi hizo za fasihi simulizi zimefaulu katika dhima yake ya kuelimisha ili kuongeza hamasa kwa askari wetu. Umuhimu wa fasihi unaonekana katika kufaulu kutatua matatizo yetu katika jamii.
                                                              
(vii)         Kuukuza Ushirikiano         
Ilivyo ni kwamba fasihi simulizi ni mali ya jamii wala sio ya mtu binafsi. Hadithi inaposimuliwa kwa hadhira kubwa, vitendawili vinapotegewa kundi pana, ni kwa sababu kimsingi fasihi simulizi ndivyo ilivyokusudiwa itumike katika muktadha wa kuvihusisha sio vikundi vidogo vidogo tu, bali pia, na hasa jamii nzima.kwa jumla.

(viii)       Kuzikuza na Kuziendeleza Stadi za Lugha         
Kwa kuwa fasihi simulizi hutegemea usemi na matamko, hatuwezi kushiriki katika kusimulia hadithi, kutegeana vitendawili, kuimba, nk. bila ya kuongea au kutamka au kuimba. Kwa sababu hii, fasihi simulizi ina mchango mkubwa wa kuboresha uwezo wetu wa kuzimiliki na kuzimudu stadi za lugha. Kwa mfano, tanzu za vitanza ulimi zilisaidia kuhakikisha kwamba utamkaji ni mzuri; utegeanaji wa vitendawili na majibu yake sahihi huukuza uwezo wa kuwaza haraka haraka na kwa usahihi. Hadithi huukuza ule uwezo wa kukumbuka maudhui.  


 



Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

23 comments:

  1. asante kaka karibu tena pia tunakaribisha maswali

    ReplyDelete
  2. This helped me a lot on my cambridge kiswahili subject cause i dont know kiswahili that much and we were given a swahili work about kazi za fasihi so this helped so much thank you mr Mwiza Peter so much

    ReplyDelete
  3. This helped a lot cause i come from a cambridge school and they gave us a swahili project to do so this helped so much i do swahili dogo dogo

    ReplyDelete
  4. Kaka kazi yako nzuri kabisa heko!

    ReplyDelete
  5. Kaka kazi yako nzuri kabisa heko!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Mwalimu kwa uthubutu wako hasa wa kutoa elimu kwa jamii. Huu ndio Uzalendo na Utaifa hasa ukiwa Mwalimu. Kutoa ni Moyo. Juhudi ya kuielimisha Jamii ni kielelezo tosha cha matumizi bora ya elimu uliyoipata. Endeleza kazi za kibunifu. Hii ndio hazina yako kuu.

    ReplyDelete
  7. NImependa sana kazi yako

    ReplyDelete
  8. Asante kwa kuwa nasi tunawapenda wote

    ReplyDelete
  9. asanta mwalimu kwa kazi nzuri Mola akubariki

    ReplyDelete
  10. Nahitaji umuhimu wa kufunza fasihi simulizi katika shule ya upili

    ReplyDelete
  11. Hongera kwa KAZI ahali kama hii Jasusi awazidishie

    ReplyDelete
  12. Can't see on the side plz put all sides clear but gd work bro

    ReplyDelete
  13. Nina swali
    Toa mifano ukieleza dhima ya fas oh I simulizi

    ReplyDelete
  14. Daaaa! Nimekipenda Sana hiui mtadao Asante Sana

    ReplyDelete
  15. Imenisaidia kuweza kupata kazi ya ziada kila kitu . Asante sana mwiza Peter kwa kuleta hii mtandao.

    ReplyDelete
  16. kazi safi kabisaa

    ReplyDelete
  17. Asante sanaa kwazi nzuri imenisaidia sana Mimi kama mwanafuzi

    ReplyDelete
  18. Asante Sana umenisaidia, kazi ya,ziada 🙏

    ReplyDelete