Jina (J) au nomino
Kama
vile: baba, mama, mwalimu, usingizi, fundi, njaa, Yusufu, Maria, nk. Majina ni
mengi, lakini yote yamegawanywa katika makundi matatu:
(a) Majina ya pekee, kama vile:
Allah
Yusufu, Maria, Iringa, nk.
Majina
ya pekee yanapoandikwa, aghalabu huanza na herufi kubwa.
(b) Majina ya jumla: majina yote yasiyo ya
pekee ambayo hutaja kitu kimoja au vitu vingi kwa pamoja, kama vile: mzazi,
mwanamke, chakula, maji, hewa, nk.
(c) Majina ya maarifa au Majina dhahania: ni majina ya vitu vya
kufikirika, au hali, kama vile: uzuri, usingizi, uhodari, wekundu, woga, utamu,
nk. Majina ya jumla na majina ya dhahania (maarifa) yanapoandikwa huanza kwa
herufi ndogo, isipokuwa yakianza sentensi au yakiwa ni kichwa ha habari.
Kivumishi (V)
Haya ni
maneno au vifungu vya maneno vinavyopambanua au kueleza zaidi, yaani kuvumisha, habari kuhusu majina. Kuna
aina nane (8) za vivumishi, navyo ni:
(a) Vivumishi vya Sifa, kama vile: -ema,
refu, kali, dogo, safi, chafu ,nk. katika: Mwalimu mwema, maji safi, kazi ndogo, nk.
(b) Vivumishi vya Idadi, kama vile: moja,
tatu, n’ne, tano, nane, sita, saba, tisa, kumi, nk. katika: Mwalimu mmoja,Walimu
watatu, ..., Niuzie kuku sita, saba,
tisa.
(c) Vivumishi vya Kuonesha au Vivumishi Vioneshi, ni maneno
yanayoonesha ujirani au umbali wa kitu au vitu. Mashina yake ni man’ne: hu-, hi-, ha-, kwa vitu vya karibu, na:
-le, kwa vitu vya mbali na –lee, kwa watu au vitu vya mbali zaidi. Kwa
mfano: mtu huyu, mtu yule, mtu yulee; watu hawa, watu wale, watu walee; vitu hivi, vitu vile, vitu vilee;...
(d) Vivumishi vya Kuuliza au Vvivumishi Viulizi,vinaashiriwa na neno gani.
Neno ‘gani’ linapotumika katika
tungo, linahitaji ‘jibu ‘ linalotaja orodha au sifa ya hicho kitu ambacho habari zake zinaulizwa, kama vile:
Mwanafunzi gani unamtaka? Jibu: mwema, hodari, wa
darasa la tatu, nk.
(e) Vivumishi vya Kumiliki au
Vivumishi Vimilikishi, ni maneno
yanayoonesha mtu au kitu/vitu ni ‘mali ya nani’. Kwa jumla, viko sita (6):
(i)
-angu
~ -etu (katika: mtoto wangu ~ mtoto wetu;
(ii)
-ako
~ -enu; (katika: mtoto wako ~ mtoto wenu;
(f) Vivumishi vya A-unganishi, vimeundwa
na vineno vidogo dogo ambavyo vinaishia na ‘a’. Vineno hivi huunganisha majina mawili,
vyenyewe vikiwa katikati, kama vile:
(i) mtu
wa hekima; (ii)
nyumba ya
Baba;
(iii) kiti cha mbao; (iv) jino la tembo;
(v) mahali
pa Babu; (vi) Chumbani
mwa Bibi; nk.
(g) Vivumishi vya Majina au
Vivumishi Majina, ni maneno ambayo
yanaleta maana ya kivumishi, na kwa hiyo yanaweza kuvumisha majina mengine,
kama vile:
(i) kipofu katika: Kijana kipofu;
(ii) mtu shujaa husifiwa;
(iii) bata mzinga;
(iv) mwaka
jana;
(v) askari
kanzu; nk..
(h) Vivumishi vya –enye, -enyewe, -ote, -ingine,
vina sifa ya kuvumisha majina au viwakilisha katika tungo, kama vile:
(i) -enye huonesha kumiliki kitu fulani katika muundo wa A-unganishi, kama vile:
Mtu
mwenye busara = mtu wa busara = mtu aliye na busara.
(ii) -enyewe huonesha na kurejesha nafsi.
◊ Mara nyingi, tendo la kuonesha na kurejesha
nafsi hutokea pamoja kama vile: ‘Mtu
amejipiga mwenyewe’; ‘Mtu
mwenyewe amejipiga’;
◊ Mara nyengine husimama
peke yake, kama vile: ‘Mwenyewe amekuja’.
(iii) -ote
huonesha umoja usiogawika =
kitu kamili kamili, kama vile:
.
Wali wote, . Mboga yote.
. Njia zote, . Swali lote.
. Mahali pote, . Chumbani
mwote, nk.
(iv) -o –ote, huonesha kila kitu, kitu cho chote kiwacho kinahusika na jambo
linalotajwa, kama vile:
·
Kalia kiti cho
chote.
·
Nenda po pote lakini tunasema:
·
Mtu, ng’ombe, kuku ye yote.
Kiwakilishi
(W)
Kiwakilishi ni
neno mojawapo linaloweza kutumika badala ya jina (J). Kama vile:
(a) Viwakilishi
vya Kuonesha au Viwakilishi Vioneshi, kwa mfano:
(i)
Huyu ameleta
asainimenti yake.
(ii)
Yule hajaileta.
Neno
huyu, yule, hapa, kule yametumika badala ya majina; yamesimama badala ya
majina; ni viwakilishi vya majina.
(b) Viwakilishi vya Kuuliza
au Viwakilishi Viulizi huashiriwa na mofu {-pi}, ambayo katika tungo, hutanguliwa
na kiambishi-ngeli cha jina husika, kama vile:
(i) Umesema
ameleta asainimenti yake yupi?.
(ii) Kauziwa
shamba letu moja? Lipi?
(iii) Ameenda
wapi?
(iv) Alikutuma
nikupe ndizi ngapi?
lakini
tunasema:
(i) Wangapi wameleta
asainimenti zao?
(ii) Vingapi vimeharibika? n.k
Aidha, maneno nani, nini na lini, kama vile:
(i) Nani kaja?
(ii) Unakula nini? Jibu
(iii) Mjomba kaja lini?
(a)
Viwakilishi
vya Kurejesha au Viwakilishi Virejeshi
vimejengwa na shina {amba-} pamoja na vipande vidogo vidogo
–ye, -o, -cho, -vyo, -lo, -po,
-mo, -ko, nk., kama vile:
(i)
Mtu ambaye amekuja, namwomba tuonane.
Neno
ambaye limetumika badala ya jina mtu.
(ii)
Neno ambalo umesema, halina mashiko.
Neno ambalo limetumika
badala ya jina neno.
(iii) Mti
ambao ameuangusha,
umetufaa sana. Neno ambao limetumika
badala ya jina mti. nk.
Elewa kwamba:
(i) vipande
vidogo vidogo –ye, -o, -cho, -vyo, -lo, -po, -mo, -ko, nk. vinachaguliwa
kulingana na ngeli ya majina
yanayorejeshwa navyo.
(ii) vipande
vidogo vidogo hivyo au silabi –ye, -cho, -lo, -po, ... vinapoongezwa ndani ya
kitenzi au mwishoni mwa kitenzi, vinawakilisha au vinasimama badala ya majina,
km.
-ye
= mtu; -cho = kitu; -lo = jambo;
-po = mahali, ...
(iii) Viwakilishi
vya kurejesha ni chombo muhimu cha kuundia
aina moja ya tungo ambazo huitwa vishazi-tegemezi.
(d) Viwakilishi
vya Nafsi, huwakilishwa na:
(i) Viwakilishi-Nafsi huru: mimi ~ sisi; wewe
~ nyinyi; yeye ~ wao.
Maneno
haya yote husimama peke yake, na yenye maana kamili yakiwa mazima hivo hivo kwa
kujitosheleza. Wala hayajiambatanishi kwenye maneno katika lugha; ni maneno
huru kabisa.
(ii) Viwakilishi-nafsi viambata: huwakilishwa na: ni- ~ tu-; u- ~
m-; a ~ wa.katika:
ni- ó
mimi; u- ó wewe
tu- ó
sisi; m- ó
ninyi/nyinyi
a-
ó
yeye wa ówao
Zingatia:
(iii) Viwakilishi hivi huitwa viambata kwa
sababu hufungwa mbele ya kitenzi:
ni (na) soma u
(na) soma
tu (na) soma m
(na) soma
a (na) soma wa
(na) soma
(iv) Viwakilishi
viambata hivi vikisimama peke yake, hufanya kazi ya neno, kwa mfano:
(a)
Mimi ni mzima. (ii) Wewe u mzima.
(b) Sisi tu
wazima.
(v) Viwakilishi-nafsi
rejeshi: huwakilishwa na: {-ji-}, {-ye-} kama vile:
(a) Nina-ji-kosoa = Mimi naikosoa nafsi yangu
(b) Wana-ji-sifu = Wao
wanazisifu nafsi zao
(c) Mna-ji-dharau= Ninyi mnazidharau nafsi zenu
.
(vi) Viwakilishi
vya kumiliki au viwakilishi vimilikishi ni kama ifuatavyo:
Umoja
Wingi
-angu -etu
-ako -enu
-ake -ao
Vitenzi (T)
Vitenzi ni maneno yanayoarifu jambo ambalo hufanywa na jina au kufanyiwa jina, kiwakilishi au kivumishi kinaposimama peke
yake kama jina.
Vitenzi
hutaja:
(i) matendo, kama vile: Mwalimu anachora.
(ii) matukio, kama vile: Simba amejificha porini.
(iii) mabadiliko, kama vile: Jamila amekua
Katika
Kiswahili, kitenzi ni neno linalobebeshwa vipashio vingi ndani yake. Kwa sababu
hii, wanaisimu hupendelea kuliita neno hili ‘kifungu-tenzi’ na kukipa alama {fT} badala ya kuliita tu kitenzi kwa alama {T}. Ieleweke tu
kwamba alama zote hizi mbili hutumika kwa maana sawa.
Vielezi (E)
Vielezi ni maneno au vifungu vya maneno
ambavyo kwa pamoja huelezea zaidi tendo au kivumishi.
Kuelezea
zaidi tendo, kwa mfano:
(i) namna gani (vipi), kama vile: Anakula wima.
(ii) mara
ngapi, kama vile: Dada anaoga mara
mbili kwa siku.
(iii) kiasi
gani
(iv) wapi
(v) lini
(vi) kwa
sababu gani
(vii) katika
mazingira gani, nk.
Kuelezea
zaidi kivumishi, kwa mfano:
(i)
(Mtu) mnene sana.
(ii)
(Mtu) mnene kupita kiasi. nk.
Viunganishi (U)
Viunganishi
(U) ni maneno
au viambishi vinavyounganisha pamoja jina na jina au tungo na tungo. Kuna aina
mbili ya viunganishi:
(a) Vihusishi, kama vilivyooneshwa katika sentensi zifuatazo:
(i) Asys na Mbaraka
wamefika.
(ii) Wamekuja pamoja na
mjomba.
(iii) Alifyeka dimba lakini hakulima.
(iv) Nilichungulia wala sikumwona.
(ii) Tumekuja
kwa sababu tuna
shida na wewe.
(iii) Tulimkuta
analima na kupanda.
(a)
Vitegemezi (viambishi), kama
vilivyooneshwa katika sentensi
zifuatazo:
(i) Alipofika
nyumbani, hakunikuta.
(ii) Juma aliendelea tu kubisha ijapokuwa
alikatazwa.
(iii) Mbaraka alizawadiwa kwa sababu amefaulu mtihani.
Vihisishi (H)
Vihisishi
(H) ni maneno
yanayodokeza vionjo vya moyo, kama vile: furaha, huzuni, uchungu, mshangao au
mshituko, huruma au laana, matumaini au kukata tamaa, nk.
Aghalabu,
vihisishi ni maneno ya mkato, na yafuatayo ni baadhi yake:
aa! asante! ee! vizuri!
hata! basi! simile! ewa!
barabara! nini! zii! sawa!
ajabu! nani! kumbe! lo!
hodi! sasa! pole! hebu!
afanaleki! ati (eti)! karibu! tena!
ebo! la hasha! vema! Je! lahaula!
Kwa
mfano:
(i)
Lo!, kasema nini huyu!
(ii) Barabara!
Nenda Bwana; haraka!
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu
MAREJEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N.
(2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili,
Kidato cha 5 na 6. Aroplus
Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu,
Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
Asante kwa somo hili ambalo ni nzuri sana kwa Kiingereza linaitwa PARTS OF SPEECH
ReplyDeleteasante na wewe karibu tena
DeletePoa mwalimu peter tuko pamoja
ReplyDelete