a)KICHWA CHA KUMBUKUMBU
Kichwa cha kumbukumbu kitaeleza mkutano unahusu nini, mahali ulipofanyika na tarehe ya
kufanyika kwake, huandikwa kwa herufi kubwa. Mfano “KUMBUKUMBU YA MKUTANO
WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KILICHOFANYIKA TAREHE 05/04/2018
KATIKA UKUMBI WA SHULE KUANZIA SAA 4:00-6:00 MCHANA.
b)MAHUDHURIO
Mwandishi anapaswa kuandika orodha ya majina yote waliofika kwenye mkutano kulingana na
vyeo vyao kwa kuanzia na yule mwenye cheo cha juu zaidi hadi kwa wanachama. Pia
wasiohudhuria waandikwe majina yao wale waliotoa hudhuru na wasiotoa hudhuru.
c)AJENDA
Mwandishi anapaswa kuandika ajenda au mambo yatakayozungumzwa katika mkutano. Mambo
yaliyojadiliwa yaandikwa kwa muhatasari na kauli ya kukataliwa au kukubaliwa iandikwe
waziwazi
d)KUFUNGUA MKUTANO
Mwenyekiti akishafungua mkutano, mwandishi au Katibu aandike saa ya kufungua mkutano na
muhtasari wa yaliyozungumzwa
e)KUFUNGA MKUTANO
Baada ya majadiliano ya ajenda, mwenyekiti afunge mkutano. Mwandishi/Katibu azingatie muda wa kufungwa kwa mkutano.
MFANO WA KUMBUKUMBU ZA MKUTANO ULIOFANYIKA MARA YA KWANZA
KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA CHAMA CHA KISWAHILI ULIOFANYIKA
KATIKA CHUMBA CHA MIJADALA TAREHE 13/06/ 2017 KUANZIA SAA TATU
ASUBUHI
1.MAHUDHURIO
Waliohudhuria ni wajumbe watano (03) na wasiohudhuria ni wajumbe watatu (03):
Waliohudhuria
i.Kapalata Hussein Mwenyekiti
ii.Vaileth Mpagama – Mweka hazina
iii.Meta Mkorofi katibu
Wasiohudhuria
i.Chinguwile Said – Naibu Mwenyekiti (Safarini)
ii.Ponea Kamgazi Msimamizi wa Mijadala (udhuru)
iii.Juma Alex (hakuna taarifa)
2.AJENDA
i.Kufungua Mkutano
ii.Uchapishaji wa jarida la Kiswahili
iii.Mengineyo
iv.Kufunga mkutano
3.KUFUNGULIWA KWA MKUTANO
Mwenyekiti alifungua mkutano mnamo saa 10:30 alasiri kwa kuwakaribisha wajumbe wote.
4.UCHAPISHAJI WA JARIDA LA KISWAHILI
Wanachama walikubaliana, Kwamba chama kitaanza kuchapisha jarida la Kiswahilina litakuwa
likichapishwa mara moja kila muhula na kuuzwa shuleni. Na kila mwanachama atachangia
katika kuandika makala na kuuza nakala za jarida hilo.
5.MENGINEYO
Wajumbe walisisitiza sana kwamba kamati iwajibike ipasavyo kuhakikisha jarida linatoka kwa
haraka
.KUFUNGA MKUTANO
Mwenyekiti alifunga mkutano kwa kuwaomba wajumbe watoe ushirikiano katika uongozi ili
jarida lifanikiwe haraka iwezekanavyo. Mkutano ulifungwa saa 12:00 jioni
Mwenyekiti…………….…… Katibu…….………………………
Sahihi……………………………… Sahihi………………………
Tarehe………………....……………. Tarehe…………………………
•Ikiwa mkutano unafanywa kwa mara ya pili au zaidi, mwandishi/Katibu hana budi
kuzingatia vipengele vifutavyo:
a.KUSOMA NA KUTHIBITISHA KUMBUKUMBU
Baada ya kufungua mkutano, kumbukumbu za mkutano uliopita zinapaswa kusomwa na
kuthibitishwa kwamba ni za kweli kisha Mwenyekiti na Katibu wanapaswa kutia saini
b.YATOKANAYO NA KUMBUKUMBU
Yatokanayo na kumbukumbu ni yale mambo yote yaliyojadiliwa kutoka mkutano uliopita. Baada
ya kusoma na kuthibitisha kumbukumbu wajumbe hujadili kuhusu yale yaliyoamuliwa
kutekelezwa. Majadiliano kuhusu yatokanayo yakishafanywa na maoni na mapendekezo
yakatolewa mwandishi hufikia hatua ya kufunga mkutano kama tulivyoona katika kumbukumbu
za mkutano wa mara ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment