(a)
Kuelimisha.
Dhima hii inatokana na ukweli kuwa kuna maudhui yenye upana katika kazi hizo
andishi; aghalabu umuhimu wa fasihi andishi katika kuelimisha hujitokeza kwenye
taasisi za elimu: shuleni, vyuoni, nk..
(b)
Kuburudisha.
Ziko kazi zinazoburudisha ambazo ni za tanzu zote tatu.
(c)
Kuadhibu
na kunasihi jamii.
Mara nyingi kazi hizo za fasihi andishi hutumika katika
kuasa na kuadhibu juu ya mambo mbali mbali yanayojitokeza katika jamii.
(d)
Kutia
hamasa, kwa upande wa ushairi na kumfanya mtu asikate tamaa.
Kwa mfano,
Kandoro(1972:138-155) aliwahi kuelezea hamasa ya wananchi waliokuwa wameungana
kama “Siafu Wamekazana”. Tunamwona pia mwandishi kwa hamasa akiwaita “Waafrika
Njooni” au “Kwetu ni Kwao kwa Nini?” Tunaona wazi kuwa kazi hizo zinajitahidi
kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni mkongwe na mamboleo.
(e)
Kupiga
vita kwa hali na mali mazingira yote ya ujinga, maradhi, njaa na umaskini.
Katika kuthibitisha hoja hii kwa mfano, tuna tamthilia kama vile Hawala ya Fedha ambayo inapambana na
maovu kama uvivu, kutojua kusoma na kuandika na mengineyo. Au tamthilia kama
vile Ngoswe inayojadili na kupiga
vita uzembe, uvivu na mengineyo. Kimsingi ndivyo ilivyo katika tanzu nyingine
za fasihi andishi.
0 comments:
Post a Comment