Ziko aina kuu tatu za viambishi vinavyonatishwa kwenye mzizi, nazo ni:
(i) Viambishi vya
Mwanzoni mwa Mzizi
Kati ya hivi Viambishi vya mwanzoni mwanzoni mwa mzizi, kuna:
(a) kile cha kwanza kabisa
ambacho kiko mbali na mzizi ambacho
hujulikana ama Kiambishi-Ngeli, au Kiambishi
cha Idadi, au Kiambishi Nafsi (mtenda, mtendwa au mtendewa).
(b) kile cha kwanza kabisa
kinachogusana na mzizi.
(c) kile kilichoko/vile
vilivyoko kati ya kile cha kwanza kabisa ambacho
kiko mbali na mzizi na kile cha kwanza kabisa kinachogusana
na mzizi.
Kwa mfano, katika neno tutampiganisha (= tu-ta-m -pig - an-ish-a) :
·
tu-ta-m-
ni viambishi vya mwanzoni mwanzoni mwa mzizi, -pig-.
·
tu- ni
kiambishi cha kwanza kabisa ambacho kiko mbali na mzizi, -pig-, (mtenda).
·
-m- ni
kiambishi cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi, -pig-, (mtendwa).
(d) -ta-
ni kiambishi kilichoko kati ya kile cha kwanza kabisa ambacho kiko mbali na
mzizi na kile cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi, -pig-, (njeo ijayo).
(ii) Viambishi vya Mwishoni
mwa Mzizi
Kati ya hivi Viambishi vya mwishoni mwa mzizi, kuna:
(a) kile
cha mwisho kabisa ambacho kiko mbali na mzizi na ambacho aghalabu huitwa
kiambishi tamatishi.
(b) kile cha mwisho, lakini
cha kwanza kugusana na mzizi.
(c) kile
kilichoko/vilivyoko kati ya kile cha mwisho kabisa ambacho kiko mbali na mzizi
na kile cha mwisho, lakini cha kwanza kugusana na mzizi.
Kwa mfano, katika neno tutampiganisha (tu-ta-m -pig - an-ish-a)
·
-an-ish-a
ni viambishi vya mwishoni mwishoni mwa mzizi, -pig-.
·
-a ni
kiambishi cha mwisho kabisa ambacho kiko mbali na mzizi, -pig-, (kiyakinishi
cha kauli).
·
-an- ni
kiambishi cha kwanza kabisa kinachogusana na mzizi, -pig-, (kitendeana cha
kauli).
·
-ish- ni
kiambishi kilichoko kati ya kile cha mwisho kabisa [a} ambacho kiko mbali na mzizi
na kile cha kwanza kabisa {an} kinachogusana na mzizi, -pig-, (kitendea cha
kauli).
0 comments:
Post a Comment