Mambo Yanayosababisha Kutokea kwa Rejesta




(i)     Ubinafsi
Ubinafsi ni tabia aliyonayo mtu, iwe ya muda au ya kudumu. Kila mtu ana namna ya kusema na kuandika au kuzungumza, ambayo humtofautisha na watu wengine. Hali hii huleta ubinafsi katika sauti yake (matamshi), msamiati, maandishi yake na mwisho huleta mtindo wa             kipekee ambao ni tofauti na watua wengine. Hii ni sababu ya kwanza inayosababisha rejesta katika lugha. Hapa tunapata rejesta za watu.

(ii)       Maingiliano
Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao. Na ili kuweza kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani fulani ambayo       hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na mambo haya huweza kuwa ya kipekee katika kundi moja tu. Mambo hayo katika lugha huhusisha matamshi ya maneno, sarufi (mpangilio wa maneno) n.k.  Tofauti hizi husababisha mitindo miwili tofauti miongoni mwa makundi hayo – hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.

(iii)     Kupita kwa Wakati
Kila mahali katika jamii, hujitokeza mitindo katika kipindi maalumu. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii fulani. Kila kipindi cha mpito wa kihistoria huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kipindi kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo, rejesta huweza kutokea kati ya kipindi kimoja na kipindi kingine. Mfano, kipindi cha enzi za Ukoloni na kile cha Uhuru, kipindi cha enzi za Azimio la Arusha na kile cha Hali Ngumu ya Maisha au,  na kile cha Mfumo wa Mageuzi.

(iv)      Shughuli Iliyopo
Hapa hutegemea ni mazingira gani ambapo shughuli hiyo inafanyikia. Mfano misikitini, makanisani, dansini, bandarini, mahakamani, shuleni, nk. Shughuli fulani katika mazingira fulani hutupatia rejesta za mahali.

(v)       Tofauti za Hadhi za Wahusika (Uhusiano wa Wahusika):
Mfano wasomi/wasiosoma, mwajiri/mwajiriwa, tajiri/maskini. Hii hali kwa ufupi husababishwa na matabaka yaliyopo katika jamii, tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha ambayo huwa ni tofauti miongoni mwao, na hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa matabaka hayo.
 (vi)     Matumizi ya Uficho/Tafsida
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta kwani husababisha mitindo mbalimbali ya lugha miongoni mwa wazungumzaji. Kwa mfano vijana wanaweza kutumia maneno haya “silaha yake haina risasi, silaha yake ni butu, silaha yake haiwezi kukata hata kipande cha mkate”  wakimaanisha kwamba “uume wake haufai”
Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

1 comments: