Kwa mujibu wa maelezo ya Masebo na Nyengwine, (2002) Kiswahili kiliingia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19. Nchi hiyo ilijipatia Uhuru wake kutoka Ubeligiji mwaka wa 1960.
Kiswahili kilianza
kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo, kuelekea kandokando ya mto Kongo.
1 Sababu za Kuenea Kwa Kiswahili Katika Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo Kabla ya Uhuru 1960
Zifuatazo ni baadhi
ya sababu zilizokifanya Kiswahili kienee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo kabla ya uhuru 1960:
(a) Wafanyabiashara
wa Kiarabu na watumwa wao ambao tayari walikuwa na umilisi katika kukizungumza
Kiswahili, waliweka vituo vyao nchini Kongo kama walivyofanya Tanganyika. Na
kama ilivyokuwa kawaida katika sehemu zote ambako wafanyabiashara waliendesha
shughuli zao, Kiswahili kilikuwa ndicho lugha muhimu ya mawasiliano.
(b) Wamishenari
(wapelelezi) wa dini ya Ki-Kristo walianzia safari zao Zanzibar na pwani ya
Tanganyika kuelekea bara ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hawa walisaidia
sio tu kuingiza lugha hiyo huko Kongo, bali pia kukiimarisha Kiswahili.
(c) Kwa
ajili ya mawasiliano ya kawaida katika sehemu nyingine, Kiswahili kilianzishwa
kwa wenyeji, kama vile: jeshini, kwenye machimbo ya shaba, na Kisangani.
Wenyeji walitakiwa kukitumia Kiswahili ili waweze kuwasiliana baina yao.
(d) Lugha
ya Kufundishia - hususan panapo mwaka 1890, katika baadhi ya Shule, kama vile
Seminari Ndogo ya Mpala huko Shaba, Kiswahili kilitumika kufundishia Sarufi ya
Kilatini, Historia ya Kanisa, Hesabu na Jiografia.
(e) Shirika
la madini laamua kukitumia Kiswahili mwaka 1906 - Shirika la Madini
lilianzishwa huko Katanga na kukusanya wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali
nchini Kongo. Lugha yao ya mawasiliano ilikuwa ni Kiswahili, na hivyo kukifanya
kiimarike na kuenea.
(f) Wamishenari
sio tu walichapisha vitabu na magazeti kwa Kiswahili, bali pia walikitumia
katika shughuli zao, na kwa hivyo walikiimarisha sana nchini Kongo.
2 Juhudi
za Kukidunisha Kiswahili Nchini Kongo Kabla ya Uhuru
Kati ya mwaka 1930 –
1940 Serikali ya Kibeligiji ilijitahidi kukipinga Kiswahili kisienee na badala
yake kutaka kukieneza Kifaransa na Kiflemishi.
3 Mbinu za Wabelgiji za Kukidunisha Kiswahili
Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Baada ya Uhuru 1960
Zifuatazo ni baadhi
ya sababu zilizokifanya Kiswahili kienee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
kongo kabla ya Uhuru 1960 kama zilivyoelezwa na Saleh na Kasisa, katika Maganga
1997:159):
(a) Sheria
namba 174 ya tarehe 17-10-1962 iliyoleta mabadiliko ya kwanza ya nchi huru
ilisema ‘Kifaransa ni lugha ya kufundishia tangu elimu ya msingi, na matumizi
ya mojawapo ya lugha za Kikongomani (yaani Kizaire), kama yanasababishwa na
umuhimu wa kielimu, yanatawaliwa na Katiba ya Kitaifa’.
(b) Kiswahili,
Kilingala, Kichiluba, Kikongo na lugha nyingine zote za kienyeji zilizokuwa
zikitumiwa, zifutwe katika Elimu ya Msingi …
4 Sura
ya Kiswahili Katika Zaire
Kwa mujibu wa
maelezo ya Saleh na Kasisa, katika. Maganga (1997:159), wanadai ‘Kiswahili
kinazungumzwa na zaidi ya makabila 120 yenye lugha mbalimbali na inatumiwa na
watu hao katika shughuli mbalimbali za kijamii’
Anaendelea kusema ‘…
ni lazima kutofautisha lahaja tatu za Kiswahili katika Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (Zaire). Kwanza, ni kile Kiswahili cha Zaire ya Juu (italiki ni ya kwangu) ambacho pia
hujulikana kwa jina la Kingwana. Pili, ni kile cha Kivu, na hasa kile cha
Manyema, ambacho hujilikana kama Kiswahili
Bora, na mwisho ni kile Kiswahili cha
Shaba.’
Aidha, anaendelea
kutufahamisha kwamba wanaisimu wa Zaire walifanya mabadiliko mwezi Mei, 1974
ambapo Kiswahili cha Zaire nzima kilipata sura mpya ambayo baadaye ilijulikana
kama Kiswahili Bora au Kiswahili Sanifu chenye umbo moja kila
mahali na katika matumizi yote… cha kuweza kufundishwa darasani kama somo
mojawapo’.
Madai haya ya mwisho
kuhusu Kiswahili bora au Kiswahili sanifu chenye umbo moja kila mahali na
katika matumizi yote cha kuweza kufundishwa darasani kama somo mojawapo si
nchini Zaire tu ambayo kwa sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, bali pia
katika nchi yo yote ambayo imekichagua Kiswahili kama ya lugha ya kutumia
katika shughuli za kila siku darasani ama nyumbani au penginepo.
NATAMANI SASA KUKIFANYIA KAZI HIKI KIITWACHO KISWAHILI SANIFU CHA ZAIRE SASA. MAANA YANGU NI TUNA VISANIFU VIWILI AMBAVYO MICHAKATO YA USANIFISHAJI WAKE INAPISHANA KWA MUDA,WAHUSIKA NA MSINGI.
ReplyDeletePIA TUNAPASWA KUHAMU MWALIMU, HICHO KISANIFU CHA ZAIRE NDICHO KILE TUSIKIACHO KIKIBANANGWA BANANGWA KATIKA MATANGAZO NA MUZIKI WAO?