KUENEA KWA KISWAHILI NCHINI BURUNDI


Kiswahili kiliingizwa nchini Burundi na Wajerumani mara walipoanza kutawala Tanganyika, Rwanda na Burundi kwa miaka thelethini (30) yaani (1885 – 1916).

1   Wakati wa Utawala wa Wajerumani (1885 – 1916)
Mnamo mwishoni mwa karne ya 19, ndipo Kiswahili kilianza kuingia nchini Rwanda wakati wa utawala wa Wajerumani. Wajerumani waliwachukua baadhi ya watumishi wao kutoka Tanganyika ambako idadi kubwa ya watu walikuwa wakizungumza Kiswahili na kuja nao mpaka Rwanda kufanya kazi. Na katika kipindi hicho, ndipo Kiswahili kilianza kuingia nchini Rwanda na kuanza pole pole kupata wazungumzaji.

2   Wakati wa Utawala wa Wabelgiji (1945 -1960)
Baada ya Wajerumani kushindwa katika Vita ya Kwanza ya Dunia (1945), nchi ya Burundi na Rwanda ziliwekwa chini ya Himaya ya Ubelgiji.
Wakati wa utawala wa Wabelgiji, kuenea kwa Kiswahili nchini Burundi kulikumbwa na matatizo mengi.

3   Mbinu za Wabelgiji za Kukidunisha Kiswahili Nchini Burundi
Aghalabu watawala hao wa kibelgiji badala ya kikiendeleza Kiswahili, walikuwa wakitafuta mbinu kadhaa na kuzitumia kukidunisha Kiswahili nchini Burundi ili kisiendelee kama ifuatavyo:

(a)       Dharau - lugha ya Kiswahili haikutiliwa mkazo waliouanzisha Wajerumani; mafunzo ya Kiswahili yalipungua sana; waliidharau.

(b)       Wabelgiji walitilia mkazo zaidi mafunzo ya lugha ya Kifaransa na Kiflemishi badala ya Kiswahili.

 (c)      Waarabu wa mji wa Bujumbura, watumwa na wafuasi wao tu, yaani wenyeji wa Kiafrika (Wabantu) ndio waliokizungumza Kiswahili, tena majumbani mwao tu.

(d)       Udini nao ulikuwa sababu kubwa ya kukidunisha Kiswahili huko Burundi. Kwa kuwa Wabeligiji walikuwa ni Wakristo, kwa upande mmoja, na kwa upande mwengine, Waarabu wa mji wa Bujumbura, baadhi ya watumwa na wafuasi wao ni Waislamu, hivyo Kiswahili kilizuiliwa kisienee, kwani Wabelgiji waliwachukia Waarabu na Waislamu kwa ujumla.
4   Juhudi za Kukuza Lugha ya Kiswahili Nchini Burundi
Juhudi kubwa za kuikuza lugha ya Kiswahili nchini Burundi zilianza kuonekana hasa tangu mwaka 1963 ambapo hatua madhubuti zilichukuliwa na Serikali kama ifuatavyo:
(a)    Habari za ‘vipindi vya salamu’ mbalimbali vilianza kusikika katika Redio Burundi.

(b)    Serikali iliingilia kati na kuwataka wananchi wazungumze Kiswahili.

(c)    Serikali iliamua Kiswahili kianze kufundishwa vyuoni, kwa kuanza na Chuo cha Wanajeshi cha Bujumbura, mwaka 1965, na baadaye Chuo Kikuu cha Bujumbura.

(d)    Katika Taasisi ya mabwana fedha, taasisi ya mawasiliano ya simu, Kiswahili kilifundishwa vile vile.

(e)    Kwa mujibu wa maelezo ya Halid Hassan, katika Maganga        (1997:1600), Wakimbizi wa ki-Rundi waliokimbilia Tanzania mnamo mwaka 1970 na baada ya miaka kadhaa kurejea tena makwao Burundi wameonesha kuwa na umilisi mkubwa wa lugha ya Kiswahili.
Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

1 comments:

  1. Asante kwa hii habari. Tafadhali tueleze hali ya lugha ya Kiswahili ilivyo sasa nchini Burundi.

    ReplyDelete