(i) Ubinafsi
Ubinafsi ni tabia aliyonayo mtu,
iwe ya muda au ya kudumu. Kila mtu ana namna ya kusema na kuandika au
kuzungumza, ambayo humtofautisha na watu wengine. Hali hii huleta ubinafsi katika
sauti yake (matamshi), msamiati, maandishi yake na mwisho huleta mtindo wa kipekee ambao ni tofauti na watua
wengine. Hii ni sababu ya kwanza inayosababisha rejesta katika lugha. Hapa
tunapata rejesta za watu.
(ii) Maingiliano
Makundi ya watu mbalimbali
yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao. Na ili kuweza
kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani fulani ambayo hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na
mambo haya huweza kuwa ya kipekee katika kundi moja tu. Mambo hayo katika lugha
huhusisha matamshi ya maneno, sarufi (mpangilio wa maneno) n.k. Tofauti hizi husababisha mitindo miwili
tofauti miongoni mwa makundi hayo – hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.
(iii) Kupita kwa Wakati
Kila mahali katika jamii,
hujitokeza mitindo katika kipindi maalumu. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya
kihistoria yanayoikumba jamii fulani. Kila kipindi cha mpito wa kihistoria
huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha
kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kipindi
kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo, rejesta huweza kutokea kati ya kipindi
kimoja na kipindi kingine. Mfano, kipindi cha enzi za Ukoloni na kile cha
Uhuru, kipindi cha enzi za Azimio la Arusha na kile cha Hali Ngumu ya Maisha
au, na kile cha Mfumo wa Mageuzi.
(iv) Shughuli Iliyopo
Hapa hutegemea ni mazingira gani
ambapo shughuli hiyo inafanyikia. Mfano misikitini, makanisani, dansini,
bandarini, mahakamani, shuleni, nk. Shughuli fulani katika mazingira fulani
hutupatia rejesta za mahali.
(v) Tofauti za Hadhi za Wahusika (Uhusiano wa Wahusika):
Mfano wasomi/wasiosoma,
mwajiri/mwajiriwa, tajiri/maskini. Hii hali kwa ufupi husababishwa na matabaka
yaliyopo katika jamii, tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha ambayo huwa
ni tofauti miongoni mwao, na hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa
matabaka hayo.
(vi) Matumizi
ya Uficho/Tafsida
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta
kwani husababisha mitindo mbalimbali ya lugha miongoni mwa wazungumzaji. Kwa
mfano vijana wanaweza kutumia maneno haya “silaha yake haina risasi, silaha
yake ni butu, silaha yake haiwezi kukata hata kipande cha mkate” wakimaanisha kwamba “uume wake haufai”
Thank you for your kindness
ReplyDelete