3.2.1 Maana Ya Fonetiki
Fonetiki ni taaluma inayojishughulisha na jinsi sauti yo yote inavyotolewa au
inavyopatikana. Hii ni sayansi huru ambayo inatumia nadharia za sayansi halisi
kama vile fizikia, uhandisi, baiolojia, nk. na kufaidi matokeo ya kiutafiti ya
taaluma hizi. Mathalani, ili mwanafonetiki aelewe jinsi ala za sauti
zinavyofanya kazi wakati wa utolewaji wa sauti, atafaidika na maelezo ya
kibaiolojia kuhusu namna mfumo wa mwili wa mwanadamu unavyofanya kazi.
Mgulu, (2001:48) anadai: ‘ ... fonetiki ni moja tu, lakini fonolojia zipo
nyingi kama lugha zenyewe zilivyo nyingi. Kwa mfano, hatuna fonetiki ya Kiingereza
au fonetiki ya Kiswhili. Fonetiki ni fonetiki tu. Kwa upande mwingine, tuna
fonolojia za lugha mbalimbali ambazo hutofautiana. Tunazo, kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya
Kiingereza, fonolojia ya Kifaransa, fonolojia ya Kinyamwezi, fonolojia ya
Kindendeule, nk.
Tunapozungumzia upatikanaji wa sauti za lugha za binadamu, tunafafanua
jinsi sauti za lugha husika zinavyotamkwa katika bomba la sauti la mwanadamu.
(Tazama Jedwali 3.5). Tunazibainisha ala, hususani alasogezi na alapahala husika katika kuitamka
sauti husika. Alasogezi ni ile ala ambayo inaweza kujimudu wakati wa utamkwaji
wa sauti husika. Alapahala au Ala-tuli ni ile ala ambayo haiwezi kujimudu
wakati wa utamkwaji wa sauti husika.
(Tazama Kielelezo 3.1). Ni alasogezi ambayo hujisogeza kwenye alapahala husika
wakati wa utamkwaji wa sauti husika (Nchimbi, 1979).
3.2.2 Utamkwaji
wa Sauti-Fonimu za Kiswahili
Ieleweke
kwamba hewa itokayo kwenye chemba ya mapafu ambayo sisi sote twaitumia kwa
kupumua ili tuishi, ndiyo hiyo hiyo itumikayo katika utamkwaji wa sauti za
lugha za binadamu. Hewa hiyo itapitishwa kwenye chemba zilizomo katika bomba la
sauti kwa mujibu wa sauti inayotarajiwa kutamkwa hadi nje ya bomba la sauti kwa
kupitia chemba ya midomo au chemba ya pua
Hewa hiyo
ikipitia chemba ya pua tu au chemba ya pua na chemba ya midomo, basi hisia za
sauti itakayotamkwa zitakuwa za sauti-ng’ong’o. Alasogezi ya kidaka-tonge huwa
imejishusha kutoka kwenye ukuta wa marakaraka (paroi pharangale) ili hewa hiyo
ipate ku
Lakini
hewa hiyo, isipopitia chemba ya pua, ikapitia chemba ya midomo tu hadi nje,
basi hisia za sauti itakayotamkwa zitakuwa za sauti-sing’ong’o. Alasogezi ya
kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo
ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. (Tazama Kielelezo
3.4).
Tutaanza
kufafanua utamkwaji wa sauti-fonimu-irabu za Kiswahili, ukifuatiwa na ufafanuzi
wa utamkwaji wa sauti-fonimu-konsoni za Kiswahili. Ufafanuzi utafanywa kwa
kuzingatia vigezo vin’ne, navyo ni:
(a) utamkwaji ki-alapahala,
(b) utamkwaji ki-sampuli,
(c) utamkwaji ki-ughuna,
(d) utamkwaji ki-ung’ong’o na,
(e) msimamo wa midomo hususani kuhusu
utamkwaji wa fonimu-irabu.
3.2.3 Utamkwaji
wa Fonimu-Irabu-Mama za Lugha za Binadamu
Irabu-mama
katika lugha zote za binadamu ni /i a u/ ambazo utamkwaji wake katika bomba la
sauti unajitokeza kwenye alapahala ya burutio-gumu/kaakaa-gumu ikishirikiana na
alasogezi ya ulimi-kati ki-alasogezi-pahala kama ilivyo kwenye Kielelezo 3.5.
Katika Kielelezo
3.5 alasogezi-pahala za irabu, irabu-mama /I/ inajidhihirisha kuwa ni ya
juu-mbele wakati irabu-mama /U/ ni ya juu-nyuma. Irabu-mama /A/ ni ya
chini-kati.
Vigezo
vya kufafanulia matamshi ya irabu ni kama ifuwatavyo:
(i) Kwa
Mujibu wa Alapahala:ni burutio-gumu; ama sehemu ya mbele, ama sehemu ya kati,
ama sehemu ya nyuma ya burutio-gumu.
(ii) Kwa
Mujibu wa Alasogezi: ni ulimi; ama sehemu ya mbele (ulimi-mbele), ama sehemu ya
kati (ulimi-kati), ama sehemu ya nyuma ya ulimi (ulimi-nyuma).
(iii) Kwa Mujibu wa Midomo: ni ama midomo-tandazi au midomo-futuzi.
(iv) Kwa Mujibu wa Mpenyo: ni ama mpenyo-mwembamba, ama
mpenyo-mwembamba-kiasi, ama mpenyo-mpana.
(v) Kwa Mujibu wa Kidaka-Tonge: ni ama irabu-ng’ong’o ama
irabu-sing’ong’o
(vi) Kwa Mujibu wa Nyuzi za Sauti/Glota: ni ama irabu-ghuna ama
irabu-sighuna.
3.2.4 Utamkwaji
wa Fonimu-Irabu //i e a o u/
Fonimu-irabu
za kiswahili sanifu ni /i e a o
u/. Fonimu-irabu-mbele za kiswahili sanifu ni /a e i/ na fonimu-irabu-nyuma
ni /a o u/. Fonimu-irabu na nusu-irabu-mbele /a e i j/.
Wakati wa
utamkwaji wa fonimu-irabu-mbele / a e i /, alasogezi ya ulimi-kati hujikweza
kuelekea kwenye alapahala ya burutio-gumu-mbele. Mpenyo unaofanyizwa kati ya
alasogezi ya ulimi-kati na alapahala yake ya burutio-gumu-mbele ni mpana wakati
wa matamshi ya sauti-endelezi ya irabu [a], ni mpana kidogo wakati wa matamshi
ya sauti-endelezi ya irabu [e] na ni mwembamba wakati wa matamshi ya
sauti-endelezi ya irabu [i].
Mpenyo
huu wa matamshi ya sauti-endelezi ya irabu [i] unapofanyizwa kuwa mwembamba
zaidi , basi matamshi ya sauti-endelezi ya nusu-irabu [j] hudhihirika, yaani [a
e i j]. Aidha, midomo hubakia tandazi
(Nchimbi,1979). Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na
kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya
hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o.
Utamkwaji
wa Fonimu-Irabu na Nusu-Irabu-Nyuma /a o u w/:Wakati wa utamkwaji wa
fonimu-irabu-nyuma / a o u /, alasogezi ya ulimi-kati hujikweza kuelekea kwenye
alapahala ya burutio-gumu-nyuma. Mpenyo unaofanyizwa kati ya alasogezi ya
ulimi-kati na alapahala yake ya burutio-gumu-mbele ni mpana wakati wa matamshi
ya sauti-endelezi ya irabu [a], ni mpana kidogo wakati wa matamshi ya sauti-endelezi
ya irabu [o] na ni mwembamba wakati wa matamshi ya sauti-endelezi ya irabu [u].
Aidha, alasogezi ya mdomo-chini na alapahala
ya mdomo-juu hujifutua, na kwa hiyo, kufanyiza mpenyo aina ya mviringo.
Mpenyo
huu wa matamshi ya sauti-endelezi ya irabu [u] unapofanyizwa kuwa mwembamba
zaidi, basi matamshi ya sauti-endelezi ya nusu-irabu [w] hudhihirika, yaani [a
o u w], na midomo hubakia futuzi.
Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa
marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua.
Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o.
Kielelezo 3.7: Alasogezi-Pahala
za Irabu na Nusu-Irabu za Burutio-Gumu-Nyuma na Midomo-Futuzi [o u w]
Tija
itokanayo na mfumo wa matamshi ya sauti-irabu za kiswahili sanifu: maelezo
yanayotokana na (a) utamkwaji wa fonimu-irabu za burutio-gumu-mbele [a e
i] na nusu-irabu [j] na (b) utamkwaji wa fonimu-irabu za
burutio-gumu-nyuma [ o u] na nusu-irabu
[w], yanatuwezesha kufanyiza (i) Jedwali ya mfumo wa matamshi ya irabu za
kiswahili sanifu [i e a o u], (ii) Tarapezi ya mfumo wa irabu za kiswahili
sanifu [i e a o u], na (iii) Jedwali la mfumo wa matamshi ya nusu-irabu/konsoni
za kiswahili sanifu [j w], kama ilivyo katika Jedwali 3.6.
Jedwali 3.6:
Jedwali ya Mfumo wa Matamshi ya Irabu za Kiswahili
Sanifu [i e a o u]
ALAPAHALA
YA KITAMKWA
|
||||
Burutio-gumu
Mbele.
|
Burutio-Gumu
Kati.
|
Burutio-Gumu
Nyuma
|
||
MPENYO
|
i
|
u
|
UNG’ONG’O
|
|
Mwembamba
(Juu)
|
Sing’ong’o
|
|||
Mpana Kiasi
(Kati)
|
e
|
o
|
||
Mpana
(Chini)
|
a
|
|||
Ulimi-kati mbele
Midomo-tandazi/sifutuzi
|
Ulimi-kati nyuma
Midomo-futuzi/sitandazi
|
|||
ALASOGEZI
YA KITAMKWA
|
Kielelezo
3.8: Tarapezi ya Mfumo wa Irabu za Kiswahili Sanifu [i e
a o u]
Jedwali 3.7:
Jedwali ya Mfumo wa Matamshi ya Nusu-Irabu/Konsoni
za Kiswahili Sanifu [j w]
MSIMAMO
WA MIDOMO
|
ALAPAHALA
YA KITAMKWA
|
UGHUNA
|
|
BURUTIO-GUMU
|
BURUTIO-LAINI
|
||
Midomo
tandazi
|
J
|
Ghuna
|
|
Midomo
futuzi
|
w
|
||
Ulimi-Kati Ulimi Nyuma
|
|||
ALASOGEZI
|
ZOEZI
1. Zitaje chemba (cavities) zinazolijenga bomba la sauti la
mwanadamu.
2. Zitaje alasogezi
(articulators) zilizomo katika bomba la sauti la mwanadamu.
3. Zitaje alapahala (places
of articulation) zilizomo katika bomba la sauti la mwanadamu.
4. (a) Tofautisha
matamshi ya irabu-mbele na irabu-nyuma.
(b) Eleza tofauti kati ya matamshi ya irabu [i] na nusu-irabu [j],
au irabu [u] na nusu-irabu [w].
5. Eleza tofauti kati ya alasogezi na alapahala.
|
3.2.5
Utamkwaji wa Sauti-Fonimu-Konsoni za Kiswahili Sanifu
Utamkaji
wa fonimu-konsonanti za Kiswahili utafafanuliwa kwa mujibu wa vigezo vinne:
utamkaji ki-alapahala, utamkaji ki-sampuli, utamkaji
ki-ughuna, na utamkaji ki-ung’ong’o.
(i) Utamkwaji
wa Sauti-Fonimu-Konsoni za Kiswahili Ki-Alasogezi-Pahala
Fonimu-konsoni
zote ishirini na tisa (29) za Kiswahili sanifu hudhihirishwa kimatamshi kwa
kutumia alapahala saba (7) ambazo nazo huhusishwa moja kwa moja na alasogezi
husika zilizomo katika bomba la sauti (Nchimbi, 1979), kama ifuatavyo:
Utamkwaji wa Vimidomo [p, b]: Wakati wa matamshi ya sauti za midomoni [p, b], alasogezi ya
mdomo-chini hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya mdomo-juu kiasi kwamba
mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya
bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka,
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o. (Tazama
Kielelezo 3.8).
Utamkwaji wa Vimdomochini-Menojuu [f v]: Wakati wa matamshi ya vimdomochini-menojuu [f] na
[v], alasogezi husika ambayo ni mdomo-chini, hujikweza na, ama kujibandika
kwenye alapahala ya meno-juu, au hujisogeza na kuacha nafasi finyu kiasi kwamba
mkondo wa hewa utokao mapafuni hujipenyeza kwa taabu kadiri unavyopitishwa
katikati ya nafasi finyu inayofanyizwa kwa mdomo-chini na meno-juu, au kati ya
jino na jino wakati mkondo huo unapoelekezwa n’nje ya bomba la sauti kwa
kupitia chemba ya midomoni.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o.
Utamkwaji
wa Viulimincha-Menojuu [θ ð]:
Wakati wa matamshi ya viulimincha-menojuu [θ]
na [ð], alasogezi
ya ulimi-ncha hujisogeza kwenye
alapahala ya meno-juu na kuacha nafasi finyu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao
mapafuni hujipenyeza kwa taabu kadiri unavyopitishwa katikati ya nafasi finyu
inayofanyizwa kwa ulimi-ncha na meno-juu wakati mkondo huo unapoelekezwa nje ya
bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomoni.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o.
Utamkwaji wa viulimincha-ufizijuu [t d s z ]: Alasogezi ya ulimi-ncha na alapahala ya ufizi-juu ndizo zinazotumika
wakati wa matamshi ya viulimincha-ufizijuu. [t d
s z
r l].
Utamkwaji
wa [t d]: Alasogezi ya ulimi-ncha
inajikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ufizi-juu; mkondo wa hewa utokao
mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia
chemba ya midomo.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika ndii... kwenye ukuta wa
marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua.
Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o. Kwa mantiki hii, viulimincha-ufizijuu vinavyotamkwa ni [t d ].
Utamkwaji
wa [s z]: Wakati alasogezi ya ulimi-ncha
inapojisogeza kiasi cha kuacha nafasi finyu kati yake na alapahala ya
ufizi-juu, mkondo wa hewa utokao mapafuni hupata nafasi ya kupenya kuelekea
n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [s z ].
Utamkwaji
wa Viulimikati-Burutiogumu [c ɟ ʃ j]:
Utamkwaji wa [c ɟ]
Wakati wa matamshi ya viulimikati-burutiogumu [c ɟ], alasogezi ya ulimi-kati, hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya
burutio-gumu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya
kupenya kuelekea n’nje ya Bomba la Sauti kwa kupitia chemba ya midomo.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [c ɟ].
Utamkwaji
wa [ʃ j]: Wakati wa
matamshi ya viulimikati-burutiogumu [ʃ j ]; alasogezi ya ulimi-kati
hujisogeza kiasi cha kuacha nafasi finyu kati yake na alapahala ya burutiogumu.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [ʃ j].
Utamkwaji
wa Viuliminyuma-Burutiolaini [k g Ɣ]:
Wakati wa matamshi ya viulimikati-burutiogumu
[k g], alasogezi ya ulimi-nyuma,
hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya burutio-gumu-nyuma kiasi kwamba
mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya
bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [k g], Tazama Kielelezo 3.15.
Unapojitokeza wakati wa matamshi ya [Ɣ], alasogezi ya
ulimi-nyuma hujisogeza kiasi cha kuacha nafasi finyu kati yake na alapahala ya
ukuta wa marakaraka au ncha ya kidaka-tonge. Nafasi hii itaruhusu mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa
kupitia chemba ya midomo. Midomo hubakia tandazi itamkwapo sauti [Ɣ]
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [Ɣ]
Utamkwaji
wa Kiglota [h]: Wakati wa matamshi ya kiglota [h], alasogezi ya
ulimi hubakia chini kiasi cha kuacha nafasi kubwa kati yake na alapahala ya
burutio. Mkondo wa hewa kutoka mapafuni unapopita katika chemba ya koromeo,
nyuzi sauti zilizomo katika chemba hiyo ama hurindima na ikapatikana sauti [ h
], au hazirindimi na kupatikana sauti [h]. Aidha , mkondo huu wa hewa kutoka
mapafuni hupitishwa moja kwa moja katika chemba ya kinywa bila kizuizi mpaka
n’nje ya kinywa. Kwa mantiki hii, nyuzi sauti zinaweza kueleweka
kama alasogezi ya matamshi ya sauti [h] ya fonimu /h/.
Midomo hubakia tandazi itamkwapo sauti [h]. Na alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [h]
(ii) Utamkaji
wa Sauti za Fonimu za Kiswahili
Ki-Sampuli
Utamkwaji
wa sauti ki-sampuli unabainisha kati ya sauti-endelezi na sauti-sendelezi. Utamkaji wa sauti ki-sampuli ni ule
unaosababishwa na alasogezi ya ulimi na mdomo-chini inaponyanyuka kuelekea
kwenye alapahala husika. Ulimi au mdomo-chini unaponyanyuka kuelekea kwenye
alapahala husika, husababisha matamshi ya sampuli za sauti zifuatazo:
Sauti-sendelezi-konsoni ambayo wakati wa utamkwaji wake,
alasogezi husika hujikweza na kujibandika
kwenye alapahala husika; ambayo kwa [p b ] ni
mdomo-juu, kwa [t d] ni
ufizi-juu, kwa [c ɟ ] ni
burutio-gumu-mbele na kwa [k g N] ni burutio-gumu- nyuma kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye chemba
ya koromeo haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti.
Kuzuiliwa kwa mkondo huu wa hewa ni kwa muda mfupi sana. Kwa mantiki hii
utamkaji wa sauti-konsonanti-katizi hauendelezeki. Mifano ya
sauti-konsonanti-katizi katika Kiswahili ni [p b t d c ɟ k g ].
Sauti-endelezi-konsoni-madende ambayo wakati wa utamkaji wake,
alasogezi ya ulimi-ncha hujikweza na
kujibandika kwenye alapahala ya ufizi-juu, kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao
kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la
sauti. Kuzuiliwa kwa mkondo huu wa hewa ni kwa muda mfupi
sana. Kwa mantiki hii, alasogezi ya ulimi-ncha huonekana ikiyumbishwa kana
kwamba inajigongagonga kwenye matuta ya alapahala ya ufizi-juu. Aidha, utamkaji
wa sauti hii huwa katizi unaoendelezeka kwa vigongo, yaani, kimadende.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya
sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o. Mfano
wa sauti-konsonanti-madende-endelezi ni [r].
Sauti-Endelezi-Konsoni-Kwama
Kwamizi ambayo wakati wa utamkwaji wake, alasogezi husika hujikweza na kuunda mpenyo mwembamba sana kwenye alapahala husika, kiasi
kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye chemba
ya koromeo hupita, lakini kwa hukwamizwa kwamizwa, unapoelekea n’nje ya Bomba
la Sauti. Matokeo yake ni matamshi ya sauti-konsonanti-endelezi kwama kwamizi,
kama vile: [f v θ ð s ʃ [Ɣ]
h]
Sauti-endelezi-konsonanti-tambazi
ambayo wakati wa utamkaji wake, alasogezi ya ulimi-ncha hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ufizi-juu, kiasi kwamba
sehemu ya mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi hapo
kwenye alapahala ya ufizi-juu ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti, na
sehemu iliyobakia ya mkondo huo wa hewa huchepukia pembezoni mwa ulimi na
hatimaye kuelekea n’nje ya bomba la sauti.
Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka
kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua.
Kwa
mantiki hiyo, hisia za n’nje zinazosikika ni za aina ya sauti-endelezi
sing’ong’o ambapo hewa yake inatambaa.
Mfano wa hii sauti-konsonanti-tambazi ni [l].
3.2.6
Utamkwaji wa Sauti za Fonimu za Kiswahili Ki-Ughuna
3.2.6.1 Utangulizi
Utamkwaji
wa sauti ki-ughuna unabainisha kati ya sauti-ghuna ambayo husababisha nyuzi za sauti/glota
zilizomo kwenye chemba ya koromeo zitetemeke, yaani hisia ya kwenye chemba ya
koromeo [KO] huwa ya mawimbi-mawimbi, yaani:
[KO: ], na sauti-sighuna ambayo haisababishi nyuzi za
sauti/glota zilizomo kwenye chemba ya koromeo zitetemeke, na kwa hivyo, hisia
inayojitokeza si ya mawimbi-mawimbi,
yaani: [KO:___________]. Aidha, hisia za sauti-sighuna hazijitokezi kwenye Chemba ya Pua
[PU:____________], wala kwenye chemba ya kinywa [KI:__________] wala kwenye Hisi
N’nje [NJE:________]. Tazama kwa mintarafu ya Kielelezo 3.19.
Kielelezo 3.19: Utamkwaji Wa Sauti-Ghuna
Na Sauti-Sighuna, Kwa Mfano, Katika Neno “Sasa” Kwenye Mingogramu (Mingo)
Ufasili
wa Mingo hii ya Neno “Sasa”:
(a) Sauti [s]:
(i) ni sauti sighuna kwa kuwa nyuzi sauti/glota
hazioneshi ishara ya kutetemeka/mawimbi-mawimbi kwenye msitari wa chemba ya
koromeo, yaani: [KO: ___________]
(ii) ni sauti sing’ong’o kwa kuwa nyuzi
sauti/glota hazioneshi ishara ya kutetemeka/mawimbi-mawimbi kwenye msitari wa
chemba ya pua, yaani: [PU:_______].
(b) Sauti [a]:
ni sauti ghuna
kwa kuwa nyuzi sauti/glota zinaonesha ishara ya kutetemeka/mawimbi- mawimbi
kwenye msitari wa chemba ya koromeo, yaani: [KO: ]
Utamkwaji
wa sauti-ghuna-sing’ong’o-endelezi za Kiswahili sanifu: Katika Kiswahili
sanifu, sauti-ghuna-sing’ong’o-endelezi zinazojitokeza ni [a], [e], [i], [o], [u], [v], [ð], [z], [r], [l], [j], [Ɣ]. Sauti-ghuna hizi ndizo zinazosababisha
nyuzi za sauti/glota zilizomo kwenye chemba ya koromeo zitetemeke, yaani hisia
ya kwenye Chemba ya Koromeo [KO] huwa ya mawimbi-mawimbi, yaani: [KO: ].
Kumbuka
kwamba wakati wa utamkwaji wa sauti-ghuna,
alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa
marakaraka, kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua
wakati wa utamkwaji wa sauti-ghuna-sing’ong’o-endelezi.
(iv) Utamkwaji
wa Sauti za Fonimu za Kiswahili Ki-Ung’ong’o
Hewa hiyo
inayotoka mapafuni, ikipitia chemba ya pua tu au chemba ya pua na chemba ya
midomo, basi hisia za sauti itakayotamkwa zitakuwa za sauti-ng’ong’o. Alasogezi
ya kidaka-tonge huwa imejishusha kutoka kwenye ukuta wa marakaraka (paroi
pharangale) ili hewa hiyo ipate kupita na kutoka n’nje ya bomba la sauti.
Utamkwaji
wa Sauti-Konsoni-Ghuna-Ng’ong’o-Endelezi
[m]: Wakati wa matamshi ya sauti ya
midomoni [m], alasogezi ya mdomo-chini hujikweza na kujibandika ndii... kwenye
alapahala ya mdomo-juu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati
nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya
midomo. Lakini wakati huo, alasogezi ya kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye
alapahala ya ukuta wa marakaraka na
kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza
mpaka kwenye chemba ya pua; sauti-ghuna-ng’ong’o-endelezi [m]
hudhihirishwa na ikadhihirika.
Utamkwaji
wa Sauti-Konsoni-Ghuna-Ng’ong’o-Endelezi
[n]: Alasogezi ya ulimi-ncha na alapahala ya ufizi-juu ndizo ala
zinazotumika wakati wa matamshi ya kiulimincha-ufizijuu [n] ambayo ni sauti-konsoni-ghuna-ng’ong’o-endelezi.
Wakati wa matamshi ya sauti ya kiulimincha-ufizijuu [n], alasogezi ya
ulimi-ncha hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ufizi-juu kiasi kwamba
mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya
bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo. Lakini wakati huo huo, alasogezi
ya kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya pua; sauti-ghuna-ng’ong’o-endelezi
[n] hudhihirishwa na ikadhihirika.
Utamkwaji
wa Sauti-Konsoni-Ghuna-Ng’ong’o-Endelezi
[ɲ]: Alasogezi ya ulimi-kati na alapahala ya burutio-gumu(kaakaa-gumu)
ndizo ala zinazotumika wakati wa matamshi ya kiulimi-kati [ɲ] ambayo ni sauti-konsoni-ghuna-ng’ong’o-endelezi.
Wakati wa matamshi ya sauti ya kiulimi-kati [ɲ], alasogezi ya ulimi-kati hujikweza na kujibandika
kwenye alapahala ya burutio-gumu kiasi
kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje
ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo. Lakini wakati huo huo, alasogezi
ya kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya pua; sauti-ghuna-ng’ong’o-endelezi
[ɲ], hudhihirishwa na ikadhihirika.
Utamkwaji
wa Sauti-Konsoni-Ghuna-Ng’ong’o-Endelezi [ŋ]: Alasogezi ya ulimi-kati na
alapahala ya burutio-laini(kaakaa-laini) ndizo ala zinazotumika wakati wa
matamshi ya kiulimi-kati [ŋ] ambayo ni sauti-konsoni-ghuna-ng’ong’o-endelezi.
Wakati wa matamshi ya sauti ya kiulimi-kati [ŋ], alasogezi ya ulimi-kati hujikweza na kujibandika
kwenye alapahala ya burutio-gumu kiasi
kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje
ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo. Lakini wakati huo huo,
alasogezi ya kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa
marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa
mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya
pua; sauti-ghuna-ng’ong’o-endelezi [ŋ], hudhihirishwa na ikadhihirika.
Katika
mfumo wa sauti-irabu za Kiswahili Sanifu [a e
i o u ], tunagundua kwamba apana sauti-irabu-ng’ong’o hata
moja baina yao, zote ni sauti-irabu-sing’ong’o. Lakini katika mazungumzo ya
kimtindo, aghalabu hizi sauti-irabu-sing’ong’o huweza kung’ong’oishwa na
msikilizaji akapata hisia ya sauti-irabu-ng’ong’o, kama hivi: [a e i o u ],
yaani wakati wa utamkwaji wa kila irabu kivyake, hewa itokayo mapafuni lazima
itoke n’nje sambamba kwa kupitia chemba ya midomo na tundu za pua, kama Kielelezo
3.25 kinavyoushereheshea.
Hewa hiyo
inayotoka mapafuni, ikipitia chemba ya pua tu au chemba ya pua na chemba ya
midomo bila kusitishwa, basi hisia za sauti itakayotamkwa zitakuwa za
sauti-ng’ong’o-endelezi [a], [e],
[o], [m], [ŋ], nk.,
yaani, sauti za ming’ung’uto. Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejishusha kutoka
kwenye ukuta wa marakaraka (paroi pharangale) ili hewa hiyo ipate kupita na
kutoka nje ya bomba la sauti, bila kusitishwa!
(v) Utamkwaji
wa Sauti za Fonimu za Kiswahili Ki-Mang’ong’o
Utamkwaji
wa Mang’ong’o ya Kiswahili Sanifu [mb]
au [], [nd] au [], [nj] au [], [ng]
au []
Utamkwaji
wa sauti za fonimu za Kiswahili ki-mang’ong’o, ni utamkwaji wa
sauti-fonimu-mang’ong’o [mb]
au [], [nd] au [], [nj] au [], [ng]
au []. Huu ni utamkwaji
wa sauti-ng’ong’o-sendelezi, yaani utamkwaji wa MANG’ONG’O kama
kielelezo3.26 kinavyotushereheshea:
Kila sauti-fonimu-mang’ong’o ni sauti-ghuna, ughuna ambao hujidhihirisha kwenye msitari wa chemba ya
koromeo [KO: ] na hususani
kwenye msitari wa chemba ya pua [PU: ] kama ilivyo katika utamkaji wa sauti-fonimu-ng’ong’o
za kawaida [m n ɲ ŋ],
Kivyake, kila sauti-fonimu-mang’ong’o hutamkwa kama ifuatavyo:
(a) Utamkwaji wa Sauti-Ng’ong’o-Sendelezi [mb] au []
Utamkaji wa sauti-ng’ong’o-sendelezi [mb]
au []
hudhihirishwa katika hatua zifuatazo:
·
alasogezi ya
mdomo-chini inapojikweza na kujibandika kwenye alapahala ya mdomo-juu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao
kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya kutoka n’nje ya Bomba la Sauti.
Wakati kitendo cha hapo juu kinatendeka, kitendo kifuatacho hufanyika:
·
alasogezi ya
kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya pua.
·
mrindimo-ng’ong’o
unapoanza kujidhihirisha kwenye nyufa za chemba ya pua, alasogezi ya
mdomo-chini hujibandua kutoka kwenye alapahala ya mdomo-juu na alasogezi ya
kidaka-tonge hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka;
vitendo vyote hivi vitatu hutendeka wakati mmoja.
(b) Utamkwaji wa Sauti-Ng’ong’o-Sendelezi [nd] au []
Utamkaji wa sauti-ng’ong’o-sendelezi [nd] hudhihirishwa katika hatua zifuatazo:
·
alasogezi ya
ulimi-ncha inapojikweza na kujibandika ndii kwnye alapahala ya ufizi-juu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao
kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya kutoka n’nje ya Bomba la Sauti.
Wakati kitendo cha hapo juu kinatendeka, kitendo kifuatacho hufanyika:
·
alasogezi ya
kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya pua.
·
mrindimo-ng’ong’o
unapoanza kujidhihirisha kwenye nyufa za chemba ya pua, alasogezi ya ulimi-ncha
hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ufizi-juu na alasogezi ya kidaka-tonge
hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka; vitendo vyote
hivi vitatu hutendeka wakati mmoja.
(c) Utamkwaji wa Sauti-Ng’ong’o-Sendelezi [nj]
au []
Utamkaji wa sauti-ng’ong’o-sendelezi [nj]
hudhihirishwa katika hatua zifuatazo:
·
alasogezi ya
ulimi-kati inapojikweza na kujibandika kwenye alapahala ya burutiogumu-mbele
kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya
kutoka n’nje ya bomba la sauti. Wakati kitendo cha hapo juu kinatendeka,
kitendo kifuatacho hufanyika:
·
alasogezi ya
kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya pua.
·
mrindimo-ng’ong’o
unapoanza kujidhihirisha kwenye nyufa za chemba ya pua, alasogezi ya ulimi-kati
hujibandua kutoka kwenye alapahala ya burutiogumu-mbele na alasogezi ya
kidaka-tonge hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka;
vitendo vyote hivi vitatu hutendeka wakati mmoja.
(d) Utamkwaji wa
Sauti-Ng’ong’o-Sendelezi , [ng] au []
Utamkaji wa sauti-ng’ong’o-sendelezi [] hudhihirishwa katika hatua zifuatazo:
·
alasogezi ya
ulimi-nyuma inapojikweza na kujibandika kwenye alapahala ya burutiogumu-nyuma
kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya
kutoka n’nje ya bomba la sauti, (angalia Kielelezo 3.27). Wakati kitendo cha
hapo juu kinatendeka, kitendo kifuatacho hufanyika:
·
alasogezi ya
kidaka-tonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa
utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba ya pua.
·
mrindimo-ng’ong’o
unapoanza kujidhihirisha kwenye nyufa za chemba ya pua, alasogezi ya
ulimi-nyuma hujibandua kutoka kwenye alapahala ya burutiogumu-nyuma na alasogezi
ya kidaka-tonge hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ukuta wa
marakaraka; vitendo vyote hivi vitatu hutendeka wakati mmoja.
Jedwali 3.7 (a): Mfumo wa
Matamshi ya Konsoni za Kiswahili Sanifu
Alasogezi
|
Alapahala
|
Alasogezi-Pahala
|
Kitamkwa/Sauti
|
Mdomo-chini
|
mdomo-juu
|
Midomo
|
[p],
[], [b], [m], [w]
|
Mdomo-chini
|
meno-juu
|
mdomochini-menojuu
|
[f],
[v]
|
Ulimi-ncha
|
meno-juu
|
ulimincha-menojuu
|
[θ], [ð]
|
Ulimi-ncha
|
Fizi-juu
|
ulimincha-
fizijuu
|
[t],
[], [d], [n], [s], [z], [r], [l]
|
Ulimi-kati
|
Burutio-gumu(kaakaa-gumu)
|
ulimikati-burutiogumu
|
[c],
[], [ ɟ], [ɲ], [ʃ], [j].
|
Ulimi-nyuma
|
Burutio-laini(kaakaa-laini)
|
uliminyuma-
burutiolaini
|
[k],
[], [g], [ŋ],
[Ɣ], [w]
|
nyuzi-sauti
(nyuzi-glota)
|
Glota
|
Glota
|
[h].
|
3.2.7
Uhusiano Baina ya Fonetiki na Fonolojia
Sauti-fonimu-irabu na konsoni zilivyojipanga katika mfumo wa
kifonetiki/matamshi ambao unasababisha kuwako tofauti ya maana katika jozi
milinganuo finyu za lugha ya Kiswahili ndio unaotuonesha uhusiano
baina ya fonetiki na fonolojia.
Upo
uhusiano wa karibu sana kati ya taaluma ya fonetiki na taaluma ya fonolojia.
Sifa-bainifu za kifonolojia asili yake iko kwenye sifa-bainifu za kifonetiki.
Kwa mfano, (a) sauti [p] inatofautiana na sauti [b] kwa sifa ya kifonetiki ya u-ghuna; kwamba
[p] ni [ - ghuna] wakati
sauti [b] ni [+ ghuna]; (b) sauti [b] inatofautiana na sauti [k] kwa sifa mbili
za kifonetiki: (i) sifa ya ki-ghuna,
kwamba sauti [k] ni [ - ghuna] wakati sauti [b] ni [+ ghuna]; (ii) sifa ya ki-alasogezipahala, kwamba
sauti [b] ni ki-midomo wakati
sauti [k] ni ki-uliminyuma-burutiolaini.
Sifa hizi
za kifonetiki/matamshi ndizo zinasababisha maana ya neno ibadilike, kwani
badala ya neno kutamkwa [paka]
linatamkwa [baka];
au [bata]
linatamkwa [kata];
nk.
Kwa
mantiki hii, sifa-bainifu za kifonetiki ndizo zinazosababisha kuwako kwa
sifa-bainifu za kifonolojia. Na tunazibaini fonimu (ambacho ndicho kipashio cha
fonolojia) kwazo. Kwa mfano:
(a) pata ~ peta ~ pita ~ pota ~ puta;
Kwa mbinu ya nitoe-nikutoe (commutation), tunadiriki kudai kwamba sauti [a], [e], [i], [o], na [u] ni fonimu /a/, /e/, /i/, /o/, /u/ katika Kiswahili.
(b) yeye
~ wewe; yote ~ wote
Kwa mbinu ya nitowe-nikutowe, tunadiriki kudai kwamba sauti nusu-irabu [j] na [w] ni fonimu /j/ na /w/ katika Kiswahili.
(c) pawa ~ bawa ~ tawa ~ dawa ~ chawa ~ jawa ~ kawa ~ gawa.
Kwa mbinu ya nitoe-nikutoe, tunadiriki kudai kwamba sauti sauti [p],
[b], [t], [d], [c], [ɟ], [k], [g] ni fonimu /p/, /b/, /t/, /d/, /c/, /ɟ/, /k/, /g/
katika Kiswahili.
Hii
ndiyo mbinu kongwe ya kiisimu ambayo inatumiwa na wanaisimu katika utafiti wa
fonimu za lugha yo yote ya binadamu. Na ndiyo mbinu iliyotumiwa kuzigundua
fonimu za lugha, kama vile fonimu za Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, nk.
ambazo tunajifunza katika vyuo vyetu.
MAREJELEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N.
(2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili,
Kidato cha 5 na 6. Aroplus
Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu,
Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu
Hongera sana kwa kutoa mchango mkubwa katika taaluma ya fonolojia ya Kiswahili. Hata hivyo, nakuhimiza uboreshe uandishi wako kwa kufuata kanuni za uandishi na matumizi bora ya uakifishi. Pia, zingatia matamshi ya Kiswahili kwa sababu hapa unafunza watu 'fonolojia' ya Kiswahili. Mfano wa matamshi yasiyo sahihi ni neno 'ufauru'. Matamshi sahihi ni 'ufaulu'.
ReplyDeletenaomba sauti za vidoko, jinsi ya kutamka
ReplyDeleteKiswahili ni kitamu sana kwani kinaelimisha, buludisha na kuikosoa jamii.
ReplyDeleteUtafiti bora wenye maudhui kapambe na wenye kuboresha wanaosoma na wapenzi wa lugha.Heko kwako kwa kazi hii.Nakutakia neema zake Rabuka.
ReplyDelete