VIKWAZO VYA KUJIFUNZA LUGHA YA KISWAHILI
- · KUWEPO KWA LUGHA MAMA:
Lugha mama au
lugha ya kwanza au kama tulivyozoea lugha ya kikabila huleteleza
matatizo katika ujifunzaji wa kiswahili kwa wanafunzi. Tatizo kubwa linalosababisha
na lugha mama ni tatizo la kimatamshi ambalo huweza pia kupelekea tatizo la
kimaandishi. Kwa mfano unaweza kusikia mtu akitamka fyatu badala ya viatu.
- · KASORO ZA KIMAUMBILE.
Athari za kimaumbile au kasoro za kimaumbile huweza
kusababisha vikwazo katika utamkaji wa maneno ya kiswahili kwakuwa kunakuwepo
na matatizo katika mfumo wa ala za sauti za mtamkaji ai mjifunzaji. Kwa mfano
mtu mwenye kithembe hutumia sauti th
badala ya s.
Vilevile kuna magonjwa ambayo huweza kumfanya
mtu kushindwa kutamka baadhi ya maneno kwa usahihi kama vile kiharusi.
- · KUWEPO KWA LUGHA ZA KIGENI.
Kuwepo kwa lugha kigeni katika nchi yetu mfano
kingereza , kifaransa. Huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibu matamshi ya
kiswahili sanifu kutokana na athari za lugha hizo kwa watanzania wengi. Hali hii
husababisha matatizo katika hatua za ujifunzaji wa lugha ya kiswahili kwa watu
wengi.
0 comments:
Post a Comment