SARUFI NA AINA ZA SARUFI:

SARUFI

 ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni za matumizi yake ambayo kwa kawaidahukubalika kwa watumiaji wake. au sarufi ni sheria zinazotawala upangaji wa mofu . mofu ni umbo ambalo linaloweza kutamkwa peke yake katika neno mfano : mtu (m- umoja).


                    AINA ZA SARUFI:
  •  SARUFI MATAMSHI: ni aina ya sarufi ambayo huchunguza sauti mbalimbali zinavyotamkwa na kuathiriana katika lugha mfano: inji -nchi(wachaga). kulingana na lafudhi ya mtu, mtu mwingine akielewa matamshi haya na maana zake, atakuwa ni mwanasarufi.

    SARUFI MAUMBO: ni aina ya sarufi ambayo huchunguza maumbo mbalimbali ya maneno yanayotokea katika lugha yameumbwa namna gani  mfano.: umbo ambalo likidhihiri halibadili maana ya maneno mfano: gali-ghali-tofauti ni h.
     
 
  • SARUFI MIUNDO: katika kiwango hiki tunachunguza jinsi maneno yalivyopangiliwa na jinsi yanavyofuatana katika kuunda sentensi ya lugha inayohusika. mfano: asubuhi sana kununua shambani alikwenda, juma samaki . hiki katika kiswahili muundo wa sentensi unafuata yafuatayo: kn +kt  . mfano huo hapo juu ulitakiwa uandikwe: juma alikwenda kununua samaki sokoni asubuhi sana.
     
  • SARUFI MAANA: ni aina ya sarufi ambayo huchukua maana zilizojikokeza katika lugha. tunachunguza kwanini sentensi zingine zinaweza kuwa sahihi  kisarufi na zingine la! na hii yote inaangalia miundo ya sentensi hizo au maneno hayo yalivyotumika. mfano tungo isiyoeleweka mfano liku akulile pange dikala chande. sentensi hii haieleweki kabisa japo imetumia silabi tunazozifahamu lakini maana hatuielewi, 




Share on Google Plus

About Se

mwiza peter ni mwalimu ambaye alipata taaluma hii chuo cha ualimu morogoro(motco) kwa sasa nipo mwanza Tanzania ni miongoni mwa vijana ambao lengo langu nikukufanya wewe kupata elimu kuhusu somo la kiswahili na kuongeza ufaulu wa somo hili. tupo mwanza Tanzania.karibu mwaa tunawapenda wote.elimu ni ukombozi wa maisha chukua hatua
    Blogger Comment

2 comments: