·
Barua za Kirafiki: Hizi ni barua
wanazoandikiwa wazazi, marafiki, watani na wajuani. Hizi zina uhuru mkubwa
katika kuziandika. Hazidai utaratibu wa
pekee sana. Mtu huwa huru kuandika
upendalo ilimradi halimvunjii mtu heshima yake.
Barua ya aina hii huandikiwa marafiki, na jamii.
Huwa mwandishi anajuli kama kwa wale anaowaandikia kwa hivyo si lazima iwe na
sahihi yake au majina (yake yote) kamili. Kwa kawaida barua hii inaanza kwa
salamu. Huwa ina anwani ya mwandishi peeke. Mwishoni mwandishi huweza hata
kuwatumia salamu watu wengineo anaowajua na wanaomjua.
(i) Muundo
wa Barua ya Kirafiki
Shule
ya Msingi kibo,
Sanduku la Posta 120,
MOROGORO.
Agosti 3, 2005
MOROGORO.
Agosti 3, 2005
Kwa Baba mpendwa,
Ni matumaini yangu kwamba hujambo, tangu
tulipoachana. Je, majirani zetu huko nyumbani huwajambo? Mimi ni mzima, sina
neno.
Madhumuni ya kukuandikia barua hii ni kukuarifu
Maonyesho ya Kilimo ya Wilaya ya Namtumbo. Kila mwanafunzi anahitajika kulipa
shilingi mia moja za kugharamia nauli, chakula na kiingilio. Nakuomba unitumie
pesa hizi tafadhali Baba, ili niweze kuandamana na wenzangu.
Nisalimie Mama, ndugu zangu na wote wanaonifahamu.
Kwa heri kwa sasa.
Ni mimi Kitinda-mimba wako,
Martha.
ZOEZI
1.
Wewe u mwanafunzi katika shule ya bweni. Mwandikie mama
yako barua ya kumjulisha siku ya
kufungwa kwa shule, huku ukimuomba aje kukuchukua kwenda nyambani.
2.
Umefuzu katika mtihani wako. Ndugu yako anayefanya
kazi Nairobi, alikuwa amekuahidi zawadi ,maalum, ukishapita mtihani huo. Sasa
mwandikie barua, umuombe akuletee zawadi.
3.
Umepata habari kwamba rafiki yako alipatwa na ajali ya
barabara. Kwa
sasa amelazwa katika hospital kuu ya Mkoa wa Mashariki. Mwandikie barua ya
kumpa pole na kumtakia apone haraka.
4.
Likizo ya mwisho wa mwaka imekaribia. Mwandikie Baba yako
anafanya kazi katika nchi za mbali. Mwambie akuletee nguo mpya na aje kushiriki
nanyi wakati wa Sikukuu.
5.
U mwanariadha mashuhuri sana. Umechaguliwa
kuiwakilisha shule yako katika mashindano ya Wilaya. Mwandikie barua rafiki
yako, umweleze vile ulivyoshiriki na kupata ushindi katika mashindano ya Kata.
·
Barua za Mwaliko:
Unapoalikwa
kwenye michezo, tafrija, mikutano ya vyama au kwenye midahalo, unaandikiwa
barua za mwaliko yenye sifa kama ifuatavyo:
(i)
Barua hizi sharti ziwe fupi na wazi.
(ii) Zitaje
tarehe, saa na mahali pa kukutania;
(iii) Jina la mwalikaji na anwani yake kamili lazima
itajwe;
(iv) Aidha, jina la mwalikwa na kusudi la mwaliko
na pengine vitu anavyopaswa kwenda navyo inapaswa vitajwe.
·
Barua za kazi na shughuli:
Barua
zinazohusika hapa ni zile za kuomba kazi, kutoa ripoti ya kikazi, shughuli za
kiserikali, kichama na kidini. Katika barua hizi kumbuka:
(i) Kutaja
nambari au/ na tarehe ya barua zinazopaswa kurejewa;
(ii) Kichwa
cha barua na aina ya shughuli unayotaka izingatiwe.
·
Barua ya Kiofisi
(Rasmi)
Barua ya aina hii huandikiwa Maafisa wa Serikali
au Makampuni ya watu binafsi. Kwa kawaida,
maafisa hawa si lazima wamjue mwandishi. Barua rasmi, basi huwa na anwani ya
mwandishi (upande wa juu, mkono wa kulia) na anwani ya anayeandikiwa, upande wa
kushoto. Anwani hufuatiwa na mtajo
– (kichwa cha habari). Barua hii huanza
moja kwa moja, bila salamu.
Ujumbe pekee ndio unaoandikwa. Mwishoni, mwandishi huandika majina yake kamili
(rasmi) na sahihi yake.
(ii) Mfano/Muundo
wa Barua Rasmi:
Shule
ya Msingi kibo,
Sanduku
la Posta 222,
MWANZA
Agosti 3, 2005
Mkurugenzi,
Chama
cha Wakuza Mboga,
Sanduku
la Posta 456,
MWANZA
KUH: UUZAJI WA MBOGA
Ningependa kukujulisha ya kwamba Wanafunzi wangu wa Chama cha MOTCA wamekuza kabichi na
karoti nyingi.
Nakuomba utusaidie katika uuzaji wa mboga hizi ambazo kwa
sasa tayari zimekomaa.
Natumai
utatusaidia uwezavyo.
Ahsante.
Wako
mwaminifu,
(Sahihi)
Nsaji Peter Njarambaya
MWALIMU MKUU
Anwani
Kama mwandishi na mwandikiwa wote wanapatikana
katika nchi moja (Tanzania, Kenya,
Uganda, Zimbabwe, Zambia, Malawi, nk.), basi anwani huandikwa ndani ya barua
kama ifuatavyo:
Shule
ya Msingi kimawe,
Sanduku
la Posta 2222,
moshi.
Agosti 3, 2005
lakini juu ya bahasha, yaani kule inakopelekwa
barua, huandikwa kama ifuatavyo:
Mkurugenzi,
Chama cha Wakuza Mboga,
Sanduku la Posta 56,
NAMTUMBO
Kama mwandishi na mwandikiwa
wote wanapatikana katika nchi tafauti
(anayeandika yuko Tanzania, na
anayeandikiwa yuko Kenya , Uganda , Zimbabwe , Zambia au Malawi, nk.), basi
anwani huandikwa ndani ya barua kama ifuatavyo:
Shule ya Msingi
Mawezi,
Sanduku
la Posta 2222,
MWANZA.
TANZANIA
Agosti 3, 2005
na juu ya bahasha, yaani kule inakopelekwa barua,
huandikwa kama ifuatavyo:
Bwana
Paul Kipruto,
Chama cha Wakulima Langas,
Sanduku la Posta 146,
Eldoret,
KENYA
(iii) Mfano
wa Bahasha
Bwana
Paul Peter Simala,
Chama
cha Wakulima Mumias,
Sanduku
la Posta 123,
Eldoret,
KENYA
·
Barua za
Biashara na Matangazo: Matangazo ya biashara magazetini ni ghali. Kwa hivyo,
barua ziwe fupi na wazi ili zisimpotezee mfanyabiashara muda wake.
·
Simu:
Kuna simu ya mdomo na barua ya simu.
Barua za simu ni fupi sana. Mtu huna fursa ya kueleza mengi au kuzungumza moja
kwa moja na yule unayempelekea taarifa. Isitoshe barua za simu zatarajiwa
kwenda haraka zaidi kuliko barua za kawaida.
Gharama ya kuilipia hukadirwa kwa idadi ya maneno
yaliyoandikwa: maneno mengi, gharama kubwa, maneno machache, gharama ndogo.
Kwa ufupi, kuna barua ya kirafiki (kindugu) na barua
ya kiofisi (rasmi).
Hatua
za Kuangalia katika Barua
Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa wakati wa kuandika barua ni kama
ifuatavyo:
(a) Hatua ya Jumla:
(i) Anwani
ya mwandikaji, ndani ya barua,
(ii) Anwani
ya mwandikiwa iandikwe vema, juu ya bahasha na pengine ndani ya barua pia;
(iii) Tarehe,
(iv) Salamu
(maamkio),
(v) Barua
yenyewe,
(vi) mwisho
wa barua.
(vi) Tumia
karatasi na bahasha safi.
(vii) Juu
ya bahasha ya mtumiwa barua, iwekwe stempu inayostahiki;
(viii) Kama
ni kifurushi, funga kamba kwa umbo la kukatana;
(ix) Iwapo
ni rejesta, chora mistari ya kukatana: moja wa wima na mwingine wa kulala
katikati ya bahasha nyuma na mbele.
(b) Hatua za Pekee:
(i) Katika Barua za Kazi na Shughuli za
Kiserikali:
Licha ya hayo yaliyotajwa katika (a) hapo juu,
·
Andika
kichwa cha barua kinachotaja nia ya barua kwa sentensi
moja fupi kabla ya maelezo ya barua
yenyewe.
·
Barua
nzima iwe fupi na wazi.
(ii) Katika Barua za Biashara:
Pamoja na hayo yaliyotajwa katika (a) hapo juu,
·
Ongeza
orodha ya vitu unavyoagizia.
·
Eleza
jinsi ya kulipia iwapo ni kwa fedha
taslimu, au malipo mara upokeapo vitu
unavyoangiza yaani, (c.o.d }ikiwa na maana ya: (‘cash on delivery’} au
iwapo ni kwa hundi.
(iii) Barua
za Simu
Mambo muhimu yanayotakiwa katika barua za simu ni:
·
Anwani
kamili ya mtu yule unayempelekea simu.
·
Toa
taarifa kwa kifupi na wazi kwa maneno yasiyozidi kumi.
·
Kumbuka maneno yote yanaozidi kumi ya kwanza
utatozwa zaidi.
·
Andika
anwani ya mtuma simu.
·
Malipo
taslimu ya nayotolewa palepale posta.
(iv) Kutuma
Fedha kwa Simu:
Ili
kutuma fedha kwa simu zingatia mambo haya:
·
Lipa
fedha taslimu kwa postamasta ofisini pamoja na ada ya kupelekea hizo fedha.
·
Dai risti
ya kupelekea hizo fedha, nayo uitunze
ili uweze kuitumia kudai pesa zako hizo ikiwa zitapotea.
·
Mwandikie
nduguyo unayempelekea hizo fedha ukimwarifu kwamba umemtumia fedha kiasi
kadhaa, ili atakapoitwa posta na kuulizwa nani amemtumia fedha hizo, aweze
kutaja jina lako na kupewa fedha zake.
(v) Kutuma
Fedha kwa Barua ya Rejesta:
Pamoja na kutumiwa fedha kwa njia ya simu,
kupo pia kupelekewa fedha kwa barua ya
fedha au rejesta. Hapa yafaa
kukumbusha tu kwamba uchukuapo fedha zilizofika kwa rejesta, ifungue bahasha
mbele ya postamasta na kuhesabu kwa uangalifu pesa zilizomo mbele yake, ili
zikipungua au zisipokuwamo uweze kuanza madai mbele yake yeye akiwa shahidi.
(vi) Kutuma
taarifa kwa njia ya Faksi
Pamoja na simu leo kuna teknolojia za kisasa zaidi za
kupashana habari. Nazo ni: Teleprinta,
Teleksi, Faksi na Intaneti.
Kwa mfano, ukitaka kutumia taarifa kwa faksi, njia
ambayo bado inayohifadhi siri kwa kiasi kikubwa, na inayochukua muda mfupi na gharama
ndogo ni faksi.
Unachotakiwa kukifanya
ni
·
Kuandika
taarifa yako kikamilifu kwenye karatasi nyeupe.
·
Kisha
ipitishe hiyo karatasi yenye taarifa yako kwenywe mashine ya faksi ambayo itaituma taarifa yako huko unakotaka iende.
Huko iendako itapokelewa na faksi-mashine nyingine
ambayo itatoa kwa maandishi nakala halisi
(kopi) ya taarifa yako ambayo ataipokea uliyemtumia.
1.
Tarehe
zinaweza kuandikwa kama ifuatavyo:
(a)
3, Agosti, 2005
(b)
3 – 8 – 2005
(c)
3/8/2005
2.
Anwani inaweza kuandikwa kama ifuatavyo:
(a) Shule la Msingi Mbeya,
S.L.P. 343,
MBEYA.
au
(b) Shule ya Msingi MBEYA,
Sanduku la Posta 343,
MBEYA.
MAREJELEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N.
(2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili,
Kidato cha 5 na 6. Aroplus
Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu,
Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu
jiunge nasi bofya hapa ku-install application yetu swahiliform ili usisumbuke kuingia kwenye website yetu
UKURASA UMEPANGWA KIUTAALAMU KWELI ENDELEA NA MWANANGU WA DRS LA V ANAUTUMIA SANA KWENYW SOMO LA KISWAHILI
ReplyDeleteasante kwa maoni yako tutafanyia kazi
DeleteAsante sana kwa saada wako maana mitihani inaanza soon..
ReplyDeletekaribu tena na karibu kwa maswali
Deletemiye ojaka moses kutoka uganda
ReplyDeletemakala haya yamenisaidia sana endeleeni vivyo hivyo
ahsanteni sana
Je, neno Ndugu katika barua ya rasmi laweza kuwa ndio salamu yenyewe au vipi?
ReplyDeleteInsha kuhusu ugonjwa alivyo nasikia
ReplyDelete