Mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili:
(i) Kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu;
(ii) Kigezo cha mofolojia ya mofu.
Tunapotumia kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu, tunapata aina
tatu za mofu, yaani:
(i) Mofu
huru
(ii) Mofu
funge
(iii) Mofu
tata
Kwa upande mwingine tunapotumia kigezo cha mofolojia au maumbo ya mofu
zenyewe tunapata aina mbili za mofu, yaani:
(i) Mofu changamano
(ii) Mofu kapa
Kwa mantiki hii tunazo aina tano za mofu ambazo ni:
(i) Mofu huru
(ii) Mofu funge
(iii) Mofu tata
(iv) Mofu-changamano
(i) Mofu
Huru
Mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno
kamili yenye maana inayoweza kueleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine.
Aghalabu, mifano mingi ya mofu huru hupatikana kutoka kwenye vipashio vya
lugha, kama ifuatavyo:
(a) Nomino: {baba},
{kuku}, {sungura}, {ndege}, {dada}, {paka}, nk.
(b) Vivumishi: {safi}, {baya}, {dhaifu}, {zuri}, {imara},
{hodari}, nk.
(c) Viwakilishi:{mimi}, {sisi}, {wewe}, {ninyi}, {yeye),
{wao}, nk.
(d) Vielezi: {upesi},
{haraka}, {sana}, {leo}, {jana},
{juzi}, nk.
(e) Vitenzi: {tafiti}, {samehe}, {arifu}, {sali}, {jibu}, {badili}, nk.
(f) Vihusishi: {ya}, {juu}, {mbele},
{kwa}, nk.
(g) Viunganishi:{na},{halafu},
{bado}, {ila}, {aidha},{pia}, nk.
Kwa mujibu wa mifano hii inadhihirika kwamba Kiswahili kinazo mofu huru
nyingi ambazo zimo katika aina zote za vipashio vya lugha. Hivyo, mofu huru ni
mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yanayoeleweka bila
kusaidiwa na viambishi.
(ii) Mofu funge au Mofu tegemezi
Mofu funge au Mofu
tegemezi ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa peke yake kama neno lililo na
maana yake kamili; aghalabu mofu funge hutumiwa kama kiambishi tu
kinachoambatanishwa na mzizi au viambishi vingine ili kulikamilisha neno
husika. Mofu funge ina sifa zake ambazo ni pamoja na:
(a) Mofu funge haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili.
(b) Mofu funge ni lazima iambatanishwe na angalau mafu nyingine moja
ndipo tupate neno kamili.
Kutokana
na sifa hii ndiyo mdiyo maana wanaisimu wengine huziita mofu hizi kuwa ni mofu tegemezi ambayo ina maana sawa na mofu funge
Mfano:
Idadi ya Umoja Idadi ya Uwingi
m-toto (m) wa-toto
(wa)
ki-su (ki) vi-su
(vi)
m-ti (m) mi-ti
(mi)
Ukumbwa wa Nomino Udogo wa Nomino
ji-tu (ji) ki-ji-tu
(ki)
ji-su (ji) ki-ji-su (ki)
Maana za mofu funge hutegemea sana muktadha wa mofu funge husika. Mofu
funge ikiondolewa kwenye muktadha wake hukosa maana na ni vigumu kujua maana
yake bila kuiweka katika muktadha wa neno. Mofu funge inaponing’inizwa peke
yake haituwezeshi hata kidogo kujua maana yake. Umbo moja linaweza kuwa na
maana nyingi kwa mujibu wa miktadha ambamo imeambatanishwa katika mzizi wa
neno. Aghalabu, mofu funge ni sawa na viambishi vya mizizi mbalimbali katika
neno. Hii ina maana kwamba viambishi vilivyo vingi katika lugha huwa ni mofu
funge. Tunasema viambishi vingi kwa sababu si viambishi vyote ambavyo huundwa
kwa mofu funge. Vipo viambishi vingine ambavyo huundwa kwa mofu huru. Baadhi ya
mizizi ya maneno pia huwa ni ya mofu funge kwa sababu mizizi hiyo huwa haiwezi
kukaa peke yake ikawa neno kamili. Mifano mizuri ya mizizi ya maneno ya
Kiswahili ambayo huundwa kwa mofu funge ni ile ya vitenzi vya silabi moja moja,
kama ifuatavyo kwa mfano:
Mofu funge Neno Mofu
funge Neno
{l-) kula {-p-} mpe
{-j-} kuja {-ny-}
kunya
{-f-} kufa {-nyw-} kunywa
{a} +
{me} + {m}
+ {nyw} +
{esh} + {a}
amemnywesha
Mizizi ya vitenzi hivi ni mizizi ya mofu-funge kwa sababu haiwezi
kutumiwa peke yake kama neno na, pia maana zao huwa hazijitokezi mpaka mizizi
iwekewe viambishi.
(iii) Mofu Tata
Mofu tata ni mofu ambazo huwa na maana zaidi ya moja au kuanzia mbili
na kuendelea.
Mfano:
Saidi alimpigia Mbaraka mpira.
Sentensi hii ni tata kwa sababu ina maana zaidi ya moja. Utata wa sentensi hii haupo kwenye muundo
wake wa kisarufi, bali upo katika kitenzi alimpigia. Kitenzi hiki kina mofu sita, yaani:
{a-} + {-li-} + {-m-} + {-pig-} + {-i-} + {-a}
1 2 3 4 5 6
Kati ya mofu hizi zote sita, mofu ya tano {-i-} ndiyo yenye utata. Mofu
{i} ni mofu ya kutendea kwa sababu tukisema: ‘Saidi alimpigia Mbaraka mpira’, maana zinazoweza kueleweka na
wasikilizaji ni nne:
(a) Saidi
aliupiga mpira kwa niaba ya Mbaraka; yaani Mbaraka ndiye aliyetakiwa aupige
mpira ule, lakini kwa sababu ambazo hazikuelezwa, badala ya Mbaraka kuupiga
mpira ule, Saidi akaupiga.
(b) Saidi aliupiga mpira kuelekea kwa Mbaraka; yaani Saidi na Mbaraka
walikuwa wakicheza mpira. Ikapatikana fursa, Saidi akaupiga mpira ule kuelekea kwa
Mbaraka. Kwa hiyo, hapa tunazungumzia mwelekeo wa mpira.
(c) Saidi alimpiga Mbaraka kwa kuutumia mpira; yaani, Saidi anautumia
mpira kama ala (silaha) ya kumpigia
Mbaraka.
(d) Saidi
alimpiga Mbaraka kwa sababu ya mpira; yaani hapa, mpira ndio sababu kubwa ya
Saidi ya kumpiga Mbaraka. Tuseme labda Saidi alikuwa na mpira wake, halafu
Mbaraka akauchukuwa kuuchezea na kwa bahati mbaya akaupoteza. Saidi anapogundua
kwamba Mbaraka ameupoteza mpira wake, basi ndipo akampiga.
Kwa maelezo hayo, ni wazi kwamba sentensi yetu ina utata kwa kuwa
inatupatia maana tofauti tofauti zipatazo n’ne ambazo zimesababishwa na mofu
{-i-} ya kutendea.
(iv) Mofu Changamani
Mofu changamani ni mofu ambazo huundwa kwa kuweka pamoja angalau mofu-sahili
mbili au mofu funge na mofu sahili yakafanyiza neno lenye kuleta maana kamili,
kwa mfano:
Mofu sahili + Mofu sahili
(i) {askari} + {kanzu} =
askari kanzu.
(ii) {gari} + {moshi} =
gari moshi.
(iii) {paka}
+ {shume} = paka shume.
(iv) {m’mbwa} + {mwitu} =
m’mbwa mwitu.
(v) {fundi} +
{chuma} = fundi chuma.
nk.
Mofu funge +
Mofu huru
(i) {mw} + {-ana}+ {nchi} = mwananchi.
(ii) {ki} + {-on-} +
{a} + {mbali}= kiona mbali.
(iii) {mw} +
{-ana}+ {hewa }= mwanahewa.
nk.
(v) Mofu Kapa
Mofu kapa ni mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi
wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno, lakini athari zinazotokana
na hiyo mofu kapa husika hueleweka. Ingawa mofu hizi huwa hatuzioni wala
kuzitamka au kuziandika, lakini maana zake tunazipata. Tukichunguza ruwaza ya
viambishi awali vya umoja na wingi katika lugha ya Kiswahili, tunaweza kuzigawa
nomino za Kiswahili katika makundi makuu man’ne, yaani:
(a) Nomino zilizo na viambishi bayana vya idadi ya umoja na uwingi:
Mfano:
Umoja Wingi
m - tu wa - tu
m - toto wa - toto
m - ti mi – ti
nk.
(b) Nomino
zilizo na kiambishi awali cha umoja tu, cha wingi hakipo, kwa hivyo, ni kapa (φ)
Mfano:
Umoja Wingi
u - kuta φ - kuta
u - funguo φ - funguo
u – kucha
φ – kucha.
nk.
(c) Nomino zilizo na kiambishi cha wingi tu, cha
umoja hakipo; kwa hivyo, ni kapa (φ)
Mfano:
Umoja Wingi
φ – kasha ma
– kasha.
φ – debe ma
– debe.
Φ – jembe
ma - jembe
nk.
(d) Nomino zisizo na
kiambishi awali cha umoja wala cha wingi
Mfano:
Umoja Wingi
Φ - mama Φ - mama.
Φ - ng’ombe Φ - ng’ombe.
Φ - baba Φ - baba.
Φ - kaka Φ - kaka.
Φ - dada Φ - dada.
Φ - mbuzi Φ - mbuzi.
Φ - ngamia Φ
- ngamia.
Φ - kondoo Φ - kondoo.
Φ - tembo Φ - tembo.
Φ - sungura Φ - sungura.
Φ - nguruwe Φ - nguruwe.
Φ - simba Φ
- simba.
nk.
(e) Sherehe kuhusu Mofu kapa
Katika kuonyesha mofu kapa tutatoa sherehe kuhusu kundi la 1.2.5.3 na
la 1.2.5.4. Katika kundi la 1.2.5.3 nomino zina kiambishi awali cha umoja tu,
wakati cha wingi hakipo. Kinachotokea hapa ni kwamba ukisema ukucha watu
wanaelewa kuwa ni ukucha mmoja tu. Lakini ukisema kucha, watu wataelewa kuwa ni kucha nyingi.
Na hali hii ndivyo ilivyo kwa maneno ufunguo ǂ funguo; ukuta ǂ kuta, nk. inajulikana kuwa ni ufunguo mmoja
tu na akisema funguo, ni kwa maana ya wingi; lakini umbo lenyewe linaloileta hiyo maana ya wingi
halionekani bayana katika neno.
Ili kuyaeleza haya maumbo ambayo hayapo lakini maana zinazowakilishwana
maumbo hayo zipo, Wanaisimu wamekubaliana kuyaita maumbo haya kapa, yaani mofu ambazo hazipo. Mofu
hizi ni dhahania tu katika
akili zetu kwa kufahamu tu kwamba maana fulani haiwezi kuja tu yenyewe lazima
iletwe na mofu fulani. Kwa hivyo, hata kama mofu hiyo haionekani, lakini ipo;
ni mofu-kapa.
Kwa mfano, katika matamshi ya maneno: kasha, debe, jembe, umoja na
uwingi wake hudhihirishwa kama ifuatavyo:
Umoja Uwingi
kasha makasha
debe madebe
jembe majembe
Katika nomino hizi mofu ya uwingi ni mofu {ma}
lakina mofu ya umoja ni mofu kapa,
yaani haipo na huoneshwa kwa alama {Φ}.
Kwa mantiki hiyo, mofu za maneno haya ni kama ifuatavyo:
Umoja Uwingi
{Φ} + kasha {ma}
+ {kasha}
{Φ} + debe {ma}
+ {debe}
{Φ}+jembe {ma} + {jembe}
MAREJELEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N.
(2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili,
Kidato cha 5 na 6. Aroplus
Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu,
Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
leksimu inaweza kuwa neno si kila leksimu ni neno wala kila neno sio leksimu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
kazi nzuri ya kusaidia
ReplyDeleteasante kwa maoni yako karibu tena kwa maswali na usauli
DeleteVizuri sana kwa nazi nzuri
ReplyDeleteasante karibu tena
Deletehogera ustadhi kazi zuri hiyo imenisaidia kupata umilisi wa lugha katika mofolojia juu ya mofimu kapa
ReplyDeleteasante kaka karibu tena tunaomba uwataarifu wengi huwepo wa swahili form blog waweze kupata elimu
Deletehongeara ustadhi umenisadia sana umilisi unao
ReplyDeleteasante karibu tena
Deletehongera sana umilisi unao
ReplyDeleteasante kaka karibu tena tunaomba uwataarifu wengi huwepo wa swahili form blog waweze kupata elimu
Deletenilikua nataka ufafanuz juu ya dhana ya leksimu.
ReplyDeleteCystal (1980) anaelezea kuwa leksimu
Deleteni kipashio dhahania kinacho wakilisha maumbo kadhaa yanayotokana nacho.
Kwa mfano;
refu – ndefu, mrefu, kirefu
baya- baya, mbaya, wabaya
nashukulu sana kwa notice
ReplyDelete